Wakati siku zikikaribia za kufanyika zoezi la Sensa ya watu na makazi, Mratibu mmoja wa Elimu Kata ya Vugiri wilayani Korogwe, Tanga, Juma Salehe (52) amekamatwa na polisi akihamasisha mitaani kwa kipaza sauti wananchi walikatae zoezi hilo.
Habari zimesema mratibu huyo wa elimu ambaye anadaiwa kuwa pia ni Sheikhe wa Msikiti wa Mazinde katika kata hiyo ya Vugiri anashikiliwa katika kituo cha mamlaka ya mji mdogo wa Mombo uliopo wilayani Korogwe vijijini mkaoni Tanga.
Imeelezwa amekamatwa jana saa 8.00 mchana ndani ya msikiti wa Mazinde, kutokana na wananchi kutoa taarifa dhidi ya mtu huyo kuendesha vitendo ambavyo vilikuwa vikiwachanganya wananchi kuhusu zoezi hilo la Sensa.
"Mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya kukamilika kwa maandalizi ya shitaka lake", amesema Kamanda wa polisi mkoa wa Tanga,Coastantin Massa


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...