Mgombea nafasi ya Uewenyekiti Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT),Halima Mohamed Mamuya akirudisha fomu ya kuomba kugombea nafasi hiyo kwa Mkuu wa Idara ya Oganaizesheni UWT Makao Makuu Riziki Kingwande jijini Dar es salaam jana.Mamuya aliyekuwa Katibu Mkuu wa zamani wa umoja huo, anakuwa mtu wa tatu kujitokeza kuwania kiti cha uenyekiti wa UWT ngazi ya taifa.
Home
Unlabelled
Mamuya ajitosa kwenye kinyang'anyiro cha UWT ngazi ya taifa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


Safi sana mamaa chukua kiti uimarishe jumuia iliyokufa hiyo.mh rais nae aelewe hao watu wake wanamuangusha sasa ni wakati wa kuimarisha chama.ccm oyeeee
ReplyDeleteHongera Halima, naamini unaweza, unajiamini, unastahili na pia uhakika upo wa kushinda na kuinyakuwa nafasi hiyo ya uwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT). Nakuombea kila la kheri ufanikiwe INSHA ALLAH.
ReplyDeleteI support you Halima Mamuya. Tulikuwa wote Ruvu na Mbweni JKT.
ReplyDeleteJamani hivi kila mtu anamjua huyo Mamuya? Maana habari hata haisemi ni yupi kati ya hao wawili!
ReplyDeleteHuyo halima ndio yupi katika hyo picha? nani anamkabidhi form mwenzie katika hiyo picha?
ReplyDeleteMimi Halima simjui lakini picha inaonyesha kuwa ni wa Kushoto,,Maana chekaji ya wa kulia,inaonyesha yeye mwenyeji hapo,na tabasamu la wa kushoto linaonyesha kaleta hiyo fomu..
ReplyDeleteKwa upande mwingine naweza kusema Halima ni wa Kulia maana inaonyesha kisha kabidhi fomu kisha anataka kutoa mkono kwa mpokeaji fomu,vile vile wa kulia inaonekana yuko kweli ofisini kwake.
Inatatanisha sana,,Ingekuwa majina ya dini tofauti tungejuwa nani kajistiri Ramadhani!
Ahlam...London
Mamuya mi naona huyo alievaa magamba
ReplyDeleteHongera sana Da-Halima. Ila hatutarajii kina mama mnaogombea nafasi hiyo ya uongozi kutukanana kama watoto, tafadhali sana epukeni kutupiana matusi na kashfa. Uchaguzi uliopita ilikuwa aibu tupu, malumbano, kashfa na matusi ya kila aina kutoka kwa watu wazima na waliokuwa wanaheshimika katika jamii, kisa????? uenyekiti wa UWT. Chonde, chonde jamani, msitudhalilishe wanawake wenzenu. Mkubali na kuelewa kuwa asiyekubali kushindwa si mshindani. All the best big girls!!!
ReplyDeleteHalima ni huyo mwenye nguo zenye rangi ya chama chetu.
ReplyDeleteHalima ni huyo mwenye mawani na amevaa kitenge cha KIjani, mtandio wa njano. Kwa mliosema hamumjui Halima ni yupi.
ReplyDelete