Ankal Michuzi na wadau,
Habarini za masiku. Mimi ni mdau nimerejea punde kutoka ughaibuni, hivi sasa nnatesti zali kama nibaki kimoja ama vipi. Hadi sasa mambo si mabaya sana, kwani ukiondoa matatizo madogo madogo kama vile ya urasimu usio lazima, watu kuishi kwa kukariri badala ya ubunifu, ujuaji (wakati alosto) wa kila jambo na kukosa kujua kinachoendelea duniani, hali si mbaya kihiiiiivyo hapa nyumbani. Vyanzo vya mkwanja kibao, na wala huhitaji kuwa na munguBaba kuweka mambo sawa.
Toka nirudi nina kama mwezi mmoja na ushee hivi. Kilichonifanya niandike leo ni hivi vyombo vya habari hapa nchini, hususan TV, ambazo kwa kweli zinatia hata hasira. Hakuna vipindi vya maana vya hapa nyumbani na kama vipo ni kutoa malalamiko weeeeee na kulaumu serikali na kila mtu kuwa hili na lile halifanyiki. Na wote unaowaona wanalalamika hakuna anayetoa solutions. Jamani hii nchi ni ya kulalamika na kulalamika na kupinga kila sheria iliyopo???? Yaani sijaona kipindi chenye kuonesha watu wanaoongea sauti za chini wakijadili mambo bila kulalamika. Kila kipindi ni jazbab na milawama tu hadi inaboa!
Ankal, mtandao wako unasomwa na wengi, na nna imani wengi hao ni pamoja na wahariri wa hizo TV. Sitaki kumfundisha mtu kazi, ila angalia TV za Tanzania kwa muda kishs fungulia za hapa hapa Kenya, Uganda ama Zimbabwe tu utaona tofauti. TV yetu ambayo nimeambiwa ndiyo ya Taifa ndiyo usiseme. Ati wao wanafungua saa 12 asubuhi na kutangaza hadi saa 2 asubuhi kisha wanapasia TV za nje. TV ya Taifa kweli ina watu wabunifu kweli. Unawanyima wananchi walipa kodi na mishahara yako kwa kutega kwa kisingizio cha ukata. TBC hamna ubunifu kweli ya kuwa na vipindi kama vya discovery channel ama National Geograpphic??
Acheni hizo jamani. Mnashindwa hata na Clouds TV ambao pamoja na kuchapia kwa mtindio wa weledi kwa watangazaji wake wengi (wanaonekana hawana training, na ujuaji umezidi, na hakuna consistency) lakini angalau wana habari kibao za nyumbani. Na si habari tu bali habari zinazochangamsha. Nikiangalia makala za TBC one aidha ni ya zamani sana na kama ni ya sasa haina ubora wa picha ama sauti ama mada yenyewe.
Naomba mjirekebishe!!
Mdau Mstaafu wa Ughaibuni
Sasa Mdau mbona unachokisema ndo unacholaamikia pia? Ulalamishi...!!! Hebu soma hiyo article yako uniambie umetoa solution gani zaidi ya kulalamika? Yale yaleee, walewaleee...!! Mdau, USA, California.
ReplyDeleteBaelezee babaake!
ReplyDeleteMbona sasa na wewe umerudi pale pale kwenye kulaumu?
ReplyDeleteKama mambo yanaenda vibaya kwanini tusialaumu tena kwa jaziba! Tunawalipa kodi halafu wanatuletea vipindi kama hivo tena vipindi vyenyewe viko biased halafu tukae kimya. Mdau kulalamika ni sehemu ya maisha kama nami ninafanya sehemu yangu ya maisha nae afanye sehemu yake. Nalipa kodi nae anipe huduma. Vitu vingine vinatia hasira huwezi kuviacha viende tu hovyo hovyo
Mstaafu wa ughaibuni wewe unafikiria kutengeneza program kama za discovery huo ni bure? Kwanza inahitaji fedha nyingi, pia ujasiri wa wapiga kamera. Wapiga kamera wa TZ hawajui hata kuogelea sasa unafikiri watatengeneza filamu ya bahari lini? Watengeneza wa zile filamu za discovery wanapata mamilioni ya pesa maana kuna TV nyingi sana wananunua hizo filamu zao. Ile filamu ya Serengeti wale jamaa walikaa Serengeti mwaka mzima kule. Walimtafuta simba mpaka wakamuona anavyozaa. Wale maproducer ni matajiri. Ndio maana watu weusi tunaonekana wajinga maana hatua akili ya kijasirimali.
ReplyDeleteYAANI BADO UNA MAWAZO ETI TBC NI TV YA TAIFA. WENZIO TULISHA SAHAU SIKU NYINGI.
ReplyDeleteINAONEKANA UMEKAA SANA NJE HUJUI KINACHOENDELEA BONGO.
PILI, UKWELI NI KWAMBA BAADHI VYOMBO VYA HABARI VIMEJAA UDAKU TU.SOMA MAGAZETI KARIBU YOTE YAMEJAA UZUSHI NA UNAFIKI, KEJELI NK. TV MUDA WOTE NI MAJUNGU NA MATANGAZO YA BIASHARA BASI.
BLOGGERS NAO WAPO KIBAO. HAO NAO KAZI YAO NI COPY AND PASTE. UKIZINGATIA HAWANA TAALUMA NDO KABISAAA INAKUWA VURUGU TUPU.
LAKINI WIZARA YA HABARI IPO, NA INAFANYA KAZI. ILA USIULIZE INAFANYA KAZI GANI.
KENYA WANA TV PROGRAMS NZURI ZA KITAALAMU ZA WAKENYA ZINAZOTENGENEZWA NA WAO WENYEWE, HATUWEZI KUJIFUNZA CHOTOTE? KWA MFANO KUNA INVESTIGATIVE JOURNALISTS WA KTN MOHAMED ALI KIPINDI CHA JICHO PEVU YEYE NA WENZIE WANACHUNGUZA UTAPELI, RUSHWA, MADAWA YA KULEVYA HALAFU VINARUSHWA NA TV. VERY EDUCATIVE AND HEROIC. MBONA BONGO HATUJARIBU? WANACHUNGUZA WACHUNGAJI FEKI, POLISI WALA RUSHWA. WATANZANIA HATA KUJARIBU
ReplyDeleteMama weee!! Mungu kasikia kilio changu, wameanza KURUDI, asante sana mdau wa ughaibuni kwa kurudi Bongo, na nakusifu sana kuyaona mengi na kwa kipindi cha mwezi mmoja tu, hee !! bongo imejaa neema sana,Tannesco wameiba weeee wala sisi wananchi hatujaandamana hata siku moja, tunaachwa gizani basi tunawasha vibatali tunalala , wakubwa wanachota pesa zote za mauzo ya tannesco na kutudanganya eti wananunua nguzo za umeme kutoka South, wizi usiyo na huruma.Mdau karibu sana Bongo.Ushauri wangu kwako ni huu, tafuta cha kufanya ufanye ,una mwanga mzuri wa maisha na uwezo wa kufanyakazi unao, rushwa zipo na kuzibiana riziki kupo,visikutishe,just blend in ,usitafute sana haki-utapasuka kifua.Achana na mambo ya TV, mimi hata hiyo TV siitazami ,im so busy with many good stuff. Nitakushangaa sana kwa weupe wa mawazo uliyonayo , kumbe tena na wewe unakosoa yasiyo na maana ??.
ReplyDeleteAcha kufuru wewe! "huhitaji munguBaba kuweka mambo safi" unamaanisha nini?
ReplyDelete