Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki,Mhe. Shy-rose Bhanji akizindua rasmi katalog ya ORIFLAME maalum kwa mwezi Julai hadi Oktoba.Katikati ni Meneja mauzo wa ORIFLAME Bi. Fortunata Nkya na Kulia ni Mmoja wa viongozi wa ORIFLAME Bw. James.
 Meneja mauzo wa ORIFLAME Bi. Fortunata Nkya akitoa maelezo mafupi kuhusu kampuni hiyo kwa wageni, kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi.

Kampuni ya ORIFLAME inayojishughulisha na kutengeneza vipodozi yenye makao yake makuu nchini Sweden, imezindua bidhaa mpya zitakazouzwa nchini kwa kupitia wasambazaji na wanachama wake.

Bidhaa hizo za ORIFLAME zinatengenezwa kwa kutumia matunda, maua na mimea mbali mbali inayoweza kusaidia ngozi kuwa katika hali bora na vilevile kukinga na kutibu maradhi mbalimbali ya ngozi.

Katika hafla hiyo watanzania wameshauriwa kutumia bidhaa za ngozi zinazotengenezwa kwa kutumia malighafi halisi ili kuboresha na kuimarisha muonekano wa ngozi zao na kuepuka madhara yatokanayo na kemikali.

Mgeni rasmi wa hafla hiyo ya uzinduzi Mhe. Shyrose Bhanji ambaye ni mbunge wa bunge la Afrika mashariki, amewasihi watu kupenda na kuthamini ngozi zao kwa kutumia bidhaa zisizokuwa na kemikali zenye kuleta madhara.

Aidha pia amewashauri watanzania wajiunge na biashara hii ya mtandao ambayo itawaingizia kipato kwa wingi na vile vile wataweza kutunza urembo wao wa asili kwa kutumia bidhaa wanazoziuza ambazo wao hupata kwa bei ya punguzo tofauti na wateja wasio wanachama.

Bidhaa ambazo zimezinduliwa kwa mara ya kwanza ni pamoja na Manukato(Pafyumu), mafuta ya ngozi maalum kwa uso, vipodozi vya usoni kwa wanawake na wanaume na pia mafuta maalum ya kupaka wanaume baada ya kunyoa ndevu.

Uzinduzi huo uliofanyika jana jijini Dar es salaam umehusisha Wanachama, wasambazaji na wageni mbalimbali.

Oriflame (EA) Tanzania Limited ni tawi la Oriflame East Africa ambayo makao yake makuu yapo nchini Sweden. Oriflame Tanzania imefunguliwa mwaka 2011 mwezi May, ambapo mpaka sasa imeweza kutoa ajira kwa watanzania zaidi ya elfu saba (7000) ikiwa ni kama wanachama, wasambazaji, na waajiriwa wa kudumu.

Malengo ya Oriflame ni kuwa kampuni namba moja duniani inayofanya biashara ya vipodozi kwa namna ya mtandao (Network Marketing)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 04, 2012

    Vipodozi vya wazungu ni sumu tupu. Juzi nilinunua lotion kutoka Canada imeandikwa Coconut butter. Nilipoangalia ingrients nyuma ya kopo, hamna hata content moja ya coconut powder, au cream imeandikwa, ni chemicals tupu zimeandikwa. Kwa hivyo jina la juu ni fake kabisa. Lakini inanukia kama mafuta ya nazi. Yaani mtu ametengeneza chemical mpaka akapata harufu ya mafuta ya nazi.

    ReplyDelete
  2. Unayosema Anonymous 12.26.00pm inawezekana ni kweli ila usijudge bidhaa katakana na ubovu wa bidhaa ulizowahi kutumia. Na ni vizuri tujifunze kusoma content za chochote tunachinunua na siyo kuangalia rangi, mvuto harufu, nakadhalika.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 04, 2012

    These guys are targeting the burgeoning middle class Tanzanians,the "mlala hoi" still uses coconut oil, which is still the best in my opinion.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...