Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh.Abbas Kandoro (kushoto) akimkaribisha Tanzania Waziri wa Maendeleo ya Maji na Umwagiliaji wa Malawi Mh. Ritchie Bizwick Muheya (kulia) alipowasili Kasumulu mpakani mwa Tanzania na Malawi kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Uzinduzi Rasmi wa Miradi ya maendeleo ya Bonde la mto Songwe uliofanyika Wilayani Kyela Jumatatu wiki hii.
Waziri wa Uchukuzi Mh Harrison Mwakyembe (kushoto) akiwa na Waziri Maendeleo ya Maji na Umwaliaji wa Malawi Mh.Ritchi Bizwick Muheya (kulia) baada ya kukata utepe na kuangalia Ramani ya Mardi huo Mh Harrison Mwakyembe alizindua Mradi huo kwa niaba ya Waziri wa Maji Mh. Prof. Jumanne Maghembe.
Waziri wa Maendeleo ya Maji na Umwagiliaji wa Malawi Mh Ritchie Bizwick Muheya akitoa hotuba katika uzinduzi wa Mradi wa Maendeleo ya Bonde la mto Songwe mjini Kyela wanzoni mwa wiki.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Eng. Christopher Sayi (kushoto) akiwa na mazungumzo ya pamoja na mwakilishi wa Masuala ya Maji katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) Bw.D.Verdeil (kulia) wakati wa uzinduzi wa Miradi ya Maendeleo ya Bonde la Mto Songwe Kyela Jumatatu wiki hii. Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa kushirikiana na Serikali za Tanzania na Malawi imetoa msaada wa kifedha karibu Euro Milioni 3 kufanikisha mradi huu.
Picha ya pamoja baada ya Uzinduzi wa Mradi wa Maendeleo ya Bonde la mto Songwe.
Wanahabari nao hawakuwa nyuma kupata taarifa ya Mradi.Mwakilishi wa TBC1 Mbeya Hosea Cheyo akizungumza na Meneja Mkuu wa Mradi huo Eng. Saidi Abbas Faraji (kushoto) kuhusu mikakati ya uendelezaji wa mradi huo.
Mto Songwe kushoto kwako ni Malawi na kulia ni Tanzania. Moja ya miradi itakayotelezwa ni kudhibiti mafuriko ya mto huu ambayo husababisha hasara kubwa na kugeukageuka kwa mpaka kila yanapotokea mafuriko.Picha zote na Nurdin Ndimbe Wizara ya Maji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...