Katika miongoni mwa vipaumbele nane vilivyounda kifupi cha AMUA katika kampeni zangu mwaka 2010 ni suala la ULINZI katika Jimbo zima la Ubungo.
Nashukuru leo 30.06.2012 kwa ushirikiano wa wadau mbalimbali tumezindua Ujenzi wa kituo cha polisi katika kata ya Sinza.

Natanguliza shukrani zangu za dhati sana kwa wananchi ambao tumeshirikiana katika mchakato huu, Diwani wa Kata ya Sinza, Renatus Pamba, Mstahiki Meya, Yusuph Mwenda (ambaye ameahidi Manispaa ya Kinondoni itatoa Sh milioni kumi (10) kuchangia Ujenzi).Hii ni baada ya kuhamasishwa na Mbunge na Diwani baada ya Sh Milioni Kumi (10) nyingine kutolewa katika mfuko wa kuchochea maendeleo ya jimbo (CDCF)
Maslahi ya Uma Kwanza.
John John MNYIKA
Mbunge wa Jimbo la Ubungo (CHADEMA)
30 Juni 2012
Kwani Mheshimiwa Mnyika na wewe unahitaji polisi? Si ndio yule yule mpinzani mkubwa wa juhudi zao za kulinda usalama wa raia na mali zao katika sehumu mbali mbali nchini? Tuachane na unafiki jamani.
ReplyDeletemdau wa kwanza ebu jieleze vyema husomeki
ReplyDelete