Beki mpya wa timu ya Yanga kutoka timu ya APR ya Rwanda,Mbuyi Twite akipokea jezi ya yake mpya kutoka kwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga,Abdallah Binkleb.
Mbuyu Twite akimwaga wino kwa dole gumba
Mbuyu Twite akimwaga wino katika karatasi ya mkataba wake na timu ya Yanga.
SIKU moja baada ya Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage kumtuhumu mtoto wa kigogo kuhusika kuwahujumu katika usajili wa beki wa Rwanda Mbuyi Twite kwa kumsajili kwa mahasimu wao Yanga, uongozi wa Yanga umekuja juu na kumtaka Rage athibitishe kauli yake ikiwa ni pamoja na kumtaja mtoto huyo wa kigogo.
Rage alitoa kauli hiyo jana mpaka kumpelekea kumwaga chozi sambamba na kujiuzuru nafasi yake ya Ujumbe wa Kamati ya Katiba,Sheria,Maadili na Hadhi za wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa madai ya shirikisho hilo kuikandamiza klabu yake.
Akizungumza Makao Makuu ya klabu hiyo Mtaa wa Twiga na Jangwani Katibu Mkuu Yanga,Selestine Mwesigwa alisema kuwa wao wanajua Rage ni muugwana na ni mkubwa katika nchi hii wanajua atamtaja na kuleta vithibitisho juu ya hilo mapema bila ya kuambiwa muda.
Aidha Mwesigwa alitoa ufafanuzi juu ya suala la mchezaji Mbuyu Twite ambaye inasemekana Simba wamemsajili na kusema kuwa wao Yanga wamemsajili kwa kufuata na kuheshimu kanuni na sheria za Cuf,TFF na FIFA hivyo basi wao hawajakurupuka katika usajili wake.
“Wenzetu naweza sema wamekurupuka kwa kuwa hawajafuata sheria wakati ndugu yangu Rage anajua kanuni na Sheria kwa hili namshangaa sana.”alisema Mwesigwa.
Alisema wao wameanza kufanya mchakato wa kumnasa beki huyo toka Novemba mwaka jana kabla ya kuanza mazungumzo na Simba juu ya aliyekuwa beki wao Kelvin Yondan na kusema kuwa walimtuma Mjumbe wa kamati ya Utendaji Abdallah Bin kleb kumfuatilia toka kipindi hicho.
“Sisi huyu mchezaji tumemsaka toka muda mrefu kabla hata ya Kagame kuanza na mara baada ya kumalizika kwa Kagame tulikuwa tunaangalia kiwango chake na kikaturidhisha.
Bin kleb akafunga safari na kwenda kuzungumza na uongozi wa timu yake ya Fc Lupopo ya Kongo na wala sio APR, Simba wao wamenunua mali ya wizi wakati sisi tumeenda kwa mwenye mali.
Aliongeza kuwa mara baada ya leo kupeleka majina ya timu yao TFF ndipo wataweka hadharani mambo mbalimbali juu ya beki huyo ikiwa na mkataba wake wa kuitumikia klabu hiyo.
Yanga kama kawaida chini ya uongozi wa Manji ni watendaji siyo wanasiasa kama simba ,siasa ni tofauti na mpira.Yanga mbele daima ,ohhh Yondani wetu ,.... oh Twite wetu ,okey usemaji tunawaachia ila utendaji na sheria tunavijua .Big up ,mdau big Joe
ReplyDeleteSimba mtajiju ... oh Yondani wetu hatacheza ,blablaaa maneno mengi kama Julio ,oh tumepata bonge la beki Afrika mashariki na kati ,Twite ohhh blablaaa ,kumbe mwali amepakatwa na yanga na yanga ndiyo kidume halisi ,simba kainama ,yanga kamt..... dol.... waohhh!!
ReplyDeleteIna maana huyu jamaa hajui kusoma na kuandika? Kwanini anatia sahihi na kidole gumba???
ReplyDeleteNafikiri mpira ni sayansi kama unashindwa kupanga karata zako vizuri hata ukimsahili Xavi Hernandez haiwezi kusaidia kitu Simba tulieni pangeni timu vzr Twite ni mmoja uwanjani wapo kumi na moja km mnajipanga vzr wanaweza wakala tano huyo Twite asifanye llte.
ReplyDeleteKitu cha kusikitisha ni pale ALHAJI anapoamua kudanganya hadharani Eti oooh Okwi kafuzu majaribio wakati siyo kweli, mara oohh sisi simba raizon yanga kandambili ile hali akijuwa kwamba raizo ni PAN Africa.
ReplyDeleteMh. Rage angalia mchezo wa mpira ni mchezo wa kishetani unapelekea watu kutukanana, unahusisha kamari, unahusisha vitendo vya kishirikina n.k nina wasiwasi u-alhaji wako ukaingia doa, leo unalia kwa sababu ya mtu badala ya kulia kwa sababu ya mungu kweli?
TWITWE NINI BWANA WALIKUWEPO AKINA SUNDAY NA AKINA KAJOLE WATU WAKABAMIZWA SITA BILA NA JUZI MBELE YA KANAVARO 5 MKONO BILA HATA MUMSAJILI NANI KAWAIDA YENU TUNAIJUA WAZEE WA RAUNDI YA KWANZA ,,,,,,,,,, TWITE KABURI HILO BABAAA ULIZA NSAJIGWA HAHAAAAA....
ReplyDeleteMdau mwenzangu wa 3 hapo juu Anonymous wa Sun Aug 12, 08:20:00 PM 2012
ReplyDeleteHata mimi nimeshangaa kwamba jamaa kutoka kwa Kagame hajafuta ujinga kwa kujua kusoma na kuandika.
Bandugu Yanga Siposi Kilabu si bora mumpeleke madarasa ya jioni pale TAASISI YA ELIMU YA WATU WAZIMA akajifunze kusoma na kuandika?