Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk Ramadhani Dau akipeana mkono na Bernadeta Kaiza ambaye aliyefika katika banda la NSSF kutoa ushuhuda wake pamoja na kuishukuru NSSF kwa kugharamia safari ya kusafirisha mwili wa marehemu mume wake (BOFYA HAPA) ambaye alikuwa mwanachama wa NSSF WESTADI aliyefariki nchini ns kusafirishwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kutoka marekani mpaka Tanzania kwa ajili ya mazishi.
Mkuu wa Uhusiano na Hudumna kwa Wateja wa NSSF, Eunice Chiume akitoa maelekezo kwa Wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi walipotembelea Maonyesho ya 36 ya Biashara ya Kimataifa Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi walipofka katika banda la NSSF katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa jijini Dar es salaam.
Mtanzania anayeishi nchini Marekani, Bi. Bernadetta Kaiza ametoa wito kwa watanzania wanaoishi ughaibuni kujiunga na mafao ya Welfare Scheme for Tanzanian Diaspora (NSSF WESTADI) huduma ambayo itamuwezesha mwanachama kupata huduma ya kusafirishwa kutoka nchi husika mpaka nyumbani Tanzania pindi anapofariki.
Akizungumza katika banda la NSSF mbele ya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Taifa la hifadhi ya Jamii (NSSF) waliofanya ziara katika Maonyesho ya 36 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam alkisema: "Kujiunga NSSF WESTADI kutasaidia mwanachama kugharamiwa safari ya kusafirisha mwili kutoka nchi yoyote mpka Tanzania na kuondokana hali ya kuchangihana fedha pindi mmoja wetu anapofariki."
"Wakati mwingine tunashindwa kusafirisha mwili kutokana na kukosa fedha lakini kwa kupitia huduma hii ya NSSF WESTADI sasa matatizo ya muda mrefu tuliyokuwa nayo sasa yatakwisha endepo watu wengi watajiunga na huduma hii kutokana na gharama zote za mwanachama kugharamiwa na NSSF, aliongeza Bi. Bernadeta Kaiza wakati akiishukuru Bodi ya Wakurugenzi wa NSSF kwa kufanikisha safari ya kuja Tanzania pamoja na mwili wa marehemu mume wangu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk Ramadhani Kitwana Dau amesema kuwa ili kujiunga na mafao hayo mwanachama anatakiwa kutoa ada ya uanachama ambayo ni Dola za Marekani 300 kwa mwaka na fomu zinapatikana katika mtandao wa NSSF.


Kwahiyo watanzania wenye uraia wa nchi za nje pia wanaruhusiwa kununua hizi huduma?
ReplyDeleteNdiyo unaruhusiwa, kwasababu uraia wako uliopata nje ni wakuandikshwa na siyo wa kuzaliwa, kwahiyo hata siku moja uraia wa kuzaliwa hautashindwa kuwa na nguvu, au kwa maneno mengine, baba yako aliyekuzaa, hawezi kubadilishwa hata kama umenunuliwa na familia nyingi, ambayo kwasababu moja au nyingine hawana mtoto wakaamua kukuchukua wewe na baba yako akakubali kwasababu yoyote ile(umasikini or so), bado baba ni baba yako, ndo maana tunauraia wa kigeni lakini tukifa eti tunarudi Tanzania kwanini, nijibu wewe sasa.
ReplyDeleteSwali lako ni zuri sana mdau namba moja, kaka michuzi tusaidie tupate jawabu kuhusu swala hili, maana tunawatoto wetu ambao hawana urai wa Tanzania lakini ni watazania kwa damu.
ReplyDeleteHuyu mdau namba bili, inaonekana ana hasira na wenye asili ya Tanzania ila hawana uraia wa Tanzania, mdau wa tatu kaeleza vizuri,sio lazima nibadilishe mimi uraia ila watoto wetu tumewapatia huku na kabla ya process zingine hazifuatia tungehitaji kujua kama tunaweza kunufaika na mpango wa NSSF
ReplyDelete