Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi- Zanzibar

ZANZIBAR JUMAMOSI JUNI 21, 2012. ZAIDI ya wafuasi 40 wa kikundi cha Jumuiya ya Uamsho Zanzibar wamekamatwa na Polisi kufuatia vurugu zilizotokea jana kwenye eneo la Darajani mjini Zanzibar.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar ACP Aziz Juma Mohammed, amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa baada ya kufunga barabara kadhaa kwa mawe, vyuma, matofari na kuchoma moto matairi ya magari.

Kamanda Aziz amesema kuwa katika vuurugu hizo hakuna Askari ama watuasi wa kikundi hicho waliofariki ama kujeruhiwa wakati wa ghasia hizo zilizokuwa nimeendelea katika mitaa mbalimbali ya mji wa Zanzibar.

Amesema wafuasi hao walitumia mawe, chupa na vipande vya mbao kuwarushia Polisi lakini amesema hadi kumalizika kwa zoezi la kuwatawanya wafuasi hao saa nane usiku wa kuamkia leo, (jana).

Hata hivyo Kamanda Aziz amesema bado Jeshi la Polisi linaendelea kuwasaka viongozi wa kikundi hicho ambao wametoroka mara baada ya kuibuka kwa vurugu hizo.

Amesema vurugu hizo ambazo zilianza jana majira ya saa 11.00 jioni, zilidumu hadi saa 8.00 usiku kufuatia wafuasi wa kikundi hicho kujikusanya katika maeneo mbalimbali wakifanya vurugu.

“Tunawatafuta viongozi wa kikundi hicho na tunawataka popote walipo wajitokeze na kujisalimisha wenyewe Polisi.” Alisema Kamanda Aziz.

Mara baada ya kuanza kwa ghasia hizo na hadi asubuhi ya leo (jana) barabara za Darajani na mlandege, mitaa iliyokuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu, ilikuwa haia hata mtu mmoja na hata biashara zilisimama.

Hata hivyo biashara mbalimbali zimerudia tena katika hali yake ya kawaida huku watumishi wa Baraza la Manispaa ya mji wakiendelea na kazi ya uongoaji wa mawe, matofari na mabaki ya majivu ya matairi ya magari.

Ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa Polisi endapo watawaona ama kubaini mahala walipojificha viongozi wa kundi hilo la uamsho ili wahojiwe kwa tuhuma za kuanzisha ghasia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2012

    Jamani hawa uamsho si wa kupuuzwa.

    Isidhaniwe kuwa siku zote hayo mabomu ndio yatakayokata kiu na adhma ya mikutano na maandamano yao.

    Madai yao yaweza kua ni ya msingi iwapo mtazamo wa wanaopelekewa madai hayo utalenga kuwaskiliza.

    Polisi wanajengewa uadui mkubwa na wanajumuiya hao kwasababu wao wanatekeleza amri za wakubwa wao.

    Ipo siku polisi watachoka na wataacha wananchi wafanye wanavyotaka.

    Uongozi na mamlaka husika chukueni hatua madhubuti kusaidia hilo.

    Polisi wapo hatarini.

    mdau -ZNZ

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 22, 2012

    Huo ni uonevu tu na kutumia mabavu na nguvu ya unyanyasaji!Ebu waacheni watu wawe huru waseme wanachokitaka,kwanini mnaendesha siasa ya kibeberu?Kila wakitaka kuandamana mnawazuia, kwanini lakini?Hiyo siyo demokratik ni komunist!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...