Mratibu wa mashindano ya soka ya vijana katika Mji Mdogo wa Utete, Rufiji, Mtangashari Mtolia (kulia), akielezea jinsi mashindao hayo yatakavyoendeshwa katika kiutano uliofanyika mjini Utete jana. Kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya mashindano hayo, Uwesu Omari na Mweka Hazina Khamis Mninge. Washindi wa michuano hiyo itakayoanza Agosti 26, mwaka huu,watazawadiwa ng'ombe, mbuzi, jogoo na kondoo. 
PICHA NA HABARI NA RICHARD MWAIKENDA

MASHINDANO ya kugombea zawadi ya ng'ombe, yatakayoshirikisha timu 16 za vijana yanatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu katika Mji Mdogo wa Utete, wilayani Rufiji, Pwani.

Akizungumza na Jambo Leo mjini Utete juzi, Mratibu wa mashindano hayo yatakayojulikana kama Vijana Cup, Mtangashari Mtolia, alisema kuwa lengo la michuano hiyo ni kuibua na kuvikuza vipaji vya soka kwa vijana wilayani humo.

Alisema kuwa wachezaji hao watakaokuwa na umri kati ya miaka 20 na 25, watatoka katika Kata tatu zinazounda mji huo wa Utete, ambazo ni Utete, Chemchem na Ngarambe.

Mtolia alisema, mashindano hayo yatakayofanyika kwa mwezi mzima kwenye Uwanja wa Azimio mjini Utete, yataendeshwa kwa mtindo wa makundi na baadaye Ligi mpaka atakapopatikana bingwa.

Alisema, kuwa timu bingwa itazawadiwa ng'ombe dume, wa pili atazawadiwa mbuzi wawili beberu, mshindi wa tatu mbuzi mmojja na jogoo halafu wa nn ataambulia kondoo.

Aliwataja wadhami wa michuano hiyo kuwa ni Mjumbe wa Baraza la Michezo Taifa (BMT), Kamishna Msaidizi wa Polisi, Jamal Rwambow na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mdogo wa Utete, Masoud Jah.

Mahindano hayo yatakayofunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Nurdin Babu yataongozwa na kamati , ambayo wajumbe walitajwa kuwa ni; Uwesu Omari (Mwenyekiti), Mtengashari Mtolia (Katibu),  Khamis Mninge (Mhazini), Athuman Sule, Ali Mopele na Mohamed Kipepe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Kichekesho kitupu na usanii mtupu. Kwanini usitoe zawadi ya kudumu kama vikombe na unatoa nyama ya kula siku moja tuu? Kwa mtaji huu tusitegemee maendeleo ya soka zaidi ya kuganga njaa tuu kwani tunawafundisha vijana kuganga njaa kwa zawadi za nyama.

    ReplyDelete
  2. Wasomi na watalamu wetu Mungu awape imani na huruma kuteremka chini na kuwa saidia watu. Changamoto kama Anonymous alivyo sema ina tumiwa na viongozi kufanya watu wajinga.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...