Wizara ya Maliasili na Utalii inafafanua kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Balozi Hamis Kagasheki hajasaini mkataba wowote na timu ya Seattle Sounders FC ya Marekani kama ilivyoripotiwa na chombo kimoja cha habari cha hapa nchini.
 Alichofanya Waziri Kagasheki ni kutembelea uwanja wa mpira wa timu hiyo ya Seattle Sounders FC kuona matangazo yaliyowekwa hapo uwanjani baada ya timu hiyo kuanzisha ushirikiano na Tanzania katika masuala ya kutangaza utalii. Mambo muhimu katika ushirikiano huo ni uwekwaji wa alama za vivutio vya utalii vya Tanzania katika maeneo mbali mbali, kama picha za Mlima Kilimanjaro, Hifadhi za Serengeti, Ngorongoro na Zanzibar.
 Picha hizo zinazohusu utalii wa Tanzania zilionekana kwa mara ya kwanza tarehe 18 Julai 2012, siku ambayo timu ya Sounders FC ilichuana na Chelsea FC hapo uwanjani.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Balozi Hamis Kagasheki (Mbunge) alikuwa miongoni mwa Watanzania waliokwenda kwenye uwanja huo kushuhudia uamuzi huo wa timu ya Seattle Sounders FC. Hao ni pamoja na  Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mheshimiwa Balozi Mwanaidi S. Maajar, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Dr. Aloyce Nzuki Mkurugenzi wa Utalii  na maofisa wengine kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii Utalii, Ubalozini na maofisa wa Seattle Sounders FC.
 Akiwa hapo uwanjani, Waziri Kagasheki alisema kuwa ushirikiano huo utatoa ya kuitangaza Tanzania nchini Marekani, hasa katika Pwani ya Magharibi ya nchi hiyo.

George Matiko
MSEMAJI
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
20 Julai 2012
                                                                    Simu 0784 468047

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...