Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la ATCL Kapteni Milton Lazaro akizungumza na waandishi wa habari juu ya kushitisha kwa mkataba baina ya shirika hilo na kampuni ya Aero Vista Dubai ambayo ilikodisha shirika hilo ndege aina ya Boeing  737-500.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la ATCL Kapteni Milton Lazaro (kushoto) akijadiliana jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa Shirika hilo bi Mwanamvua Ngucho kabla ya mkutano huo.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali wakifuatilia mkutano huo 
=======  =======  =======
SHIRIKA la Ndege la Air Tanzania (ATCL) limesitisha mkataba wake na kampuni ya Dubai ya Aero Vista kutokana na kuwa makubaliano yaliyofikiwa mapema mwezi Mei hayakuleta maafanikio yaliyotarajiwa.

ATCL ilikodi ndege aina ya Boeing 737 – 500 yenye uwezo wa kubeba abiria 108 mnamo mwezi wa tano ambayo imekuwa ikiitumia kufanya  safari za Dar es Salaam – Kilimanjaro- Mwanza na baadae kuzitumia katika safari nyingine ya Dar es Salaam – Hahaya (Comoro) iliyozinduliwa mwezi uliopita.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL Kapteni Milton Lazaro alisema kuwa shirika limefikia uamuzi huo baada ya kugundua kuwa shirika halipati faida iliyokusudiwa kabla ya kusaini mkataba huo.

Aidha, Lazaro alisema kuwa shirika lipo katika mazungumzo na kampuni nyingine ili kuafikiana katika kufanya biashara pamoja na kuongeza kwamba mazungumzo hayo yanatarajia kukamilika katika wiki chache zijazo.

 “Tumeamua kusitisha mkataba tuliosaini na kampuni ya Aero –Vista kutokana na ukweli kuwa mkataba huwo haujatuletea mafanikio tulieyeyekusudia. Kuna uwezekano wa kujadiliana upya na tunaweza tukaingia nao katika mkataba mpya baada ya mazungumzo kama wanaweza kuondoa baadhi ya vipengele ambavyo si vizuri kwetu kama kampuni.

 “Abiria ambao tayari wameshakata tiketi katika kampuni yetu hawana sababu ya kuwa na wasiwasi sababu tayari tumeshawakatia tiketi katika mashirika mengine ambayo na safari zao zitaendelea kama walivyopanga,” alisema Lazaro.

Aliongeza kuwa shirika hilo la ndege la taifa litarudisha safari zake Dar –es Salaam- Kilimanjaro-Mwanza baada ya kukamilika kwa matengenezo ya ndege ya shirika hilo aina ya Dash 8Q-300 ambayo ipo katika karakana ya shirika hilo kwa sasa.

Pia, Kapteni Lazaro alisema kuwa safari ya Dar es Salaam – Kilimanjaro – Mwanza ndiyo safari pekee itakayoathirika kutokana kusitishwa kwa mkataba huwo na kuongeza kuwa shirika litaendelea na safari zake za Dar es Salaam – Hahaya kama kawaida.

 “Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza. Wateja wasifikirie kuwa hatupo kabisa kwenye biashara. Tutaendelea na safari zetu za Dar es Salaam – Hahaya (Comoros) kwa kipindi hiki. Ni safari za Dar es Salaam – Kilimanjaro – Mwanza pekee ndizo zitakazodhurika katika kusitishwa kwa mkataba huu,” alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Wasiangalie tu mikataba bali wajiangalie wenyewe kwanza kwani ufisadi mdogo mdogo unalimaliza hilo kampuni. Yaani baada ya kutangaza kuanzisha safari tu basi watu walishangilia kwamba ticketi za dili zitaanza kupatikana! Na zaidi tumewaona wakiwasafirisha marafiki zao kishkaji tu kati ya Dar, Mwanza na KIA... We have a long way to go na mkurugenzi unatakiwa kujipanga kisawasawa...

    ReplyDelete
  2. Tanzania imelogwa na aliyeloga hayupo duniani!!! Nimepita nairobi airport, kutokea DSM nilitaka nipige picha msururu wa ndege za kenya airways ambazo idadi yake sikuweza kuipata kiurahisi. Nilipokuwa nimekaa waiting lounge nikawa natafakari sana, hivi sisi tumekula sumu gani inayotufanya tunafikiria tu kujijazia mali na kuhujumu mali ya uma. Nisaidieni anayejua kweli kuna hata nchi moja ya africa ambayo haina ndege ya shirika la ndege serikali?????

    ReplyDelete
  3. Shirika ili linakufa kutokana na ukweli kwamba kuna wafanyakazi waliopo ndani ya ATCL wenye kutekeleza mipango ya makampuni mengine (Spies) ambao wanatumika kuivunja ATCL.

    Inasikitisha kuona ATCL inashindwa kumiliki ndege zake zenyewe zaidi ya kukodi!! Pia na kuwa na safari chache!!

    NI AIBU KUBWA SANA KWA TAIFA ZIMA LA TANZANIA!

    ReplyDelete
  4. kwanini walewote walikuepo pale Atcl wasitolewe na kuanza upya kwani kila siku shida na shirika!Nakumbuka enzi ya kina bosi karere,mwapachu,rwembiza hivi hanikuepo sasa kwanini tunashindwa kuwa na uzalendo jamani!!Twiga ni muhimu kwa nchi yetu kwani ndio shirika mama,naumia sana nikiwa naona kunawatu wapo Atcl kwa manufaa ya kulimaliza ili P air indelee kama mnajua history ya most of wafanyakazi wa P wametoka Tc na best zao bado wapo ndani so!!!

    ReplyDelete
  5. Jamani ATCL mbona mnatulet down namna hiyo jamani.Tuchangisheni basi hata sh.mia mia.Hata mimi nikipita Nairobi natamani kulia,kiwanjani ndege za KQ,zingine zinakuwa hewani wakati huo..Weka kwenye kodi huko Sh.200 kila kona za kununua ndege zetu mpya.hah.Nimeona hata Rwanda wana Boeing 737-800.Ufisadi ufisadi....

    David V

    ReplyDelete
  6. huyo P air naona kama mnamuonea tu, yule aliyetoa maamuzi na pesa ya kununulia G5 na fokker 50 (ndege za serikali) ambao pia wana fokker 28, ambazo zinaota jua tu muda mwingi, yupo wapi? kwanini asitoe pesa na maamuzi kukanunuliwa ndege kwa ajili ya ATCL? akachukuliwa na yule anaye endesha kitengo hicho chenye G5 na f50 kwa ufanisi ambacho hakizalishi bali kinatumia tu , aje aendeshe ATCL ambayo itazalisha? kama wapo wanaoiua ATCL kwa manufaa ya P air basi wapo ngazi za juu huko serikalini na si ATCL.

    ReplyDelete
  7. Ni aibu na janga la Kitaifa kufikia mpaka sasa 'MBUNI' (ATCL)HAJARUKA JUU KWA MBAWA ZAKE, ANGALIA NAKIMBIA KWA MIGUU CHINI!

    ReplyDelete
  8. Matatizo ya Tanzania ni kulindana. Watu wanaua mashirika na hawachukuliwi hatua. Wanaendelea kula na kuwacheka wengine.

    ReplyDelete
  9. Si afadhali Kenya kiuchumi wako Juu. Embua angalia Ethiopian Airline. Toka niko mdogo nasikia hili shirika...sasa hivi linachanja mbuga mpaka majuu na bei yao si ya kitoto nikimaanisha si among cheap flghts.

    Sisi tuna nini jameni???????

    Kwa nini msijifunze kwa wenzenu. Mnatia hasira nyie!!!!

    Kutakuwa na hujuma mahali fulani haiwezekani; why now na si ATC ya miaka ile?

    Nadhani kama alivyosema mdau...Tz maadili yameporomoka hakuna shirika la uma linalojiendesha kwa faida...board members unakuta wapo pale kwa maslahi binafsi.

    Utakuwaje board member wa shirika lililoko ICU na wewe unatembea kifua mbele...si bira mjiuzuru tu kama Kofi Annan na Srya

    ReplyDelete
  10. ATCL inabidi ivunjwe kabisa iunde upya kwa kuajiri wafanyakazi wachache on performance based contract with clear clear key performance indicators na management mpya kabisa hata ya foreign sawa tu.....it is very dicouraging kila kukicha ni matatizo tu.... mnadhani wateja wenu tunawasubiri tu nyieee... muwe na difference business approach...

    ReplyDelete
  11. Duniani kila Taifa na kipaji chake!

    Bongo madege hatuyawezi, Biashara mgogoro hiyo kuendesha magege ya bamia na dagaa tunaendesha kwa bahati bahati!

    Sisi Tanzania kipaji chetu ni :

    1.Uenezi wa Kisiasa
    2.Idadi kubwa ya waganga na tiba asilia
    3.Ufisadi na ubinafsi
    4.Uhujumu
    5.Majungu

    Hatuna unwezo wa kuehdesha mashirika ya ndege!

    ReplyDelete
  12. USALAMA WA TAIFA MPO WAPI??!! INGILIENI KATIKA MAKAMPUNI YA UMMA YANAYO DONDOSHWA MAKUSUDI KWA MANUFAA YA MAKAMPUNI YANAYOMILIKIWA KWA ASILIMIA KUBWA NA NCHI NYINGINE NA WANATISHIA UCHUMI WA NCHI HII KUDONDOKA!

    LINDENI NCHI NA VITEGA UCHUMI VYAKE! USHAHIDI UPO TENA WAZIWAZI ILA HAKUNA CHOMBO CHOCHOTE CHA USALAMA KILICHO INGILIA KATI!

    NI AIBU KUBWA SANA KWA VYOMBO VYA USALAMA, WANANCHI, RAIS WA TANZANIA NA SERIKALI YAKE PAMOJA NA TAIFA ZIMA LA TANZANIA!

    ReplyDelete
  13. kwanza ni P air! ghafla 540! Duh...

    ReplyDelete
  14. Hamna nia ya dhati.Nilishawahi kuposti mahali kwamba tatizo la ATCL na mashirika mengine ni intervetion ya serikali kwenye uendeshaji wa shughuli zake.Hapa kwanza mfumo urekebishwe.Mashirika yawe semiautonomous kwa maana ya kufanya mambo mengi yenyewe bila kuingiliwa na serikali au wanasiasa wenye ajenda zao za siri.Deal la kukodi hiyo ni the best hapa TZ hata hao P hawajakodi Boeing zao kwa bei kama ya ATCL.Kama ni vipengele si vinarekebishwa then mnaendelea ba Biashara ? kusitisha huduma kunavuruga mipango kabisa ya kufufua ikizingatiwa kwamba nilimuona waziri ambaye tunaambiwa ndo ka order kuvunja huu mkataba akifurahi kuanzisha kwa maintenance hangar ya sheria P ambalo kiukweli linanufaika na utendaji mbovu wa ATCL ambao kwa mtazamo wangu unasababishwa na watu wa Wizara ya uchukuzi.Kuna ambao wanataka waonekana maheros wakati ukweli wana ajenda zao tofauti itakapofika 2015

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...