Marehemu Dennis Paul Mwafongo
11/08/1989 – 20/08/ 2012

Familia ya Bwana Paul na Bertha Mwafongo inapenda kutoa shukrani zao za dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki wote walioshirikiana nao kwenye msiba na kukamilisha shughuli ya kumuaga mtoto wao Dennis Paul Mwafongo aliyefariki dunia tarehe 21 Agosti, 2012.

Shukrani za dhati ziende kwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Mwanaidi Sinare Maaajar, na wafanyakazi wote wa Ubalozi wa Tanzania, Uongozi na Wana Jumuiya ya Watanzania waishio DMV, Uongozi na Waumini wa Kanisa la Bethel World Outreach, madaktari, wauguzi na wahudumu wa Hospitali ya Suburban iliyopo Bethesda, Maryland.

Mwili wa Marehemu Dennis Mwafongo unatarajiwa kuondoka Washington DC Jumamosi tarehe 25 Agosti, 2012 kuelekea Dar es salaam, Tanzania kwa mazishi. Msiba utafanyikia nyumba Tabata Kisiwani. Aidha heshima za mwisho zitatolewa siku ya Jumatano tarehe 29 Agosti, 2012 kwenye Viwanja vya Kareemjee na baadaye mazishi kwenye makaburi ya Kinondoni Dar es salaam, Tanzania.

Bwana Alitoa, Bwana Ametwaa, Jina lake Lihimidiwe!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...