Timu ya Hassan Maajar Trust (HMT) inapenda kutoa shukurani kwa wote waliotembelea banda lao kwenye maonyesho ya Dar Fashion Festival 2012 yaliyofanyika tarehe 18-19 Agosti kwenye viwanja vya TTCL jijini Dar es Salaam
Hapo kwenye banda la HMT watu mbalimbali waliweza kuleta nguo, viatu, vitabu, mabegi, na vitu vingine kwa ajili ya duka laola HISANI linalopatikana Mikocheni – Jengo la Arcade gorofa ya chini. WOTE MNAKARIBISHWA KUTEMBELEA DUKA HILO KUNUNUA VITU MBALIMBALI KWA BEI NAFUU SANA NA PIA KUPELEKA VITU VYAKO USIVYOVITUMIA TENA (Kama nguo, viatu, mabegi, na kadhalika).
![]() |
Mbali na hayo HMT pia inaendesha kampeni ya “CHANGIA DAWATI” ambapo unaweza changia kiasi chochote kadri ya uwezo wako ili kuwezesha watoto wa shule za msingi kusoma kwa ufanisi zaidi. Yote haya ni katika jitihada za kuhakikisha elimu bora kizazi kijacho hususani Tanzania. Kwa mawasiliano tafadhali tembelea tovuti yetu: http://hassanmaajartrust.blogspot.com/ |




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...