Taswira za kunguru wenye baka jeupe kifuani katika mji wa Chalinze mkoa wa Pwani leo. Siku hizi kunguru wa aina hii wamepotea sana hususan mijini na badala yake kunguru weusi wametawala kila kona na kuleta kila aina ya kero, ikiwa ni pamoja na kukwapua kila aina ya vitu. Mwenye data zaidi tunaomba msaada tutani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2012

    ao kunguru hapa Songea wapo kibao. Hawana fujo kama wale wause mwili mzima.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 22, 2012

    Wameathiriwa na muungano

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 22, 2012

    Ngege anayejua kutumia ubongo wake!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 22, 2012

    Hata hapa katika eneo la Kwembe Maduka Matatu wapo bali wale washenzi nao wameishafika hivyo nivurugu tupu. Hawa wenye baka jeupe wamebaki kama saba hivi

    Observer

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 23, 2012

    Kunguru hafugiki!.Hawa wenye baka jeupe,Daresalaam wamekuwa adimu.Watu wa fani hii watatusaidia

    David V

    ReplyDelete
  6. Hao kunguru wenye 'vizibao' vyeupe, baadhi unaweza kuwaona sehemu za Dodoma. Ila wale weusi afiriti, wamejazana tele Zanzibar, enzi hizo ilifikia wakati wakawa wanafanyiwa 'usasi' kwa kero na bughudha zao, wanaweza kukukwapulia mpaka 'baraghashia' yako kichwani, hawana woga wala kusikia.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 23, 2012

    Unawatafuta umetumwa na mganga?! Nitakuletea tenga zima kwa basi ukiwahitaji!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 23, 2012

    Huyu kunguru wa Bara. Wale weusi tunaita kunguru wa Zanzibar. Kwa hiyo njoo bara utawaona kibao tu.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 23, 2012

    Pia wanapatikana kisiwani Pemba hususan maeneo ya mkoani. Kunguru hawa ni 'wapole sana' kulinganisha na wale weusi wasio na mabaka. Wale weusi hata 'kapelo' uliyovaa wanaipora na kutimka nayo!!, we acha tu

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 23, 2012

    Kunguru hawa waliathiriwa na uzuzu wetu wa kudandia mambo hovyo bila kufikiri. Kunguru weusi waliletwa ati kulisafisha jiji la Dar. Hivi mtu na akili zako timamu ukamtegemee ndege kukusafishia mji? Sisi kila tunaloambiwa na mzungu tunakubali tu. Kunguru hawa walikuwa nanaleta mandhari nzuri jijini kwa rangi zao. Hata milio yao ilikuwa maarufu kabisa. Hivi sasa jijini wamejaa kunguru hanithi wale wa kiZanzibari ukishika kitumbua anakupora, bah! Ingekua uwezo ninao ningaliwaulia mbali wote,nirudishe kunguru wetu wa kijambakoti.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 23, 2012

    Sehemu yenye kunguru hawa wenye baka jeupe wakiingia wale weusi kamili, wenye baka huisha kwa sbb hawa weusi hula mayai ya ndege wa aina zote na hivyo huenda kwenye viota vya hao wenye baka na kula mayai yao. MBAYA SANA.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 23, 2012

    Sio kapelo tu mdau wa hapo juu, sifa moja kubwa ya kunguru hawa weusi ni wapenzi sana wa chupi za akina dada zinapoanikwa. Inasemekana kinachowavutia ni ile harufu inayovutia ya kinachositiriwa ndani ya chupi hizorespoap, heheheheh!!!!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 23, 2012

    Wenye baka jeupe ka huyo wapo Iringa wengi sana kama ilivyo dar kwa wale weusi kabisa, ila hawa wanabusara sana tena husaidia kuondoa sana sana ule uchafu ulooza, mfano mnyama kama paka, mbwa, na ndege wakifa wao hunyofoa kidogo kidogo nyama yao mpaka waisha inabaki mifupa tu

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 23, 2012

    Wewe mdau wa 9:58 kasome historia vizuri. Kunguru hao walikuwa introduced Zanzibar (na siyo bara) kwa kazi ya kusafisha mizoga. Hiyo ni karne ya 19 walipoletwa Zenji kwa kazi hiyo.

    Nani aliwaleta huku Bara? Nadhani wanao uwezo wa kusafiri na kwenye miaka ya sabini ndiyo wameanza kuonekana.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 23, 2012

    pemba wako wa kumwaga kama mganga wako anahitaji niambie nije nao kwa mtubwi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...