UTANGULIZI
1.          Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Fedha na Uchumi, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu likubali kupokea, kujadili na kupitisha Makadirio ya Mapato, Matumizi ya Kawaida na ya Maendeleo ya Wizara ya Fedha kwa mwaka wa fedha 2012/13.

2.          Mheshimiwa Spika,  awali ya yote napenda kutumia fursa hii kutoa pongezi zangu za dhati kwako pamoja na Naibu Spika Mheshimiwa Job Yustino Ndugai, Mbunge wa Kongwa, Waheshimiwa Wenyeviti Jenista Joakim Mhagama (Mbunge wa Peramiho), Sylivester Massele Mabumba (Mbunge wa Dole) na Mussa Azzan Zungu (Mbunge wa Ilala), kwa kuongoza vema majadiliano ya Bunge la Bajeti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...