Naibu katibu mkuu wa UVCCM Zanzibar, Jamal Kasim Ally akimkabithi fomu za kugombea nafasi ya uongozi wa UVCCM-NEC Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Bw Jerry Silaa jana katika ofisi za CCM mkoa mjini magharibi Zanzibar, (ktk) mwenye suti nyeusi ni Bw Abdallah Mwinyi-katibu wa vijana mkoa kusini unguja akishuhudia tukio hilo. UVCCM -NEC imetangaza nafasi zinazogomewa kua ni Mwenyekiti, Mkamu mwenyekiti, Katibu, wajumbe wa baraza kuu na wajumbe wa halmashauri. 

Hata hivo mstahiki meya wa manispaa ya ilala alipohojiwa hakuweka wazi nafasi gani anayotaka kugombea kwani alikua bado anakusanya maoni na ushauri kutoka watanzania mbalimbali na kujipima mwenyewe ni nafasi ipi itakayo mfaa zaidi ili kuweza kuwatumukia wananchi vema.Tetesi kutoka kwa wadau wake wa karibu zinasema  mstahiki meya anataka kugombea nafasi ya Mwenyekiti UVCCM-NEC.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. biashara hiyo kila mtu sikuhizi anaitaka maana ina faida sana

    poleni sana watanzania mliokuwa na hali ngumu A.k.a walalahoi jasho lenu linaliwa na wachache.

    ReplyDelete
  2. Hivi kuna nafasi hiyo Mwenyekiti UVCCM-NEC? Au ujumbe???????

    ReplyDelete
  3. Huyo anafaa ni kijana makini na mpenda maendeleo. Kwa hivyo watu wafanyeje? Wote wakauze machungwa au wote tulale hoi, kazi zisifanyike au kwa hivyo watu wafanyeje namuuliza ndugu yangu anon Sat Aug 04, 03:53:00 PM 2012, hayo maneno ya mkosaji kama unaipenda nchi yako toa mawazo ya maendeleo sio ya kuchochea chuki.

    ReplyDelete
  4. Kaka songa mbele ktk kujenga chama Chetu.

    ReplyDelete
  5. he is a smart guy. real he deserve any post. BIG UP JERRY

    ReplyDelete
  6. Imefika wakati hata wamiliki wa blog kuchuja maoni kuna maoni unayaona hayana nia njema zaidi ya kupandikiza chuki humu.....kama siasa tuifanye kwa masingi ya maendeleo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...