Salaam Ankal Michuzi,
Naomba nitoe dukuduku langu linalohusiana na hali ya ukabaji na uporaji unaendelea kwa kasi hapa jijini.
Siku Jumapili tarehe 12 August 2012 tulienda kufuturu Russian Cultural Centre, Sea View. Wakati wa kurudi kwa vile tunakaa mjini tukaamua kutembea.
Tulikuwa mimi, baba yangu mdogo na mtoto wa dada yangu. Niliwashauri tupite Upanga Road lakini wao wakasema kwa nini tusipite baharini tupate upepo wa bahari na vile vile njia hiyo ni karibu na nyumbani kuliko ile ya upanga road wakisema kuwa siku hizi hiyo njia ni salama kwani kuna doria.
Tukapita hiyo njia, kufika kwenye kona ya kuingia gymkhana usawa na ule mti mkubwa walitiririka watu karibu ishirini na zaidi wakiwa na mapanga na magongo wakatuzunguka tukajaribu kukimbilia barabara ya ocean road hapo tukaomba misaada ya waendesha magari lakini hawakusimama na wao walishawaona hao watu.
Wakagawana mafungu matatu kila mmoja wetu akawa anafungu lake la kumpekuwa. Mimi walichukua handbag ndogo iliyokuwa na simu tatu (blackberry bold, samsung touch screen na nokia), mkufu wa dhahabu, pete na saa. Walipokuwa wanaichukua pete alinivuta kwa nguvu nikaumia kidole ambacho mpaka leo hii kimekaa upande na siwezi kukitumia.
Baba yangu mdogo yeye aliibiwa simu (blackberry) na wallet yake iliyokuwa n ashi 40,000 na card zake za bank na kitambulisho cha kupiga kura na cha kazi. Mtoto wa dada yangu yeye aliibiwa simu mbili (zote Nokia), wallet yake iliyokuwa na sh. 20,000, card za benki na kitambulisho cha kupiga kura pamoja na cha kazi.
Baada ya kuchukuwa vitu vyote hivyo hawakutosheka wakawa wananivuta kwenda chini (baharini) lakini kwa bahati hawakufanikiwa ingawa walikuwa wananitisha na mapanga yao nilisema wache waniuwe lakini huko chini sitaenda. Wakati tunavutana ikatokea gari kutoka upande wa ocean road hospital na wao walivyoona mwanga wa gari wakakimbilia baharini.
Nikawaomba wanipe funguo zangu za nyumba wakanirushia. Tulipotoka hapo tukaenda moja kwa moja kwenye kituo kidogo cha polisi gymkhana. Tulipoeleza kesi yetu wakatuambia hiyo njia ni hatari maana kuwa watu wengine wawili walikuja kabla yetu na wao walipata matatizo hayo hayo na vile vile kuna wachina wawili nao wamekatwa mikono na kunyanganywa milioni sita.
Tukaandikisha statement lakini cha kushangaza zaidi ni kuwa polisi wakaanza kutuuliza mmoja kati ya hao majambazi alikuwa mrefu na mpana tukajibu ndio wakatuambia kuwa huyo ametoka jela hivi karibuni, na mwengine akaniuliza mama huyo aliyekuwa anakuvuta wewe muende chini alikuwa mfupi kama mimi hivi nikamwambia ndio. Sasa nataka niulize hivi:
1. Kwa nini vitu kama hivi vinaachiwa mpaka vinaota mizizi. Maana tunavyoambiwa usipite njia hiyo kuna hatari ina maana kuwa tunawalea hawa majambazi. Kwani Polisi kazi si ni "Serve and Protect" sasa hapa wanamserve nani na wanaprotect nani?
2. Kwa nini mwananchi asiwe na uhuru wa kutembea kwa usalama hasa ukizingatia sehemu yenyewe ni karibu na Ikulu na bado kuwa uhalifu wa hali ya juu.
3. Kama Polisi na Insitututions husika zinajua kuwa sehemu hiyo haiko salama wanachukua hatua gani kurekebisha hali hii.
4. Kwa nini tuwape leeway hawa majambazi wafanye kazi zao kwa raha zao bila kuogopa ukizingatia kuwa kuna kituo cha polisi hapo hapo jirani, kuna Ikulu na taasisi za Serkali ambazo zote zina ulinzi.
5. Tuwaelewaje Polisi kama wao ndio wanaotuambia hii njia sio nzuri kupita ukizingatia time yenyewe ni mapema mno saa moja na nusu sio usiku mwingi, sasa wao wanachukua hatua gani.
Vile vile wanajua mbinu zote ambazo hawa jamaa wanazifanya maana walitueleza kuwa hizo bank cards inabidi muende bank asubuhi mapema maana hawa majambazi wana mtu wao ambaye ikifika saa kumi/kumi na moja alfajiri anaweza kutoa pesa kwenye ATMs bila hata kujua password..
Maombi yangu Mr. Michuzi ni kuwaomba wote walioathirika kwa kupita njia hiyo wajitokeze ili kwa pamoja tuweze kutatua tatizo hili. Vile vile ni kuliomba jiji lifyeke lile pori lote pale ocean road kuwe kweupe kabisa wasipate sehemu ya kujificha.
kwa leo ni hayo tu wadau.
mdau niliepatwa na janga hilo


Jamani hapo si ni karibu kabisa na Ikulu?
ReplyDeleteNi rahisi sana kuwakomesha mafedhuli hawa. Hapo wende askari kanzu kama watatu wenye silaha na kujifanya ni watembea kwa miguu. Majambazi hayo yakijitokeza tu ni kuyatwanga yote risasi na kuyaua.
ReplyDeleteNdugu yangu kwanza pole sana inasikitisha sana na ukizingatia polisi haifanyi kazi yeyote!leo wanawezaje kwenda kuwanyanyasa wamachinga wanaojitaftia rizki zao kwa jasho lao wanashindwa hiki kitu kidogo sana!wanakaa pale polisi wanasogeza siku zao za mishahara siku zinakwenda!nafikiri watanzania tunatakiwa sasa tuanzishe organisation ambazo zitatusaidia sbb serikali haina msaada wowote kwa jamii!hapo iundwe polisi jamii na wapewe silaha kumaliza uhalifu huo nisoft criminal polisi hawawezi kukomesha je heavy criminal?na sisi jamii tunatakiwa tuonyeshe action kama demostration jamii hili tatizo si lahuyu dada yetu na tumshukuru mungu hawakukurep dada yangu sbb kama wangekupa ukimwi maskin mungu atakuvua na mitihani mingine inshaallah!inasikitisha kama unavyosema IKULU hapo hapo na kituo cha polis kipo karibu!
ReplyDeleteYaani hapo na karibu kabisa na makao makuu ya jeshi letu tukufu la polisi. Bongo kweli imeoza.
ReplyDeletePole sana. Lakini kwanini utembe na simu zote hizo jamani!!!!!
ReplyDeletempaka sasa hivi na jinsi story inavyokwenda sijui mapolisi wa tanzania kazi zao nini haswa kulinda usalama wa wananchi au kulinda usalama wa majambazi. kwanini nasema hivyo( natumia lugha ya polisi aliyosema ukikaa mpaka saa kumi na moja wanamtu wao atatoa hela bila password kwanini kama anajua mlolongo huo wa ujambazi amechukua hatua gani yakisheria kama mlinda amani wa tanzania?nchi yetu inasikitisha kwa kweli na inalia huruma
ReplyDeleteHuwezi jua labda hao polisi wapo kwenye payrol ya hao majambazi sijuhi vibaka. Si umeona wanavyowajua vizuri.
ReplyDeleteTanzania zaidi ya uijuavyo.
Mimi mume wangu alinambia upanga maeneo ya karibu na regency ni hatari ku drive mwenyewe usiku...nikabaki mdomo wazi. Maana ndo nia yangu. Nasikia kuna vibaka uwa wanaibuka toka mtaroni wakiwa na mawe...waliwahi kupiga mawe gari ya mama wa kihindi ila yeye alikuwa jasiri akaendelea ku drive hadi alipofika kwa walinzi nadhani wa regency ndio ikawa pona yake.
Kwa sasa ni mara elfu maeneo tunayoishi ya nje ya mji ni salama kuliko Upanga. Upanga imeoza kwa vibaka ikifika jioni.
Pole sana kwa yaliokukuta kwa maana na mimi yalinikuta kama hayo kule kigamboni kwenye foleni ambapo vijana watatu wenye visu walivamia bajaj mchana mchana tu kwenye foleni na kuchukua watakacho nakutokomea taratibu. Na mimi nilivyoenda ripoti polisi wkaniuliza je, yule kijana mdogo alikuwa hajavaa viatu, nikajibu ndio. Sasa sijui niwasifie askari wetu kwa kuelewa detail za wahalifu bila kukosea au vipi.Siku hizi simu iliyoibiwa inaweza kuwa track hata wakitoa sim card na Police wanaweza, kama unabisha "wawezeshe" kesho ujionee. Na pia ikinunua simu ya wizi siku hizi ukitumia tu unajulikana labda uwe na sim card isiyosajiliwa ambavyo haiwezekani siku hizi. Mimi naona Polisi wameshindwa maana wakitaka kuwakamata hata leo wanaweza tena kirahisi saaaana. Kuna sababu ambayo haijulikani vizuri wizi kama huo hupo maeneo haswa ya osyterbay na masaki..ndio usishangae ndio mambo yalivyo.wanene hawatembei na miguu siku hizi ni ving'ora na magari kwahiyo vibaka wanasubiri wapite harafu waendelee. Lakini siku moja ndugu wa karibu au mtoto wa mnene mmoja ataporwa na "kuvutwa" baharini na kuvutika.
ReplyDeleteSolution hapa ni moja tu,sungusungu,hii ni most effective way na mwezi mmoja tu wizi WOTE unakwisha hasa huu wa uporaji wa kijinga kijinga.Kuna wakati tuliwahi kufanya mambo yakawa safi na salama.Polisi wenyewe watafanya kazi zingine lakini tuwe na sungusungu tulinde wenyewe,tushirikiane watu kila nyumba usiku watoe kijana au support yeyote kwa wanaolinda kama hamna vijana. Solution ni kufweka vibaka sio kichaka.
Ila pia hawa vibaka saa ingine tunawatengeza wenyewe kukamata wachuuzi na kupora mtaji wao wote na kuwadhurumu viwanja na haki zao zingine. Mimi naamini ongezeko la vibaka linatengenezwa na sisi wanene wenyewe. Kama mtu ana njaa na kidogo ulichokuwa nacho unamyang'anya unadhani atakula upepo?
Pole sana dada yangu, kwa jinsi story ilivyo inaonesha polisi wanashirikiana na hawa majambazi na wanawafahamu. Umesema kabla ya nyie kufika kituoni kuna wengine walikuwa wameshatangulia na kutoa taarifa ya kuporwa vitu vyao, kwa nini hao polisi hawakuchukua hatua zozote za kufanya doria ilo eneo? Eti wachina waliporwa mil 6, yaani dadangu watanzania hatuna pa kukimbilia, na hawa mapolisi ndo vibaka wenyewe, dawa ukimshika kibaka ni kumchoma moto tu na kuachana na mambo ya kusubiri polisi maana wanakula plate moja na vibaka, usalama wa raia upo hatarini kwasababu polisi hawafanyi kazi zao iwapasavyo.
ReplyDeletehapa , hata mimi tumbo linaniuma kwa hasira, leo,hata hiyo hamu ya kuwaomba waliokimbilia UK warudi sina.Yaani Polisi wako kituoni wamekaa ??? wanapiga gumzo la simba na mtibwa !!!! Said Mwema soma Michuzi mara moja moja Please .Zebedayo msema kweli
ReplyDeletePole ndugu yangu., Hiyo njia haifai, na polisi wanajua ingawa iko ikulu kabisa. nilipata somo langu hapo 2006, nimekuja likizo nyumbani sina hili wala lile, simu, fedha, kadi za banki kiujumla kama milioni nzima na kiasi zilienda, kabla sijafika huko chini nilikutana na kijana mmoja namfahamu ni polisi alikuwa lindo pale offisi ya waziri mkuu sasa akaja kukumbuka tumepita njia sio wakati ni too late, kuja kutufuata wameshachukua kila kitu, nakumbuka walichukua mpaka miwani ya macho.walipoona hao polisi walikimbia walizama kwenya bahari wote. so that place ni known kwa hilo na hapafai, sometimes utakuta watu wengi na unaweza dhani ni normal business watu wanapita tu but wanajua kumsoma mgeni and may be fedha na mali wanakuvamia. Pole sana. that place is known na sijui wahusika wanafikiri nini. Umenikumbusha mbali.
ReplyDeletePole sana kwa yalokukuta. Bila kumung'unya maneno, kutokana na maswali mlioulizwa na polisi ni dhahiri kabisa wanawatambua hao watu na wanafahamu fika kuwa wako hapo kwa kazi ya unyang'anyi. Jambo moja ambalo linajionyesha dhahiri hapa ni kwamba hao polisi wa kituo cha Gymkana wana mikataba na hawa watu. Kilichofanyika kukuulizeni ili kuwatambua hao watu ni kujua idadi ya vitu mlivyoibiwa ili waweze kwenda kudai share yao. Haingii akilini hata kidogo polisi wanawatambua manyang'anyi halafu hawafanyi doria. Kama walikuwa wameshapokea malalamiko toka kwa watu wengine walitangulia kabla yenu kwanini hawakuweka doria eneo hilo? Hilo ni dili la polisi...naomba kuwasilisha
ReplyDeletepole sana dada ila hao polisi moja kwa moja wanahusika na hao vibaka maana kama wanajua kuna alie mrefu alikuwa jela na mfupi sijui nini na nini usenge mtupu nchi hii
ReplyDeletesungu sungu ndio dawa yao hata sisi marekani tuna neighbourhood watch
ReplyDeleteSOMENI HII:
ReplyDeleteKatika hao vibaka kuna polisi, N unapotoa taarifa ya vitu vilivyoibiwa ni ili wavifikishe vyote wagawane. KUWAKOMESHA ILI WAUANE MUWAAMBIE UMEIBIWA MILIONI KUMI HIVI?? WATATAFUTANA USIKU HUOHUO ILI WAGAWANE.
dada unayelalamika mimi yamenikuta na kwa sababu nilipitia jkt na pia nikawa mkufunzi ya mambo ya usala na ulinzi niliweza kusikiliza maongezi yao kwa makini nikagundua kuna polisi ndani ya kundi. mara nyingi polisi hawa wameacha kazi kwa sbb za ujambazi na wengi walipelekwa pemba kipindi kile cha uchaguzi ule wa mkapa.
Nafikiri ni vyema hizi taarifa zikapelekwa kwenye vyombo vya habari pia mana ni karaha kubwa iwaje pahala kama pale kuna ofisi za usalama na njia ya kwenda ikulu hospitali kunafanyika uhalifu namna hiyo ni kwamba polisi hawawajibiki halafu tusema tunataka kukuza utalii wakati fukwe zetu haziko salama
ReplyDeleteMuathirika Said..
ReplyDeleteKwakweli polisi malengo yao wawakamate hao watu alafu tuitwe kwa utambulisho thats stupid coz the end of the day wanatolewa jela na watarudia tu. Pia ni ngumu kumjua sura bora mhalifu yoyote akikamatwa suala la uporaji ni akatwe mkono mmoja akirudia wapili na akiwa na silaha ni shoot to kill, hapo baada ya miaka miwili wizi na ujambazi utapungua kwa asilimia 80 tanzania.
Ila ninaomba mtoto mmoja wa mnene wa serikalini apate tukio hilo eneo hilo hilo na akutane na kundi kubwa kama hilo ndipo serikali itashtuka.