Msanii wa Ras Innocent Nganyagwa akiwasilisha mada kwenye Jukwaa la Sanaa wiki hii. Kushoto kwake ni Afisa Habari Mkuu BASATA Bi Agnes Kimwaga.
Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Habari kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Lebejo akisisitiza jambo wakati akihitimisha programu ya Jukwaa la Sanaa wiki hii.

Na Mwandishi Wetu

Watanzania wametakiwa kuuenzi utamaduni wa makabila ambao una thamani kubwa sana, wito huu umetolewa wiki hii kwenye ukumbi wa BASATA na mwanamuziki mkongwe wa regge nchini na mtafiti mbobevu wa masuala ya historia za jamii, Innocent Nganyagwa, alipokuwa akiwasilisha mada katika Jukwaa la Sanaa kuhusu Umuhimu wa Utafiti Wa Makabila Katika Kuendeleza Utamaduni Wetu.

Alisema tamaduni za makabila mengi ya Tanzania zina mashiko mazuri na yenye thamani ambayo yakienziwa na kuendelezwa, yatawasidia watu katika maendeleo ya sasa.

Alisema Watanzania tunapaswa kujitambua na kujua mashiko ya Sanaa na tamaduni zetu na kuhuisha thamani ya maadili yetu kitaifa.

“Kila kabila lilikuwa na taratibu zake na mifumo yake ya utawala na shughuli zake za uchumi, pia makabila mbalimbali yalishirikiana, mambo haya yakiendelezwa ni dhahiri tunaweza kuendela zaidi katika zama za sasa za changamoto za utandawazi, uliorahisisha maendeleo lakini pia ukatuletea baadhi ya tamaduni za kigeni zinazopotosha maadili.

Msanii huyu aliwataka Watanzania kufanya tafiti zaidi na kujitambua wao ni nani na asili yao ni nini ili wasitegemee historia zilizoandikwa na wageni peke yake, kwani nyingi zinaishia katika mazungumzo waliyopewa bila kushiriki kikamilifu katika kupata taarifa zaidi za historia hizo kwa kuzipima katika ‘mzania jumuishi’ wenye kina kirefu cha mila na desturi.

Nae Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA, ndugu Lebejo, alisistiza kuwa tungeendeleza kilichopo kwenye tamaduni zetu na kukichanganya na teknolojia tungefika mbali sana katika kila eneo, tushikilie mila zetu tusiige vya Wazungu kwani wao wana mila zao na wanaziendeleza kwa mujibu wa mashiko yao ya utamaduni wao, tusibweteke na kupenda vya kuiga vya kigeni wakati tuna mambo yetu mengi yenye thamani na mafundisho ya kuishi maisha sadifu ya kimaadili.

“Tujitambue na kuzifahamu mila zetu kwa kufanya tafiti, tusisubiri mpaka tuwe maprofesa ili kuweza kufahamu tulikotoka, kwani mengi kati ya yanayohusu utamaduni wetu yanatuzunguka katika maisha yetu ya kila siku. Ni suala tu la kuwa na mtazamo chanya na kuamua kwa dhati kuuenzi utamaduni wetu”,alisisitiza ndugu Lebejo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. huyo nganyagwa amekosa kofia yenye rangi za bendera ya Taifa ya nchi yake mpaka ameamua kuingia na bendera sujui ya Ghana au wapi vile, utamaduni wa tanzania mfano uonyeshwe na wasanii wenyewe,sio utamaduni wa tanzania bendera ya ghana, huwezi kumkuta mghana kavaa kofia ya bendera ya Tanzania katika kuhamasisha utamaduni wa Ghana.Tuamke watanzania na kutangaza vyetu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 17, 2012

    Hawa jamaa wamekuja na mada halisi wala siyo ya kupingwa, tamaduni (culture) za makabila zinakwenda zinafifia.

    Kitu kimoja ambacho miaka ya nyuma kilikuja kuua tamaduni na hususan ngoma za makabila ni vile vikundi vya kibiashara vilivyozuka kwa majina tofauti kama "ngoma troupes"

    Hivi vikundi mostly vilikuwa vya majeshi, vilichanganya sana tamaduni tofauti na ngoma za asili tofauti. Kwa mfano kuna dada kweli alikuwa na sauti nzuri sana ya kuimba alikuwa ni mgogo na aliimba taarab, sitaki kuchekesha wala kutoa kebehi lakini mgogo na taarab wapi na wapi? Yeye anaimba "ewe njiwa ewe njiwa" waitikiaji maafande wanaitikia "pereka saramuu" sasa this was only taarab.

    Kitoto (ngoma ya wangoni) nachokijua mimi cha Hamisi kitoto wa Songea siyo kile nilichokuwa nakiona cha hizi 'cultural troupes' au mnanda wa wazee wa kinyasa.

    Inabidi kweli ufanyike utafiti kufufua hizi tamaduni zinazofifia.

    Village museum (Kijiji cha makumbusho) pale makumbusho kingeweza tumika kwa hili lakini badala yake pamegeuka kumbi ya starehe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...