Askari wa jiji dar wakibeba banda na bidhaa zote za chinga na kuondoka nalo. pembeni kushoto chinga mwenye banda akiomba yaishe bila mafanikio.

Baadhi ya wakazi wa kinodoni Mkwajuni wakishuhudia askari jiji la Dar wakiwa kazini katika kamatakamata maeneo hayo. Picha na mdau Yakubu Mkaka 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. hawa watu wakale police. Huu ni unyama mtu anajitafutia riziki yake na mtaji mnauchukua kabisa sasa atatunzaje familia yake. Ipo siku TZ itaamka hao askari nao watapewa cha moto.

    ReplyDelete
  2. Ndio maana MAJAMNGA HAYAISHI WANAONEA BUZI LAKINI GOMBE OGOPA. kunawanaoiua njii hawafanwi lolote wala chochote ha wanaojitafutia MLO wa SIKU wanateswa na KUDHURUMIWA.(SHANGARORO- USA)

    ReplyDelete
  3. Hivi Tanzania tuna viongozi kweli? ifikie wakati mfikirie hawa watu wa kipato cha chini mnatengeneza majambazi wenyewe. Hii nguvu inayotumika kwa wanyonge laiti ingetumika kukamata wenye mabilioni uswisi na wengine wanaotafuna nchi kama muwa. MUNGU TUANGAZIE MWANGA WAKO NA KUIKOMBOA TANZANIA

    ReplyDelete
  4. Shangaroro wa USA, hata huko nafikili kuna sheria , au huko mtu unajiamulia tu kuweka kibanda chako cha HOT DOG popote ??? Huku uliko watu wametengewa sehemu ( flea market. ndugu zangu tuweni wa kweli na tujaribuni kutafakhari kabla ya kusema , ni hatari kupotosha umma namna hii. eti wanateswa, sasa wewe mwenye huruma njoo basi utujengee nchi. Tuone kama tutapata hata hiyo sehemu ya kuegesha magari,maana kila mwenye shati mkononi anauza popote njiani,au mwenye nyanya zake basi kazianika barabrani kabisa na ukimgonga !!!!!! Rais Shangaroro anakusweka lupango. Mheshimiwa , wewe baki huko huko USA na kama food stamp zako zimekwisha sema tukutumie pesa ukale.Zebedayo msema kweli

    ReplyDelete
  5. Hao Askari wangesafisha jiji kwanza sio kuwadhulumu maskini hao zebedayo mkandia watu wasema kweli ungesafisha jiji kwanza ndio ukawatengea watu sehemu yakufanyia kazi lakini jiji chafu mnaonea watu walipa texi hawapati huduma yeyeto!mimi ninakuona wewe nistupid wa mwisho na sio mtanzania anaeipenda nchi yake wewe si mtanzania ndio maana huna huruma na hiyo nchi!

    ReplyDelete
  6. Wewe zebedayo nilikua nakutafuta sana...mm naitwa tajiri wa mawazo endelevu..sikusoma ila naona mbali...ww mawazo yako yote hasi sio chanya kama yangu..coz hata siku moja sijawahi kukuona ukikemea mambo ya ajabu ajabu yanayo likumba taifa letu..why nasema hivi...ww zebedayo katika maisha yako ushawahi kukaa kwenye majera ya hapa kama vile keko au ukonga na kama bado basi jaribu siku moja kutembelea wafungwa..kisha utajiuuliza mwenyewe hivi hii nchi hawafungwi wahindi au warabu au hao wanaojiita wazungu...au wao hawafanyi makosa kitu ambacho si kweli kabisa...so amka ZEBEDAYO MSEMA UOONGO. aibu kwako....amani kwa wadau wote.

    ReplyDelete
  7. zebedayo uko juu kweli msema kweli endelea hiyohiyo kwani unajua mambo yote ya watanzania wanavyoishi ughaibuni

    ReplyDelete
  8. zebedayo hebu basi tuambie hizo bidhaa wanazozichukua zinamalizikia wapi? Ni wizi wa macho kabisa, kila mtu anajua kama hao askari na wakubwa wao ndio wanaochukuwa matunda na vyakula wanavovikamata na kupeleka majumbani mwao, haki hapo iko wapi?

    ReplyDelete
  9. hizi nguvu zinazotumika hapa kwa watafuta riziki yao kama hawa wanamgambo hawana kazi ya kufanya siwaende kufanya usafi na nchi imeoza kwa uchafu kila kona?

    ReplyDelete
  10. jiji lenyewe chafu sijui kunasafishwa nini?

    ReplyDelete
  11. Natafuta rizki jamaa wananidhulumu. Ingekuwa mimi ningeanza biashara mpya...wizi.

    ReplyDelete
  12. kila mtu anajua kuongea lakini kumbukeni kuna SHERIYA YA SERIKALI ikivujwa hukumu itatumika

    ReplyDelete
  13. Bwana Zebedayo Hayo maneno unayoyatoa ni yako wewe au umetumwa? yaani hukuona lolote la kutetea unatetea ushenzi? yaani kinachokuuma wewe ni kwamba wamachinga wanatundika biashara kiasi kwamba unakosa kwa kupaki gari lako sio? AAACHA HIZO Siasa zako za kifasadi, sasa lipi bora Kuuza chinga au kwenda kupola simu? Acha hizo tena Acha kweli na tena usiniudhi, Tanzania ina mambo mengi yanayoendeshwa kiholela kuliko hilo la kufanya biashra katika maeneo yasiyipaswa lakini serikali inapuuza,kuna linalokera kama la kuwakumbatia MAFISADI? Mbona hatuwaoni hao askari kwenda kuwasomba mzobe mzobe kama walivyokibeba hicho kibanda cha mmachinga wa watu anaejitafutia kwa jasho lake na sio kama huyo fisadi anaedhulumu mamilioni ya umma?
    Acheni hizo au nawewe ni mmoja wa hao? na ndo maana unatetea au hakuna parking? .

    ReplyDelete
  14. TUANGALIE JAMANI HII DHULUMA YA KIMACHO MACHO, NDO MNATAKA KUWEKA JIJI SAFI LAKINI NYIE WATU MNA WATOTO KWELI? FIKIRIENI HUYO MTU HANA JINSI NDO MAANA ANAFANYA HIYO BIASHARA JAMANI, TANZANIA HAPO HAKUNA ALTERNATIVES NYINGINE HAKUNA SOCIAL BENEFITS WALA PENSIONS, MSIANGALIE TU MAISHA YENU MUANGALIE NA UBAZI WA PILI WA SHILINGI NDUGU ZANGUNI. KAMA KUSAFISHA NCHI TUANZE NA VIONGOZI WACHAFU KWANZA," UNAWEZAJE KUKOGA KTK BAFU CHAFU? SAFISHA BAFU KWANZA NDO UINGIE UKAKOGE" UNASAFISHA NCHI KIONGOZI MCHAFU, HII IKOJE?? NA NDO MAANA NIMETUMIA CAPITAL LETTERS KWA MAANA INANIUMA SANA.
    MDAU MBEGU.

    ReplyDelete
  15. angalieni hapo juu wadau, yaani hovyoooo !! dunia nzima na kila nchi hujiwekea sheria zake na wananchi wanapaswa kuzifuata, mimi sitashabikia tu ujinga na kutotaka kuelewa NO please NO Zebedayo niko pale pale , hatuwezi kuruhusu nyanya , sindilia mnazotuletea kutoka huko ziuzwe tu popote barabarani, halafu kingine , ubapoanika vyakula kwenye mitaa ya magari namna hiyo ,vumbi,moshi wa magari inzi n.k je ?? hicho chakula unachouza kinausalama ??? Mahodari wa kushabikia tu nyie ha !!! Mashaka umemsikia katoa kauli yoyote hapa ? no. jamani darasa lenyewe dogo,mlichobakia ni kuhamazisha upuuzi. Hebu tujengeni nchi ya wenye ustarabu ,please people.Zebedayo msema kweli

    ReplyDelete
  16. Ndugu watanzania, usafi, kufuata sheria, kuwa makini, kujali wengine, kuheshimu sheria, usafi, utu ..na mengine yanayoendana na USTAARABU..huletwa ..kwanza na wachache na pia kwa kuwashurutisha watu....huwezi kuleta hayo kwa kuomba. Barabara hasa za dar zimejengwa kukawa na vituo vya basi na sehemu za wapita kwa miguu...kwa hela ya wananchi. sasa wachache wanatoka huko walikotoka wanapanga nyanya na mitumba iliyotoka kwa watu waliostaarabika....tena pale Kitega uchumi Samora, wanakukatalia hata kupita kama hununui!!!wakati huo huo pale mbele ya ubalozi wa wingereza pasafi na pia njia nzuri na unafurahia mji. HIVI HUYU ZEBEDAYO NANI ALIMWAMBIA KUWA MJINI NI MAHALI RAHISI? ZEBEDAYO HAWASAIDII HATA HAO ANAOFIKIRI WANATAFUTA RIZIKI. MJI UKIWA MCHAFU NA HAUNA USTAARABU SISI WENYE HELA NA VIWANDA VYETU TUTAONDOKA NA WAO WATAMPATA NANI WAKUMUUZIA MITUMBA???, USTAARABU. ZEBEDAYO NENDA RWANDA NA HAO WAMEKUWA VITANI KWA MUDA MREFU WALA SIO KWA WABEBA MABOX UTAONA JINSI PALIVYO NA USTAARABU. SIO UCHAFU NA UPUUZI ULIOPO HAPA DAR. SERIKALI YA TANZANIA IMEKUWA ZEMBE KWA MUDA MREFU LABDA INAWASIKILIZA WAKINA ZEBEDAYO. TUNATAKA KUONA USTAARABU...KAMA KUNA MUUZA MITUMBA AKAUZIE MAHALI MAALUMU..HATA KWA WABEBA MABOX KUNA MAENEO HAYOOO.. KAMA LIVERPOOL STREET KULE LONDONI. NA MTU UNA ENJOY KUFANYA SHOPING YAKO..SERIKALI ONDOENI UCHAFU WOTE WEKA MAZINGIRA SAFI, ASIYEWEZA KUISHI KATIKA HALI HIYO AENDE VIJIJINI...WEWE ZEBEDAYO WAJAPNI WENGI WANGEPENDA KUISHI TOKYO...LAKINI KAMA HUWEZI KODI YAKE UNAISHI PEMBEZONI. .KAMA HUWEZI KUISHI DAR TAFUTA MJI WA RAHISI..HIYO NDIO FACT YA MAISHA
    mimi ni mbongo tena kutoka kijijini ila nimehamia mjini kwa kuwa napamudu. mungu ibariki tanzania

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...