Balozi wa Marekani anayeshughilikia maswala ya Uhalifu unaofanywa wakati wa Vita,Balozi Stephen Rapp (pichani) amerudia wito wa taifa lake kuwa itatoa kiasi cha Dola za Marekani milioni tano katika kufanikisha kupatikana kwa watuhumiwa wa kadhaa wanaodaiwa kusababisha mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994.
Balozi Rapp alitoa kauli hiyo leo baada ya kufanya ziara yake kwenye mahakama ya Kimataifa ya Rwanda(ICTR)yenye makao yake mjini Arusha,Tanzania na kuwataja watuhumiwa watatu ambao Marekani imesisitiza kuwa ahadi yake ya kutoa kiasi hicho cha fedha iko palepale ili wafikishwe mahakamani mjini Arusha ni Felicien Kabuga ,Protais Mpiriranya na Augustin Bizimana.
Pia watuhumiwa wengine ambao serikali ya Marekani imeahidi kutoa kifuta jasho kufanikisha kufikishwa mbele ya haki ambao kesi zao zimehamishiwa nchini Rwanda ni Jean Uwinkindi na Bernard Munyagishari na wengine ni Fulgence Kayishema,Charles Sikuwabo,Ladislaus Ntaganzwa,Ryandikayo na Aloys Ndimbati.
Katika Mkutano huo pia Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya kimataifa ya Rwanda(ICTR)Hassan Bubacar Jallow alishukuru mchango mkubwa unaotolewa na serikali ya Marekani kwa Mahakama hiyo



Unanatuchanganya mbona kwenye mabano umeweka elfu tano wakati unasema million tano, imekaaje hii?
ReplyDeleteHiyo ni dola milioni tano au elfu tano???
ReplyDeleteKwa habari za ukweli mauji ya kimbari Rwanda chanzo ni Kagame mwenyewe. Yeye ndiye aliyeanza kuua watu toka mwaka 1990 na ndiye anayehusika moja kwa moja na vifo vya marais watatu wa afrika (Burundi, Rwanda, na Kongo). Kagame akamatwe na afunguliwe mashitaka. Bila huyu Kagame yale mauaji ya kimbari yasingetokea Rwanda. Kwanza akamatwe yeye kisha wengine.
ReplyDelete