Hapa karibu na njia panda ya Kunduchi. Baada ya muda wadau waliondoka Dar muda mrefu uliopita wakija nyumbani watakuta mabadiliko makubwa kwenye barabara hii na nyingine kibao ambazo foleni zake ni za kufa mtu kutokana na ufinyu wa barabara
Maeneo ya Kunduchi karibu na pale wanapochimbaga kokoto za kujengea
Maeneo ya Tegeta njia panda ya Wazo Hill
Daraja karibu na kufika Tegeta kituoni
Barabara ya Bagamoyo Road!! Duh
ReplyDeleteAnachonifurahisha mkandalasi huyu ni kutambua na kutunza miti. Ameweza kuacha miti mingi barabarani iendelee na maisha yake hasa eneo la Africana hadi Mbuyuni.
ReplyDeleteHongera sana kwa jambo hilo
Bagamoyo Road (in English) au Barabara ya Bagamoyo (kwa lugha yetu ya Taifa), vyovyote vile ni fasaha kabisa na inajitosheleza. Haya mazowea ya kusema au kuandika "Barabara ya Bagamoyo ROAD" ndio hizo lugha gongana na hatimae zinakuwa mazowea yetu. Kila la kheri katika shughuli nzima za ujenzi wa barabara hiyo.
ReplyDeleteMichu,good job.Please zidi kutuletea taswira za barabara,hii inakoga mioyo ya watu sana hasa hasa waliolowea nchi za mbali na kwa miaka mingi hawajarudi bongo . pia nachukua nafasi hii kukuomba unitangazie kwa wanablog kwamba ,nina mashine za kuprinti picha kwenye vikombe na (mag) zake (vikombe) vyake kama elfu moja hivi,naomba mjasiliamali aje tuonane nimuuzie. email yangu ni jacobmayillah@hotmail.ca.
ReplyDeletemichuzi nakuomba sana kaka yangu utuwekee kituo cha mabasi cha hiyo barabara alafu utuwekee na kituo cha moroko kwa pamoja halafu uangalie vina fanana?mimi sijapenda wameweka kituo vibaya sasa magari yata simama vipi kipaa chenyewe kifupi basi litakwangua kianguke,nafasi ndogo halafu hakuna mchepuko hiyo ni hiway.unaweza simama unapakia abiria unagongwa kwa nyuma sababu haijulikani umesimama au unakwenda ni mbaya sana.nenda kaone mwenyewe utaelewa ninachokueleza.utatusaidia sana labda kwa namna yeyote mdau wa kunduchi.
ReplyDeleteBarabara ya bagamoyo road! badilisha hiyo statement please!
ReplyDeleteNi vizuri sana kuongeza road, Je usalama wa wananchi utaendana na barabara mpya, hivi sasa hatuna barabara lakini tunachinjana kwa ajari ,je zikamilika itakuaje?naomba serikali ilitazame hilipia
ReplyDelete