Kikosi cha Yanga
Kikosi cha Simba
Yanga
Majira ya joto ughaibuni,almaarufu kama summer huwa yana matukio mbalimbali yenye kuvutia na yenye lengo la kuwaunganisha wananchi na hususani watanzania wanaoishi katika nchi mbalimbali ulimwenguni. Miongoni mwa matukio ya namna hiyo, ni pamoja na michezo.

Katika kuendeleza “jadi” hiyo ya kujidai na kujumuika kunako majira ya joto, jiji la Toronto nchini Canada linatarajiwa kushuhudia mpambano wa kukata na shoka baina ya mashabiki wa Yanga na Simba wanaoishi nchini Canada. 

Pambano  hilo ambalo ni la marudiano linatarajiwa kufanyika Jumamosi hii tarehe 14 Julai katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Bur Oak uliopo katika mji wa Markham,Ontario ambao ni mji shirikishi wa eneo linalojulikana kama Greater Toronto Area(GTA).

Katika pambano la kwanza,mashabiki wa Yanga waliondoka vichwa chini baada ya kuangukia pua kwa kuchabangwa jumla ya magoli 8-3. Kutokana na kipigo hicho,Yanga wanasema ni muhimu kwao kulipiza kisasi na kulinda heshima ya Yanga. 

Tayari Yanga wameongeza nguvu kwa kuwaingiza kundini vijana sita ambao wapo chini ya umri wa miaka 20 kwa minajili hiyo hiyo ya kulinda heshima.

Kwa upande wa Simba,wao wanasema kama ilivyo jadi,ushindi kwao ni lazima na Yanga watarajie kipigo kingine kikali tu.

Waandaji wa pambano hilo wanaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi ili kuweza kuunga mkono timu zao wanazoshabikia. Mechi itachezeshwa na refa kutoka Iran ili kuondoa uwezekano wa “mlungula” na upendeleo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 13, 2012

    Go Simba gooooooooo!!!
    Tunawatakieni mpambano mwema; sie washabiki tutakuwepo kwa sana kupiga kidedea......

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 13, 2012

    Yap, mambo si hayo. Ninaishi maeneo ya GTA. Lazima nikacheki ni jinsi gani watu wanahaha uwanjani. Ushauri wangu kwa wachezi: No ulabu au mapenzi siku moja kabla ya mechi otherwise, utabebwa kwenye machela. Enjoy the game.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 14, 2012

    Simba oyeeeeeeee, simba daimaaaaa. Yanga hamna lenu bwana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...