Kumekuwa na uhaba wa picha na habari kutoka vyama vya siasa, ukiondoa CHADEMA na CCM, kiasi hata inaonekana kuna kutoa kipaumbele kwa vyama hivyo tu, jambo ambalo si kweli hata kidogo. 


Hii bila shaka inasababishwa na changamoto za maofisa uhusiano/habari wa vyama vingine, ambao hawachangamkii ipaswavyo fursa hii isiyo gharama ya kutangaza vyama na shughuli zao. Yaani ukiona picha na habari za chama fulani zinashamiri humu ujue kuwa maafisa habari wake wanachangamkia fursa hii bila ajizi na si vinginevyo.

Globu ya Jamii inasimamia kwa dhati sera yake ya HATUBAGUI, HATUCHAGUI; ATAYETUZIKA HATUMJUI. Hivyo shime vyama vya siasa amkeni na mlete habari zenu zichapishwe bila malipo, sharti likiwa mradi usichafue hali ya hewa ama usijeruhi hisia za mtu/watu.



Lete habari zenu tuzichapishe  bila malipo kupitia

issamichuzi@gmail.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. ASANTE ANKAL KUNA VYAMA TUNAVISIKIA TU ILA HATUJUI VINA SERA GANI VIONGOZI KINA NANI NA JE VINAMGOMBEA YUPI WA URAIS 2015. VYAMA VIWILI VIKO KIMYAAA NCCR MAGEUZI NA DP. ZAMANI ILIKUWA BWANA WEEE ACHA TU, ENZI ZA MCHUNGAJI MTIKILA NA KATIBA YA JAMHURI... SISEMI

    ReplyDelete
  2. Una uhakika na unalolesma? mbona tunajua kuwa kapu lako la limejaa email za vyama vya upinzani ?

    ReplyDelete
  3. ANKAL KWA MUDA MREFU UMEKUWA UKIPENDELEA CCM/SERIKALI.
    MPAKA NILIKUWA NAWAZA KUWA HII BLOG NI KAMA VILE GAZETI LA UHURU AU REDIO UHURU. KWA SABABU MATUKIO NA COMMENT YENYE MTAZAMO WA CCM NDIZO HUWA UNAZIPATIA NAFASI KUBWA.
    HATA HII COMMENT YANGU UNAWEZA USIIRUSHE.

    ReplyDelete
  4. Wewe Michuzi ni muongo na mnafiki pia unapendelea.Uongo wako wakutoa tangazo hili ni kujikosha.Unapendelea wazi wazi tena unaipendelea serikali pia CCM huo ni ukweli tupu.
    Wakati kuna mgomo wa madaktari blog yako ilisusia kutoa taarifa za mgomo huo hata kikwete alivyowaita madaktari kuzungumza nao ikulu picha zo hukutoa tuliziona kwingine kama mjengwa,hakingowi na wavuti pia kwingine siyo huku.Juzi hapa kulikuwa na mgomo wa walimu hukutoa taarifa mpaka ulipotoa breaking nyuuzi yako wakati mahakama imetengua mgomo huo ni unafiki na upendeleo.Wakati wa uchaguzi arumeru hukutoa taarifa kama blog zingine kwakuwa wewe na CCM yako,pia serikali yako mlikuwa mnashindwa,operation za chadema unaziweka kapuni,habari za upinzani hasa chadema za kibunge huziweki humu huo ni unafiki kuweka tangazo hili humu.tunajua bloggers wengi mnakopy na kupaste taarifa bila kujali nani wakwanzqa kuitoa lakini hata hivyo hufanyi huo ni upuuzi unafiki lazima tukwambie ukweli.
    lazima ubalance CCM na Serikali yake vimeshindwa na kama wewe pia humo humo na umeshindwa useme lakini siyo utoe tangazo kutafuta habari za vyama kwani zamani ulikuwa unazipata wapi? naleo unataka uzipate wapi? tuliisha kujua wewe na vizuri na ushabiki wako kila nyanja.

    ReplyDelete
  5. Mdau wa hapo juu na wengine wenye msimamo huo. Asante kwa kutoa maoni yako, na nakuhakikishia kwamba msimamo wetu Globu ya Jamii ni huo huo. Kwa mifano michache tu kudhihirisha wewe si mkweli bofya hapa na uje tena kusema hayo uliyosema.

    http://issamichuzi.blogspot.com/search?q=chadema

    pia bofya hapa http://issamichuzi.blogspot.com/search?q=chadema&updated-max=2010-11-01T17:58:00%2B03:00&max-results=20&start=12&by-date=false

    Na pia BOFYA HAPA http://issamichuzi.blogspot.com/search?q=chadema&updated-max=2010-11-01T17:58:00%2B03:00&max-results=20&start=12&by-date=false

    BOFYA HAPA PIA http://issamichuzi.blogspot.com/search?q=chadema&updated-max=2011-02-22T12:52:00%2B03:00&max-results=20&start=39&by-date=false

    ReplyDelete
  6. Ankali Michuzi,
    kwanza niseme nimeshangaa umepata muda kujibu hoja kupitia huku kwetu wadau. Ni nadra mno kukona katika sehemu hii, na ikitokea ni lazima kuna jambo. na hili si dogo ati!

    Mimi kwa maoni yangu naomba uachane nao hao wasioridhika, na haki ni pale wanapokuwa wamefaidika wao. Mfano; kesi ya Igunga wangeshindwa ungesikia haki haijatendeka. Achana nao hao, wewe piga mzigo tu. Kama angalizo ndio umeshatoa, na mwenye tafsiri yake na alale mbele. akitaka afungue blog yake. Tena akuombe radhi kwa kukufananisha na akina Haki na Mjengwa na kale kadada ka Wavuti ambako kazi yake ni ku-copy&paste kazi za wenzake kama alivyo Haki. Afazali na Mjengwa anatuleteaga utumbo wake wa vijijini ambao ni wake na sio wa kukopi.

    Swala hapa ni kukaribisha vyama vya siasa vilete habari zao, na waondoke usingizini. sasa wewe kosa lako ni lipi? Hizo link uliozotoa (japo ukibofya hazifunguki hadi juzikopi na kuziweka kwenye mahala pake) ni jibu tosha kwa huyo jamaa hapo juu. Kelele za mlango hazimkoseshi mwenye nyumba usingizi.

    ReplyDelete
  7. Wewe ni mnafiki kuna comments nyingi nimetuma kukosoa CCM kiroho safi ukazibania lol.Yaliyo tokea igunga hujasikia bado. Safari zako za Nje ya nchi zina walakini?Soma kimya na tafakari.Maji ni uhai.

    ReplyDelete
  8. MBON MJENGWA ANAYEPENDELEA CHADEMA HAMJAMSEMA?

    ReplyDelete
  9. Wajemeni mwacheni ankali wetu ze vakesheni za kudandia mchuma wa kikwete na kufanya ulinzi wa taifa a.k.a usalama wa taifa mzee wa kuzuga na ze fulanaz.......atakapoelekea kikwete ze fulanaz lazima itangulie mlinda chama cha mafisadi na serikali isiyojali sisi kina lalahoi

    ReplyDelete
  10. Ukiona Ankal Amejibu humu ujue amepata negative Comments nyingi mno na alizozirusha hapa ni thelethu ya watu walizo comment. Wise advise: '' Huwezi kumridhisha kila mtu pia Kuwa an Entrepreneurial..Take Negative Feedback comments as opportunities and work on them. Then Blog yako itazidi kushamiri na kuchanja mbuga to Generations.

    ReplyDelete
  11. Ankal ,shikamoo. mimi ninashida moja tu, nakuomba sana unitangazie kwa wana globu kwamba nina mitambo ya kupeki juice kwenye mabox,imekaa tu takribani mwaka wa 5 sasa, sina ujanja wa kuifanya ifanyekazi,naomba kama kuna mtu mwenye maarifa anitafute ,niko tayari kuiuza .Pia nina mashine 2 za kubandika picha kwenye vikombe ( Mugs) mpyaaa-nililetewa kama mradi,na hizo pia nimechemusha ,nani mkali aje azinunue ???? vikombe vyake vya kuanzia pia ninavyo 2000 hivi. Njoni jamani hatutakosana bei. jacobmayillah@hotmail.ca

    ReplyDelete
  12. Ankal nani asiyekujua kuwa wewe ni CCM na ni jamaa wa jumba jeupe?, sijui kimekutokea nini leo mpaka ukawaomba wapinzani walete habari zao kwako.au umeshasoma mshale wa nyakati kuwa upinzani unaenda kuchukua madaraka 2015 kwa hiyo unaanza taratibu kufagilia kibarua chako?.

    ReplyDelete

  13. Ankal no matter unapenedele Chadema au CCM i dont care what i love from you is the news ahead.. unazatupa sisi tuliopo ughaibuni alafu achana na maneno ya hao watu siku zoote huwezi kmuridhisha mtu hata kidogo.... Kingine jamani watanzania ushauri wangu ni tuachane na siasa mavi za kiafrica sasa ni wakati wa kufanya kazi kwa bidii na kumuomba Mungu atusaidie tufanikiwa bila kujali chama chochote kumbuka hata dini inasema amelaaniwa yule amtegemeae mwanadamu,, naona hicho ndo tunataka kukifanya sasa kwa kuona chama fulani ndo kinaweza.

    ReplyDelete
  14. someni alama za nyakati,ankal nashukru kwa kuweza kuweka bayana hili,pengine unaona mwelekeo wa kisiasa,chama chako ni ccm na mara nyingi ndiyo unawarusha sana hewani lakini pamoja na hayo kaa ukijuwa kuwa watu wanataka nn na si ccm unakataa kutokuipendelea ccm,unasafirigi na mheshimiwa kutafuta nn mbona mjengwa hatujawahi kuona? brother mabadiliko yaja na hayapingiki,tusubiri na tuone.

    ReplyDelete
  15. ANKO MICHUZI NINAVYOMPENDA NITAKUNYWA SUMU JUU YAKE SIO SIRI AAAA NAUMIAAAAA

    JAMANI MWACHENI ANKALI SO FAR NIMETOA HOJA KADHAA HAJANIBANIA HATA MARA MOJA. NA ANAZIRUSHA LAIVU ZA MOTOOOO
    MIMI SIO CCM WALA SIJAWAHI KUWA CCM.

    SHUKRAN JAZEERA ANKAL

    ReplyDelete
  16. Mtazamo wagu binafsi ni kuwa Mheshimiwa Michuzi anajaribu kutuletea maoni ya upande wa upinzania lakini ni lazima akubali pia anabana maoni ya wana blogi hii ambaye haimpendezi yeye au chama tawala. Mimi binafsi pamoja na wengine hapa wamebaniwa maoni yao wasiopendeza CCM bila ya kutukana mtu. Nina elimu tosha ya kutoa maoni na msimamo wangu bila ya kutumia lugha chafu, ila itakuwa sio kweli kwa Mheshimiwa Michuzi kusema kuwa habanishi maoni ya upinzani kwa kuwa amechapisha machache. Wadau wote hapa wanaodai maoni yao yamebanwa, sio wote waongo. Mie binafsi maoni sijatoa kwa muda kwa kuwa yanaenda kapuni hata kama natumia lugha safi.

    Hayo tu.

    ReplyDelete
  17. keep it up Michuzi. achana nao hao wenye sera za kishari wamekaa kulalama tu kama viongozi wao. hii ni blog ya jamii endeleza libeneke kaka. wadau tuko nyuma yako

    ReplyDelete
  18. Anony Wed Aug 22, 01:49:00 AM 2012 ebu tutake radhi waumini wa mjengwa blog. Nimefurahi umekiri kwamba mjengwa anatundika kazi zake mwenyewe na kwa taarifa yako ni kwamba, huo utumbo wa vijijini sie ndio unaotukosha.

    Lawama kwa aliyekuleta mjini ukiwa na chunusi tayari!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...