Taasisi ya Maendeleo ya Kiuchumi na Mipango ya Afrika (IDEP), ni moja ya taasisi zilizoanzishwa na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwaka 1962. Lengo kuu likiwa ni kuendeleza na kuinua shughuli za kiuchumi barani Afrika. Sambamba na hili IDEP inaratibu mafunzo kwa ajili ya kuwajengea uwezo watalaam katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo. IDEP inaongozwa na Bodi ya Magavana ambayo Tanzania ni mjumbe wa Bodi hii. 

Katika kipindi hiki, IDEP itaendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo watalaam kutoka nchi wanachama wanaoratibu shughuli za kimaendeleo.  Kozi zitakazoendeshwa ni pamoja na Sera za Viwanda, Sera za Madini, Mikataba. N.k. Kwa taarifa hii fupi Ndugu Watanzania Wenzangu tunaoratibu shughuli za kimaendeleo katika taasisi za Umma na sekta binafsi tuombe kozi hizi kwa manufaa ya nchi yetu. Kwa taarifa  tembelea www.unidep.org humu utapata fomu na taarifa zote muhimu kwa ajili ya kozi hizi. Aidha, IDEP inatoa ufadhili wa kozi hizi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...