Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Jan Eliasson akisaini kitabu cha Maombolezo ambacho kimefunguliwa katika Ubalozi  wa  Kudumu wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania katika Umoja wa  Mataifa.  Katika Salamu zake, Naibu Katibu Mkuu ameelezea kuguswa kwake na tukio la ajali  ya kuzama kwa meli  na  hasara iliyotokana na ajari hiyo ikihusisha pia kupotea kwa maisha ya watu. Mhe. Jan Eliasson ni miongoni mwa wanadiplomasia ambao wamekuwa wakifika kutoa salamu zao za pole na kuungana na watanzania katika kipindi hiki cha majonzi.
Naibu Katibu Mkuu  wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Jan Eliasson akizungumza na Kaimu Balozi, Dkt. Justin Seruhere mara baada ya kusaini kitabu cha  maombolezo ambapo   alielezea  namna gani anavyoifahamu Tanzani na mapenzi yake makubwa kwa nchi hiyo  na kwamba ni kama miaka miwili tu iliyopita alikuwa Kisiwani Zanzibar.   Katika salamu zake za pole  Mhe.  Elliasson amesema sala na dua zake anazielekeza kwa wahanga wa tukio hilo,  Serikali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na kwamba Umoja wa Mataifa uko pamoja na watanzania katika  kipindi hiki kigumu.

Na Mwandishi Maalum
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Mhe. Jan Eliasson ametoa salamu za pole kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na  Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kufutia ajali ya kuzama kwa  meli iliyotokea hivi karibuni.
Katika salamu zake ambazo amezitoa wakati akisaini kitabu  cha   maombolezo kilichofunguliwa katika Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  Naibu Katibu Mkuu amesema, ameshtushwa na kuguswa  sana na taarifa za tukio la kupinduka na hatimaye kuzama kwa meli, tukio ambalo limesababisha kupotea kwa maisha ya watu.
 “ Ninapenda kutoa salamu zangu za dhati kwa  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania  na Serikali ya  Mapinduzi ya Zanzibar  na wananchi wa pande zote mbili.  Nimeguswa sana na taarifa hizi, sala na dua zangu zinakwenda kwa wahanga wote wa  tukio hili.  Mimi Binafsi na Umoja wa Mataifa tupo pamoja nanyi katika kipindi hiki kigumu ”  Amesema Naibu Katibu Mkuu.
Katika mazungumzo yake na  Kaimu Balozi, Dkt. Justin Seruhere  mara baada ya kusaini kitabu, Mhe. Jan Eliason amesema anaifahamu vema Tanzania na   kwamba miaka miwili  iliyopita alikuwa Kisiwani Zanzibar.
“ Ninaifahamu  vizuri sana Tanzania,  nimefanya kazi kwa karibu sana na Dkt. Salim Ahmed Salim, bado ninakumbukumbu nzuri sana za Tanzania. Na nililikuwa kisiwani  Zanzibar kama miaka miwili hivi iliyopita. Kwa kweli tukio hili limenigusa sana”. Akasema  Naibu Katibu  Mkuu raia wa Sweden ambaye aliteuliwa hivi karibuni kushika nafasi iliyoachwa na Dkt. Asha-Rose Migiro.
 Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa   ni miongoni mwa wanadiplomasia ambao wamekuwa wakifika hapa Ubalozini  kutoka salamu zao za pole kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar na kwa Watanzania wote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 21, 2012

    hahahaha picha hiyo nimeipenda sana kunta kinte bwana wana mambo kweli kweli

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...