Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisoma hotuba ya kuwahamasisha wananchi kushiriki Sensa ya Watu na Makazi kwa mwaka 2012.

Ndugu wananchi;

Imekuwa ni mazoea yetu kuwa Rais huzungumza na taifa kila mwisho wa mwezi. Lakini, leo nazungumza nanyi siku saba kabla ya mwisho wa mwezi kwa sababu maalum. Sababu yenyewe si nyingine bali ni Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika kwa siku saba kuanzia kesho Jumapili tarehe 26 Agosti, 2012. Shabaha yangu ni kutaka kuwakumbusha Watanzania wenzangu wote kuhusu wajibu wao wa kujitokeza kuhesabiwa siku hizo. Naomba kila mmoja wetu ahakikishe kuwa anakuwepo kuhesabiwa na kujibu maswali yote yatakayoulizwa na makarani wa sensa kwa ufasaha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ma'ansha'Allah!Mh wetu Rais hapo mbona umeonekana kijana sana!Ramadhani imekusafisha nini?....Utafikiri ni wa miaka hiyoooo ya 2000 au 2006 ya waziri wa mambo ya nje,au enzi za campaign!
    Mimi Urais hata nikipewa bure siutaki,,maana unazeesha sana!hata rafiki yako Obama nae kazeeka ndani ya mika 4 tu!
    kichwa cha rais kinajazwa mambo mengi
    kuzidi uwezo wake,matokeo yake mvi zinachachamaa kicwani!
    Kila la Kheri Rais wetu!Mwenyezi Mungu Akuja'alie Afya njema,maisha marefu na familia yako na watanzania wote kwa ujumla
    Ahlam...London

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...