Kwako Ankal

Habari ya Swaumu?

Napenda kuwatakia wale wote wanaofunga Ramadhan Kareem.

Ankali mimi ninaomba uniwekee kwenye blogu yetu ya jamii swala hili la tipu kwenye sekta ya utalii Tanzania.

Mimi ni mtanzania ambaye niko mbele sana kutangaza vivutio vya watalii vilivyopo nchini na niko sawia kupendekeza kwa watalii makampuni ya Kitanzania pale wanapotaka kuja kutembelea Tanzania. Nafanya hili kwa moyo tu sio kwa kutegemea malipo.

Jambo lililonileta hapa bloguni leo ni hili swala la TIPU. Madereva wengi wa tours za Tanzania na wafanyakazi wa mahotelini kila unakokwenda wote wanaomba tipu. Watalii wanalipia safari yao ofisini na wanaambiwa gharama zote zimelipwa na kutoa tipu kwa dereva au tour guide ni hiyari yao.

 Lakini wanapoingia tu garini dereva anaanza kulia shida mara hatulipwi mshahara tunategemea tipu, mara maisha magumu basi safari nzima inakuwa ni wageni kusikiliza malalamiko ya wenyeji wao ambao wanatakiwa wawape maelezo ya kuhusu vivutio vya watalii walivyokuja kuviangalia wanaishia kusikiliza shida zetu wabongo.

Wakifika huko lodge mbugani basi maweita nao watalazimisha tipu hata kama kuna tangazo linasema tipu iwekwe mahali fulani. Kila mlo mtalii anaombwa tipu. Mfanyakazi wa hoteli anayepeleka begi anataka tipu, yule anayesafisha chumba anadai tipu atasimama mlangoni mpaka apewe pesa, basi wageni wote niliowaleta kutembelea mbuga zetu wanalalamika huduma za kubabaisha halafu kila mtu wanayekutana nae anadai apewe tipu. Gharama za safari zinakuwa juu kupita bajeti zao.

Ankali naomba hili litupiwe macho na wahusika. Kwanini bei ya safari isijumuishwe na gharama za madereva na tour guide na kadhalika? Hii itasaidia mtalii kujua anamudu safari au la. Haya ya kushtukizwa na matipu yanachosha.

Nimewahi kutembelea Kenya, wenzetu hili wana nafuu kabisa.

Nashukuru kwa kuniweka hewani

Mdau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Ni aibu kwa kweli wanaoomba tipu,maana tipu ni hiyari ya mtu kutoa na sio kulazimishwa,Yaani siku hizi watu aibu zimewatoka kabisaaa,kuomba wanaona ni kitu cha kawaida kwao,Kwani wanadhani wageni wanaokuja huko kutembea wana mfuko umejaa pesa tu za kugawa hovyo?hao watalii wanafanya kazi na kusave kuja kutembea na wanakuwa na bajeti zao,sio wana pesa za kumwaga tu! Ustaarabu ni kitu muhimu jamani!

    ReplyDelete
  2. Nimetembelea mbuga za wanyama nyingi tu hapo TZ, Serengeti, Mikumi, Ngorongoro,Manyara NK, lakini hata siku moja sijaombwa tipu,nawapa kwa hiyari yangu tu, pengine wananiona mimi "mpingo" mwenzao arosto chokambaya, kumbe hawajui nina kohoa fuba.

    ReplyDelete
  3. Kutoa na kupokea tip ni utamaduni tulioiga kutoka huko huko watokako watalii, yaani nchi za ulaya.
    Nchi kama Marekani tip ni LAZIMA kwenye restaurant zote zenye waiter service. Kima cha chini ni 15% ya bill.
    Sasa mnashangaa nini huku nako wakihitaji tip? Kwanza mmeshaona kazi za madereva/guides wa kitalii zilivyo ngumu? Hao watalii wanaolalamikia kutoa tip are probably cheap backpackers.
    Hii hotel/restaurant/tourism industry ina culture ya kutoa na kupokea tips dunia nzima.

    Wangeenda Misri wakaone Wamisri wanavyodai tip kimabavu. Unapandishwa ngamia, hasimami mpaka utoe tip, akisimama haondoki mpaka utoe tena tip. Akitembea, hakurudishi mpaka utoe tip. Akirudi hakushushi mpaka utoe tip.....
    Now that is FLEECING big time!!

    ReplyDelete
  4. wewe mtoa hii maada ,umeabisha kweli kweli, au hujui kwamba tip nchi zingine ni lazima ?? siku hizi basi huko majuu ,ukipanda teksi,hela iliyojiandika kwenye mita ya teksi utatoa na tipu utatoa na ni huko huko wanakotoka hao watalii wako. Badala ya kutuhamasisha na sisi wakata mbuga tuige , unatukataza !!!! mtu unakaa kwa mama ntilie unakula wali maharage unatoa 1000 na bei yake tuseme ilikuwa 950,basi utaliona libaba lizima linasubiri chenji ya 50 ,badala ya kusema asante na kuondoka. Tuigeni na sisi tabia nzuri za majuu,ingawa siyo zote. Zebedayo msema kweli.

    ReplyDelete
  5. Hawaombi tipu ni RUSHWA ili watoe huduma wanazotakiwa kutoa. Hii ni aibu. Halafu kama mdau aliyesema hapo juu wanaangalia ngozi nyeupe. Mimi nilikuwa na mke wangu waniacha mimi wanamkimbilia mke wangu wakati fubu linatoka kwangu.

    ReplyDelete
  6. HIVI NI LAZIMA WABONGO TUIGE DESTURI MBAYA ZINAZOFANYWA NCHI ZINGINE? KAMA WAMISRI WANADAI TIPU KILA KONA NA SISI TUJITUMBUKIZE HUKO HUKO? HAYA NI MAMBO YA AIBU, U WAPI USTAARABU WETU KAMA WATANZANIA? MKUMBUKE SIO KILA MTALII NI TAJIRI HUKO ALIKOTOKA. KUNA WAALIMU, WASTAAFU, WANAFUNZI NA WENGINEO WANAOPENDA KUONA MANDHARI YA TANZANIA KATIKA UHAI WAO. WAMEJIKUSANYIA VIAKIBA VYAO MIAKA KADHAA ILI WAONE UZURI WA NCHI YETU JE TUNAHITAJI WATALII WENYE MAMILIONI TU? TUACHE OMBA OMBA TUFANYE KAZI. TUSIJIBWETEKE NA KUIGA KWA SABABU WENGINE WANAFANYA HIVI NASI TUJITUMBUKIZE HUMO HUMO. AIBU!

    ReplyDelete
  7. Ndugu zangu. SOMO la JUMAPILI HII naomba liwe nini maana ya TIPU. Tipu ilianzishwa miaka ya 1800 wakati wa enzi za biashara za utumwa na viungo,na hasa hasa waarabu ndiyo walikuwa waanzilishi,enzi hizo Tipu ilikuwa inaitwa bahshishi au barashishi. Ilikuwa na maana ya kutoa asante baada ya kupewa huduma,mbali nakuwa umeilipia hiyo huduma. Lengo lake kubwa hiyo bahshishi ilikuwa kuonyesha upendo zaidi kwa huyo mtoa huduma na kumtia moyo aendelee kuitumikia jamii. Kwa hiyo jamani narudia tena kwamba ,sioni ubaya kama tutaiga yale wanayofanya wengine maadamu ni mazuri na yanasaidia kuiweka jamii katika hali ya udugu zaidi na upendo.Wasalam alekhoum.Zebedayo msema kweli.

    ReplyDelete
  8. Mimi nikiwa kama mdau wa utalii si kubaliani na watoa maoni yao waliotangulia. Kwa baadhi ya sababu na moja kubwa na hii ni kuithani taaluma yako. Mfano Dereva guide kwanza anatakiwa atekeleze wajibu wake kwa kiwango ambacho kinahitajika au hata kupitiliza matarajio ya mgeni anaye muhudumia ndipo mwisho wa siku tunasema anstahili pongezi na ahsante(TIP) kutoka kwa mgeni. Kufanya kazi yake vizuri ni wajibu sio ombi au sio hisani kwa mgeni huyo. Sasa kama haitoshi vituko vikubwa vipo katika migahawa ya chakula Muhudumu hajui chochote kuhusu chakula anacho muhudumia mteja na akiulizwa swali lazima atafute msaada Lakini anaona nihaki yake kupata hiyo tip. Jamani tip ni kipato cha ziada anachotoa mteja baada ya kupata huduma nzuri. Ni kweli kabisa tumeshuhudia wageni wengi wakiwa hawana raha baada yakuwekewa mazingira ya kulazimisha tip. Na mie siungi mkono kwamba kila linalofanyika Huko Ulaya au Marekani tuliige, sisi kama watanzania tuna utamaduni wetu bwana nalazima tuheshimu hayo ili tulinde thamani yetu kama watu si vinginevyo.Jambo muhimu hili soko la Utalii liachane na swala la cheap labor waajiriwe watu kwa Taaluma na uwezo wa kufanya kazi hizo tunahitajika kulinda soko La utalii Tanzania na to focus kwenye Quality tourism sio mass tourism hii itafanya mabadiliko mengi mno tusitumie kuharibu sifa ya nchi kwamba tunatengeneza ajira huwezi tengeneza ajira wakati unavunja sifa ya hilo soko la utalii ambalo hivi sasa limevamiwa na watu wengi wasio na uwezo wa kufanya hizo kazi. Zamani huku kanda ya kaskazini kila mtoto akifeli shule anaishia Garage kutengeneza magari lakini sasa hali Imebadilika kila anefeli shule basi anaenda soma short course za utalii na ndo hao wanaogeuka proffessional omba omba kwa watalii.

    ReplyDelete
  9. Kabula ya kuchangia huu mjadala, jiulize tipu ni nini? Kwa nini mhusika atoe/anatoa tipu?
    Endelea sasa!

    ReplyDelete
  10. Mzaha mzaha hutumbua usaha!

    Hizi zote ni dalili za mwanzo wa kukua kwa 'rushwa' kwa kuwa hata mti wa mbuyu huanza ukiwa kama mmea wa Karanga.

    1.Kiustaarabu tipu haiombwi ni mapak upewe tena kwa ridhaa ya mtoaji na sio kwa kumwonyesha uso wa kutia huruma ama 'smilling cat' maana unapokuwa unakula msosi wa minyama minyama paka hupenda kuzungukia chini ya meza huku akipekesa mkia wake na kulia lia, ile ni njia ya kuomba msosi!,,,kitu kama wanavyofanya waomba tipu ktk huduma.

    Na ingefaa hata kama mtu akikupa kwa ridhaa yake ukatae, sio wajibu kuwa ndio utamaduni kila umhudumiaye lazima atoe,,,ndio mbuyu sasa unaanza kukua hivi hivi!.

    2.Hii kitu inatudhalilisha sana na inajenga picha mbaya kama Taifa la njaa kali na omba omba, hivyo watu wanaotoka jamii zilizo endelea wanajua huo ni mwanzo mbaya kijamii.

    Ndio baada ya kukomaa na kuota mizizi (tipu) inakuwa ndio rushwa kamili!

    ReplyDelete
  11. Mdau wa 08:35am
    Soma na uelewe mwandishi aliyetoa mfano wa Misri kasema nini.
    Au ndio mwoshakinywa umombo umekupita?
    Baada ya kutoa mafano wa Misri, jamaa kamalizia kwa sentensi moja yenye maana nzito;
    "Now that is FLEECING big time."
    Uliielewa hiyo?
    Au unataka upewe darasa????

    ReplyDelete
  12. Na mimi nakubali Misri wanaongoza kuomba Tip wenyewe wanaita Bakshish. Nililala hotel nilipokuwa on transit nilikoma. Nilidhani ni watu wakarimu walipokuwa wananiongoza wapi pa kufanya hiki wapi pa kufanya kile...nlichoka walipoanza kunidai cha juu...na walikuwa kwenye uniform mi nkadhani ni kazi yao hawapaswi kulipwa.

    Sikuwa na ela ndogo nilitoa Euro yangu ya maana roho iliniumajeeee?

    Warning. Kwa wasafiri wanaopita Egypt wawe makini wasikubali mtu yeyote anayejidai kusaidia bila kuombwa...utadaiwa bakshishi tena kwa sauti maanake siyo siri ni tamaduni yao.

    Hata dereva wa bus la hotel alichukua bakshish karibu kwa kila mtu...wakati bus ni bure kwa wasafiri wa Egyptaire. Mi sikumpa..anacheza. walimpa wazungu tu.

    Ila yeye alikuwa alii njaa kama hawa wa kwetu

    ReplyDelete
  13. Hivi nyie mnaotaka tuige tamaduni za ulaya na marekani kudai/kuomba tip hamuitakii sekta ya utalii uhai. Hao hao wazungu ndio wanaokuja kutembea Tanzania na kupeleka sifa nzuri huko kwao kwa kupata huduma nzuri kutoka kwa staff wa tours. Hivi wakiacha kuja na nyie waomba tip mkakosa ajira mtafanya nini? Acheni kuiga tembo kunya, hawa wenzetu wanatabia mbaya ya kuweka vitu hadharani, wanaambiana kila kitu wanachokiona huko wanakotembelea.

    Fanyeni kazi kwa kuwa mnalipwa, na hata kama mshahara ni mdogo hiyo ni juu yako maana hukulazimishwa kufanya kazi, mtalii analipa hela yake kupata huduma na kujifurahisha baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu, tatizo watz hamna culture ya kutembelea maeneo tofauti duniani au kwenda holidays.

    Mwisho tip ni asante atoae mtu baada ya kupokea au kufurahishwa na huduma aliyopewa, na sii lazima ipokelewe kwa kuwa huduma ile imelipiwa, achane kutangaza njaa zenu kwa wageni, ndo maana hawaishi kutudharau.

    ReplyDelete
  14. Mimi kwa kweli tip natoa lakini kwa huduma niliyoridhika nayo tu na sio kwa kulazimishwa. Nahisi hata huko Egypt huyo ngamia akigoma kuinama nishuke ntaruka tu, potelea mbali......

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...