Nyumba ikiwa imeshika moto ambao inasadikiwa ulitokana na shoti ya umeme katika chumba cha mpangaji mmoja wa nyumba hii,maeneo ya Mburahati jijini Dar es Salaam jioni ya leo.
 Wakazi wa nyumba za jirani na nyumba inayowaka moto wakiendelea kushangaa huku moto ukiendelea kuwaka kabla na mmoja wao kupata wazo la kutafuta ndoo za maji ili kuuzima moto huo ambao ulizunka ghafla kutokana na shoti ya umeme.
 Juhudi za kuuzima moto huo zikiendelea kwa kutumia ndoo za maji.
Nyumba moja ya makazi ya watu maeneo ya Mburahati jijini Dar es salaam imeshika moto kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kutokana  na shoti ya umeme.

Mpaka sasa haijafahamika kama ndani ya nyumba hiyo kuna idadi ya watu wangapi kwani ni nyumba yenye familia nyingi.

Juhudi za kuuzima moto huo zinafanywa na baadhi ya majirani wa nyumba hiyo kwa kutumia maji,huku juhudi za kuwatafuta watu wa faya zikiendelea kufanywa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Haya ni matatizo ya ujenzi usio wa mpangilio sasa hata hiyo faya itafika vipi hapo

    ReplyDelete
  2. Sasa hiyo mijitu mingine mbona imekaa inang'aa macho tu awasaidiiau wanangoja kuiba.Hata kwenye kuzika utakuta mtu hasaidii chochote, hivi 2koje?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...