Habari zimetufikia punde kwamba magari matatu yameshika moto Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar usiku huu. Inasemekana moto ulianzia kwenye gari moja aina ya Range Rover kabla ya kusambaa kwenye magari ya aina ya Toyota na Corolla kabla ya kuzimwa na zimamoto waliofika hapo muda mfupi baadaye. Habari zaidi baadaye....
Home
Unlabelled
moto wachoma magari matatu uwanja wa ndege dar usiku huu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


Vipi michuzi Mbona Hamna habari za binti aliyebakwa hadharani vingunguti kwa kuvaa uchi? Naona ni kitu wasomaji wako wangehitaji kujua kabisa
ReplyDeleteHaya Magari Freelander / Range Rover yote Jamii ya landrover sijui yana laana Gani? Any way Nina kama matukio Matatu nimeshughudia haya aina ya Magari yakiungua Moto!!
ReplyDeleteKwani corolla si Toyota ?
ReplyDeleteHizi Range za kununua kwa dili ndio tatizo lake. Poleni wahusika wote.
ReplyDeletePole kwa waathirika wote. Tukio hilo lingetokea mbali na Uwanja wa ndege sipati picha madhara yangekuwaje.
ReplyDeleteMdau wa kwanza hiyo habari ya binti kubakwa si kazi ya MICHUZI peke yake maana si kwamba kila tukio analijua. Wewe kama ulikua unaifahamu ulitakiwa umtumie na ametoa contact zake for any BREAKING NEWS hivyo ni jukumu lako pia kumtumia ili yeye afanye verification ya hizo information
ReplyDeleteMdau Igwamanoni wa Itabagumba