Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi imemtumia salamu za rambirambi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kufuatia Vifo vya Watanzania waliofariki katika ajali ya boti boti ya Skagit iliyotokea hivi karibuni maeneo ya chumbe kisiwani Unguja

Kufuatia ajali Wananchi wa wilaya hiyo Wanaungana pamoja na Watanzania wote katika maombolezo ya vifo hivyo vya ajali iliyotokea na kusababisha vifo na majeraha waliyopata Watanzania wenzetu na watu wasiokuwa raia wa Tanzania. 

Alimuomba afikishe salamu za rambirambi kwa ndugu zetu waliopotelewa na jamaa zao na kuwapa pole waliopata majeraha na maumivu Bi Chonjo alisema kuwa huu ni msiba wetu sote na kwamba majonzi yao ni majonzi yake na ya Watanzania wote. 

Kwa ndugu zetu waliojeruhiwa tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu awape ahueni na wapone haraka ili waweze kuendelea na shughuli zao za kujiletea maendeleo na kulijenga taifa letu.

Aidha amewapongeza maafisa na askari wa vyombo vya ulinzi na usalama na wafanyakazi wa meli binafsi, kwa juhudi kubwa walizozifanya za uokoaji wa ndugu zetu waliopatwa na maafa haya makubwa na ya aina yake. Ambapo alisisitiza na kuomba waendeleze juhudi hizo kwa manufaa ya Nchi yetu.

‘’’’Hakika Inauma sana kuona Watanzania wakipoteza maisha hasa tukikumbuka vifo vingi vya MV Spice Islander miezi 10 iliyopita Wananchi wangu wameniomba nikuombe uunde tume ya uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha ajali hiyo pamoja na njia ya kunusuru vifo vya Majini vinavyopoteza nguvu kazi nyingi kwa Maendeleo.

Alimalizia Chonjo Kutokana na ajali hiyo na msiba huu mkubwa,Tumeungana nawe Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete,katika maombolezo ya taifa ya siku tatu ambapo bendera zilipepea nusu mlingoti

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...