Leo Ninatimiza Miaka 61
Leo ninatimiza miaka 61 ya maisha yangu. Pamoja na kumshukuru Mungu kwa kuniweka hai hadi leo, ni lazima nijiulize: nimetumiaje fursa hii aliyonijalia Mungu ya kuwepo duniani miaka yote hiyo?Mungu ametuweka hapa duniani kwa sababu gani? Maisha yetu yana faida gani kwa wanadamu wenzetu? Tuna malengo gani yenye manufaa kwa wanadamu wengine siku hadi siku, mwezi hadi mwezi, mwaka hadi mwaka?
Miaka hii ninamwazia na kumsoma sana Ernest Hemingway. Alifariki akiwa na umri unaofanana na huu niliofikia leo. Tangu akiwa kijana, na miaka yote ya maisha yake, alitoa mchango mkubwa kwa walimwengu kwa uandishi wake. Alipokuwa na miaka 53, alitunukiwa tuzo ya Nobel katika fasihi. Je, nikijifananisha na watu kama Hemingway, mimi nimeshafanya nini?
Masuali haya ni magumu. Siku ya leo, pamoja na kumshukuru Mungu, pamoja na kujiuliza kuhusu wajibu wangu hapa duniani, nawajibika kuwakumbuka wenzetu wengi ambao hawakupata fursa ya kuishi miaka niliyoishi. Wengi wamefariki wakiwa wachanga, wengine vijana. Kwa nini Mungu kaniweka hadi leo? Hilo liwe suali la kujiuliza muda wote, liwe mwongozo wa maisha yangu yaliyobaki.
http://hapakwetu.blogspot.com/


Hongera. Bila shaka hayo masuala yako ni lecture kwetu pia. Tunamuomba M/Mungu akupe maisha marefu yenye faida kwa umma, nasi tutajifunza kutoka kwako. Bila shaka mtu mwerevu hufanya mambo kwa kutimiza malengo yake na kuisaidia jamii yake, wewe ni mfano huo
ReplyDeleteHongera Prof Mwenyezi akuzidishie akupe afya njema na hekima zaidi na zaidi maana tunazipenda hekima zako.HEPI BESDEI. MDAU ENGLAND
ReplyDeleteHongera sana.... Your words are so inspiring Sir. Please keep doing the good work which you are still doing in this world. May our Gracious God bless you abundantly and let you see your 100th birthday!
ReplyDeleteMwalimu Mbele Hongera sana kwa miongo hiyo uliyokata, ni zawadi iliyoje katika maisha haya ya mashaka kujaliwa kuishi miaka mingi hivyo, miaka ambayo haina uwiano na kiwango cha kuishi kwa Mtanzania. HOngera sana Mwalimu, natumaini utaendelea kuwa kisima cha maarifa kwa miaka mingine mingine 61 inayofuata. Mungu akujalie na akuzidishie siku zako za kuishi hapa duniani.
ReplyDeleteh b day Prof.
ReplyDeleteManshallah ya profesa
ReplyDeleteEid Milad
Eid Mubarak
Naona wajiuliza masuala magumu ya philosophia na theologia.Masuala yako yazaa masuala mengine makubwa kabla hayajajibika, naona ni kama conundrum. What is life all about, what is the meaning of life, why are we here? The answers are simple really, just answer another question: Is there GOD?
Mungu akuzidishie.
Umenena vyema Prof. Mbele!
ReplyDeleteHappy B'day Prof. Mbele. Basi uchane na nywele na ku trim ndfu Prof.
ReplyDelete