Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt. Wilbald Lorri (pichani) kuwa Msaidizi wa Rais, Masuala ya Lishe (Nutrition).
Taarifa iliyotolewa leo, Jumatano, Julai 18, 2012 na Ofisi ya Katibu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue, kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inasema kuwa uteuzi huo wa Dkt. Lorri ulianza tokea Juni Mosi, 2012.
Kabla ya uteuzi wake, Dkt. Lorri ambaye ana shahada ya uzamivu (PhD) katika Sayansi ya Lishe alikuwa mtaalam wa lishe katika Mradi wa Feed the Future unaoendeshwa nchini na Shirika la Maendeleo la Marekani - USAID.
Aidha, kati ya mwaka 1994 na 2003, Dkt Lorri alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Lishe Tanzania – (Tanzania Food and Nutrition Centre).
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
18 Julai, 2012
The guy needs to diet.
ReplyDeleteHahaha mkuu wa Nutrition lakini ukiangalai afya mmmhh... Ila wadau sijaelewa hii nafasi yaani ni mshauri wa diet ya Raisi au Lishe ipi? Natanguliza shukrani.
ReplyDeleteAisee!!! Mungu ni mwema,naamini utafanya yale uliyokuwa ukiyafanya lishe, nimeamini mungu kweli akitaka lake linakuwa, waliofanya majungu, fitina na umbea wako wapi kina ndossy sasa, aibu kwao! Keep it up Baba.
ReplyDeleteLishe kwa vitendo!
ReplyDeleteHujakosea kumteua mpambanaji.....mtu wa watu kisha mpiga kazi! Dr. Lorry kapige kazi nakuaminia kaka!
ReplyDeletenimefurahishwa sana na uteuzi wa huyu mbaba, ni mchapakazi sana na mpenda haki ila walimpiga majungu mengi sana alipokuwa tfnc, ila ndio hivyo sasa kauchinja....
ReplyDeleteHongera sana Dr Lorri umetufanyia kazi nzuri sana feed the future ubarikiwe tunaamini utaendelea kuwa mpambanaji wetu
ReplyDelete