Mashabiki wa bendi pinzani za Msondo Ngoma na  Mlimani Park Orchestra (Wana Sikinde Ngoma ya Ukae) leo mchana watafurikia kwenye  viwanja vya Leaders Club, Kinondonikushuhudia bendi gani itaibuka mshindi.
Pambano ya leo imeandaliwa Keen Arts na kudhaminiwa na Konyagi kwa ajili ya kukusherekea Sikuku ya Iddi.
Takribani mwezi moja iliyopiata bendi hizo zilikuwa zikijiandaa na pambano ya leo ambao itamua ni bendi gain itaibuka mshindi 2012.
Mratibu wa mchuano huo Joseph Kapinga amesema pambano ya leo litakuwa la aina yake ukizingatia kuwa bendi zote zimekamilika.
Kapinga alisema ili kuondoa malamiko ya kuhujumiwa, kila bendi itatumia jukwaa lake. “Litakuwa pamabano la aina yake ukizingatia kuwa itakuwa ni mara ya kwanza kwa bendi hizi pinzani kupambana siku ya sikukuu ya Iddi tangu zianzishwe,” alisema Kapinga.
Pia itakuwa ni mara ya kwanza kwao kushindana katika viwanja vya Leaders Club.
Kapinga alisema mchuano huo itaanza saa nane mchana hadi liamba.
Msondo itaingia jukwaani ikitokea Dodoma ilikokuwa imeweka kambi, huku Sikinde ikitokea mafichoni.
Sikinde itakuwa ikiwategemea wanamuziki wake ambao wamewasili hivi karibuni wakitokea nchini Marekani ambao ni Hassan Rehani Bitchuka na Ally Jamwaka. Wengine ni Hassan Kunyata, Abdallah Hemba, Habib Jeff, Yusuph Benald na wengineo wengi.
Msondo itakuwa itatawakilishwa na Muhidini Maalim Gurumo, Said Mabera, Hassan Moshi, Shaaban Dede, Eddo Sanga, Abdul Ridhiwani na wengineo.
Mwaka jana bendi hizo zilipambana vikali kwenye ukumbi wa TCC Club sikukuu ya Krismasi ambapo mbali na muziki safi na vituko vya hapa pale zilitoka sare.
Mratibu huyo amesema kuwa mwaka huu mshindi ni lazima apatikane hata kwa kurusha shilingi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...