salaam, mambo vipi habari za siku nyingi

naomba uniweke tangazo naitafuta gari yangu nilimuazima rafiki yangu kaingia nayo mitini nimeshatoa ripoti polisi

REGISTRATION NUMBER: T445 AMS
MAKE: TOYOTA
MODEL: HARRIER,STATION WAGON
COLOR: SILVER, 2001

UKIIONA WASILIANA NA MIMI 0716 041044

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. mh! ubinadamu kazi.
    simu walikua wanaiba hivyo, sasani magari.

    ReplyDelete
  2. Pole sana. Siku hizi hutakiwi kumuamini mtu yeyote.

    ReplyDelete
  3. we muongo kama kweli aliyekuibia ni rafiki yako tuwekee picha yake .. tuanza kumfuatilia haiwezekani rafiki yako huna hata picha yake hana hata fesibuku >?>>

    ReplyDelete
  4. hatukuamini.
    hujaweka jina lako wala la huyo unaedai katoweka na gari lako wala eneo la tukio.
    ni nini nia na makusudio yako?

    ReplyDelete
  5. Rafiki yako kabisa hawezi kuingia na gari lako mitini.Haa haaaa..Pole sana.Magari watu wanaazimana kila kukicha na marafiki zao kwenda masafa marefu..huyo siyo rafiki yako,ni adui wako.

    ReplyDelete
  6. JITU ZIMA OVYOOOO.
    UMEIBIWA GARI UNAITAFUTA HATA JINA LAKO HUJITAJI.
    PILI JINA LA HUYO RAFIKI YAKO HUJAWEKA ILI WATU WAJUE. ARE YOU SERIOUS? AU UMEIBIWA NA CHANGUDOA USIYEMJUA JINA MKIWA GUEST HOUSE?

    WATU KAMA NYIE NDIO MAANA MNAIBIWA.

    ReplyDelete

  7. Ni "rafiki yako" wa kike au wa kiume?

    ReplyDelete
  8. Hivi inakuwaje mtu unamuazima mtu gari?. Gari si kitu cha kuazima binafsi ni bora mtu nimpatie hela ya tax kuliko kumuazima gari ni tabia ninayoichukia na kuikana. Huu ujamaa wetu sasa unataka kupitiliza, tunakoelekea sasa watu wataanza kuazimana nyumba etc. Ukitaka kujua implication ya kuazima gari basi ukate thefty insurance yeye kuambatana na comprehensive. Hebu tuache tamaduni za kujima hizi inakuwaje unamuazima mtu chombo chako cha usafiri akienda kulegeza kitu ili akupigishe mzinga utamlaumu nani?. Bora lawama kuliko!, Liwalo na liwe kuazimana gari mwiko kwangu. Siku akitaka kukuazima mkeo/mumeo amsindikize kwenye Receiption party utamkatalia?

    ReplyDelete
  9. Che GuavaraAugust 28, 2012

    Atakuwa ameibiwa na Hawara yake ndio maahna anaficha ficha

    ReplyDelete
  10. Jamani mnaomlaumu huyu jamaa hamna upeo. Rafiki ni rafiki tu. Na huyu walikutana kwa mara ya kwanza siku hiyo hiyo club na yeye alikuwa ndiiii, wakakubaliana wawe marafiki na kwenda kupumzika. Asubuhi anaamka rafiki hayupo, hamkumbuku jina, sura wala kuwa anaishi wapi na gari limeshaondoka!! pole sana mdau hili ni fundisho kwa watu wote.

    ReplyDelete
  11. Wabongo wana tamaa sana na vitu vya muonekano kama magari na anasa anasa.

    Jamaa Muungwana hana makosa kwa kumuamini Rafiki aliyekuwa mnafiki.

    Ndio maana jamaa kwa usmati na wema wake alipoombwa gari akatoa kwa moyo wake mzuri.

    Sasa wajameni mtu huna gari, au hata kama unalo una dharura ya nini kumkerehesha mwenzio kwa kumuazimia chombo chake cha usafiri?

    Kwa nini kama huna gari usikodi taxi?

    ReplyDelete
  12. Siri ya mtu ni kichaka!

    Ama kweli unaweza kumuamini mtu ukidhani unaye mshirika wa ukweli kumbe anakulia mahesabu.

    Katika maisha changamoto kubwa kwetu ni kuwa ni vigumu kuelewa mtu ana mawazo gani akilini mwake ama moyoni mwake.

    Isipokuwa unakuja kumuelewa mtu baada ya tendo atakalo kufanyika ndio utakuja ona lengo lake lilikuwa ni nini?

    Vile vile, kama ukiwa ni mtu uliyechaguliwa unaweza kumgundua mtu ambaye ana lengo baya dhidi yako.

    Kwa dalili hizi:

    1-Mtazame usoni hasa akiwa anaongea na wewe utaweza kusoma alama za Kisaikolojia ktk uso wake na kubaini ya kuwa ana mpango dhidi yako (Mungu amebainisha uso wa mnafiki kwa dalili).

    2-Jaribu kumuacha peke yake akiwa ana uhakika kuwa haupo kisha tokeza ghafla utaona anashituka kidogo ama anakuwa na wasi wasi.

    3-Atakuwa na ka uwoga fulani hivi au mashaka hasa akiwa anaongea atakuwa anajikanyaga kanyaga kwa kupindisha kauli zake ana anaongea kwa kuji gonga gonga na kuwa na wasi wasi kama utamchunguza kwa makini.

    4-Atakuwa na haraka zisizokuwa na msingi wowote, atakuwa anapumua kwa kutweta lakini kwa mhalifu mkomavu anao uwezo mkubwa wa kuficha hii dalili.

    5-Kubwa ya yote uso wa Mnafiki haujifichi una kitu kinaitwa 'smilling cat' yaani paka anaye tabasamu kiuongo.

    Hizo ni dalili 5 za Kisaikolojia kwa mtu mwenye hila dhidi yako ya kuwa kuna kitu kinaendelea moyoni mwake au akilini mwake kwa siri,,,MTAMBUE!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...