Ankal Habari,
Naomba kuwajulisha Watanzania wote wasifikirie kabisa kufika Umangani (UGIRIKI) Kwa wakati huu kwa kuwa :
Maisha yamebadilika sana kufikia ya kwamba
Wagiriki wenyewe hawana
1.UMEME
2.CHAKULA
3.Wagiriki na Wageni wananyang'anyiana Mapipa ya TAKA TAKA kutafuta chakula.
4.PIA Watu wengi wamejiandikisha kurudi makwao na Serikali haina hela za kuwarudisha
5.PIA Ubaguzi umeinuka kwa hali ya kutisha tokea chama cha Golden down kupata 7%
FIKIRIA (ANGALIZO)
(A).Ikiwa MUAFGHANISTANI na MKURDI ameamua kurudi milimani kwao JE wewe Mtanzania Utaweza kuishi Ugiriki?
(B).MPAKISTANI na MUIRANI wanaolipa hadi dola elfu 10 Kufika ulaya Wameamua kurudi JE wewe Mtanzania?
*Kibaya zaidi sasa hivi vyakula vinagaiwa kwa mfano PASTA Olive mikate bure lakini kwa masharti haya 2 tu
i. UONESHE KITAMBULISHO CHA URAIA WA KIGIRIKI na
ii.UONESHE BLOOD TYPE YAKO KAMA WEWE NI MGIRIKI
Wagiriki wana msemo wao unaosema BEING GREEK IS BY GREEK'S BLOOD sasa kama hata ukiwa na uraia huna damu ya kimanga umeumia
Haya ni ya Ushahidi kabisa na hii hapa ni link ya habari hizo.http://www.ekathimerini.com/4dcgi/_w_articles_wsite3_1_04/08/2012_455401
na picha na pia website za BBC.
Ahsante



Mtalijuwa jiji sasa wenye nchi wamegeuka kuwa ombaomba hapo ndugu zetu watanzania wengi waliobakia ni wale wanaotegemea maisha ya biashara za mitikasi a.k.a vumbi la pele
ReplyDeleteMichuzi, mitundiko kama hii inashusha hadhi ya blog yetu.
ReplyDeleteHe he he Uwwii!Mimi nilikuwa sijui kama kila nchi ina damu yake,,kumbe na sisi waTZ tukipimwa damu inaonyesha kuwa mTz Na Mkenya hivyo hivyo?
ReplyDeleteMimi nafikiri inawezekana ikawepo same damu ya Africa mashariki,,maana dalili niliiona jana tu ,,katika Marathon Masai wa Kenya alivyorudishwa nyuma iliniuma mno,Lakini hata hivyo nilifurahi Mo kushinda.
Kwani Ugiriki hakuna ubalozi wetu?Si Wabongo wajikusanye Ubalozini wasafilishwe kama walivyofanya waliokuwepo south Africa?
Hali ikiwa hivyo bara ndugu zetu mrudi nyumbani,,maana saa nyingine itakuwa hali mbaya zaidi mtu ukashindwa hata kutoka.
Mimi sishawishi watu kurudi home kwa kuwa na mimi niko hapa UK,,,lakini kwa vivyote Insha'Allah najianda wakati wowote kurudi nyumbani,,Ingawa maisha ya hapa sio kama huko Ugiriki
Najuwa mtu kama uko mahali utasema hizo shida au ukame ni wa watu flani wewe haukuhusu..lakaini kumbukeni kwamba hao watu wanadaiwa wana ubaguzi sasa,isije ikatokea kitu kingine kibaya zaidi.
Au hamieni nchi za jirani.
Ahlam ,,London
Makubwaaaa
ReplyDeleteMichu, asante sana kwa hii ya leo yaani ni kali. Nakuomba tunza kabisa hii habari kwenye maktaba yako ili kila baada ya miezi kadhaa unatupositia tena , nimeongea weee na nimetukanwa sana -kwa kuwashauri wabongo wote walioko majuu kurudi kwao waje tujenge nchi yetu kwa amani na utulivu,lakini wengi wao kiburi na kejeri,sasa kiko wapi ??? Hata huko UK bado janga litawafikia tu maana hamna damu ya UK na huko hao mapanki wa ki UK ni wabaya zaidi bora Magiriki mara mia maana wao watasema msemo wao wa ( Malaka mavro) basi wanaishia hapo.Mgiriki kamwe harushi ngumi ni matusi tu na amejaaliwa kweli kwa matusi. Rudini nyie Mavro huko mnangoja nini ?? Kama Mpesa inaweza kuwafikia huko semeni,sisi huku nyumbani tutaanzisha mchango wa kuwatumia pesa.By the way Mavro ni kigiriki na maana yake ni ( mtu mweusi) Zebedayo msema kweli
ReplyDeleteAcha kabisa kutisha watu..
ReplyDeleteUlaya ni JUNGU KUU.. HALIKOSI UKOKO
Usilinganishe kabisa na VUMBI la hapo BONGO..
waliopo Italy nao wajiandae, maana picha tumesha iona.
ReplyDeleteHome Sweet Home. Karibuni nyumbani kwa mikono miwili mtapokelewa kama wana wapotevu kwenye ile story. Msione aibu, wakati wa kurudi nyumbani umefika sasa. Tunawapenda sana!
ReplyDeleteWatu wa 'Ulaya' ndo zenu hizo! Mnatwambia sisi tusije huko mliko,eti maisha mabaya,mbona nyie hamrudi basi?!
ReplyDeleteAcheni roho mbaya iyo. Tutabanana huko huko!!
Poleni sana Ndugu zetu watanzania haya yoote hayapo greek peke yake hata U.S.A yana nukia kwa ukaribu sanaa kutokana na hii economic crisis wengine wanasema ni recision
ReplyDeletempumbavu muongo wewe, sehemu gani watu wanagawa chakula,mtu gani anayelala nje, acha upumbavu na uongo wako, unaongea maneno hayo wakati wala huishi ugiriki
ReplyDeleterudi wewe bongo, usikatishe tamaa wenzako, watu bado wanapiga hela kama kawaida
ReplyDeleteWatu bado tunapeta tu, tena sasa kula totos easy, mpunga wako tu
ReplyDeleteBlood type inaonyeshaje kwamba mtu ni mgiriki? Nimekupata kuhusu kitambulisho cha uraia wa ugiriki, lakini Blood type!!
ReplyDeleteHawa wamanga maisha yakiwa magumu wanachukia watu weusi, si wehu huu.
ReplyDeleteMaisha magumu ugiriki lakini bongo balaa jua kali
Mungu kawalani wagiriki wanapenda sana mchezo wa
ReplyDeleteLSM if you know what I mean.
Hiyo wewe tu. Mbona sie tunapeta? Mtoni kama kuingia Dar kutoka mkoani, wapo wanaoitoa na wanaochapika. Usiwakatishe tamaa wasafiri kwa uzembe wako
ReplyDeleteKuna Wagiriki walikuja Tz siku chache zilizopita kuwekeza ktk secta ya Nishati. Na viongozi wetu wakawapokea. Hatuoni tu kwamba wale walikuwa wakimbizi na si wawekezaji?? Tukoje sisi Wa-Tz? Hatuwezi kutambua pumba na mchele??
ReplyDeleteunaposema umangani ni nchi za kiarabu
ReplyDeletekaka michuzi kabla ya kurusha tasimini habari inafundisha nini jamii...samahani sina maana ya kukukosoa...mi simuelewi huyu jamaa kalenga nini....kuna njaa ndio ...serikari haina pesa ya kurudisha watu...maswali yote kajibu sasa anataka watanzania wafanye nini..watu wameishi sudani miaka ya themanini ndio itakuwa Ugiriki hii mitoto mboga sita inanzai maisha lele mama
ReplyDeleteJamani rudini miloko huko tz imejaa neema tele chemchem za asali na maziwa pamoja na huruma kibao. Hat nyie ndugu zangu wengine mnaobangaiza ughaibuni rudini acheni hizo cheap labor ilihali hela inaingia mfukoni na kutoka hapohapo bila saving yoyote poleni sana. Huku masha ysnaonekana magumu lakni tunaishi vizuri hata baridi haitupigi. Kaka Michuzi yangu ni hayo tu wabongo tupende kwetu sisi si wakimbizi hatuna vita
ReplyDeleteBongo maisha poa siku hizi rudini nyumbani.
ReplyDeleteDuh kweli kwa mwenzio sio kwako, hapo utakuta kuna watu walipata makaratasi ya ugiriki wakajua mchezo umeisha kumbe ndo kwanza unaanza, rudini bongo tu wandugu. Nyumbani ni nyumbani.. Bora kula kitunguu nyumbani kuliko nyama choma vitani #AfandeSele
ReplyDeleteUna maana gani ukisema BLOOD TYPE YAKO KAMA NI YA KIGIRIKI? Kuna blood group (type) ya Kigiriki?
ReplyDeleteJamani ugiriki kumekua umangani?. kama hukujui umangani bora ukae kimya tu
ReplyDeleteASANTE SANA MDAU. NINGEPENDA TUPATE NA UPDATE YA SPAIN.
ReplyDeleteHaya sasa Katibu wa Umoja wa Watanzania Uguruki upo hapo?
ReplyDeleteWewe si ndio ulikuwa unaandika humu kupinga hali halisi huko?
RUDINI NYUMBANI WANDUGU TANZANIA SASA MAMBO POA!
Naomba hii comment iwepo kwa waliopinga mambo ya blood type na wapi watu wanagaiwa vyakula Ugiriki
ReplyDeleteXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
By Nikos Xydakis
The distribution this week by Greece’s far-right Golden Dawn party of free food on SYNTAGMA Square was a turning point in society’s moral and spiritual decline.
The offer was limited to card-carrying Greek citizens and only after they had submitted important personal information including their BLOOD type.
Even by the contemporary standards of this crisis-hit country, a Greek person can only feel shame in seeing volunteers from a neo-fascist party, all of them dressed in black t-shirts, distribute packs of pasta and other foodstuff after inspecting, as it were, the BLOOD of the needy.
HAYA KWA MSILOLIFAHAMU HILO BASI HIYO NDIO NEWS GAZETI LA EKATHIMERINI TAR 3.AUG.2012 Nadhani nimejibu uzuri-kuhusu kula kwenye taka taka nitakutumieni picha tu karibuni nitazinasa huku huku mikoani si athina tu.
UMANGANI NI UGIRIKI NA WAARABU NI WASHIHIRI kwa alieuliza
WIMBO:
ReplyDelete1.Tangu zama za kale asili yetu ni wakulimaaa hatuna budi tuendeleze kilmoooo X3
2.Tutumie mbolea za kisasa mashambani kundeleza kilimoooo X2
3.Niwajibu wetu tuendeleze kilimo cha kisasa kwa mazao boraaaa X3
----------------------------------
Wandugu Ugiriki, bundi ameshaunguruma muda mrefu wimbo wa kuwakaribisha nyumbani Tanzania kwa shughuli za kilimo ndio huo hapo juu.
KARIBUNI SANA NYUMBANI MJE MSHIRIKI KILIMO!
Madiaspora kutoka Ugiriki,
ReplyDeleteHaya moja kwa moja hadi Mabwe Pande Kambini na Kaliuwa-Tabora kukata mkaa!
Nafikiri Watu Wanashindwa kutofautisha Wazamiaji, wasio na elimu na wavuta bangi waliokuepo Ulaya, na wasomi waliosoma Ulaya na wanafanya kazi ulaya wanaokula bata mpaka kuku anaona wivu. Mimi ni IT technician nimesoma hapa nafanya kazi hapa nalipwa vizuri kuliko mbunge wa bongo, sasa na mimi nirudi kwenye foleni na vumbi la bongo?? acheni kasumba nyie, njooni mpate exposure sio kuneng'eneka tu. Fitina zimewajaa watanzania.
ReplyDeleteAssalam Alaykum!
ReplyDeleteKayu Ligopora Katibu wa Umoja wa Watanzania Ugiriki.
Nilikuwa napita tu huku nikisema RAMADHANI KAREEEM!
Ukweli unauma sana, ni vizuri kujua kujifunza kwani Ulaya sio kama wengi wanavyofikilia, kuna wamasikini na kunamatajili kama nyumbani tu. Ugiriki kwa sasaivi hali yake sio nnzuri kwa wao na zaidi kwa watu wakuja, hii sio siri Dunia yote inajua, sasa kama kunawatu inawauma kutoa hii siri wenyewe wanafikili ni siri lakini mjue kuwa tunaishi 2012 tunapata habri kwa njia mbalimbali na hakuna siri tena kama apo zamani watu waishio Ulaya walivyokuwa wananganya watu uku nyumbani. Kwenye shida lazima kutafutwe sababu na nnchi za Ulaya mala nyinig sababu yao kubwa ni watu wakuja ndio wanaohalibu nnchi ndio wanaochukua mali zetu. Watanzania ni watu wakalimu sana lakini hata sisi wenyewe uwa tunawalaumu waindi kwa kutuchukulia mali zetu wakati sisi wenyewe tumelala, sasaivi kuna wachina wazungu wa afrika kusini .nk. Lawama ziko na lazima ziwepo kwani ndio changamoto la maisha. Kwa serikali yetu inabisi isikie hiki kilio cha watanzania wenzetu wanaoshidwa kuludi nyumbani kwa sababu za kukosa anauli, hali hii ipo na wala sio ya uwongo. Kama wewe unaweza kujisitili na kujitafutia ridhiki yako Mungu akuzidishie, lakini kwa wanao hitaji msaada inabidi wasaidiwe kwani kila mtu anandoto za mafanikio lakini sio kila mala inakuwa vile tunavyooota. Asante.
ReplyDeleteBongo mambo mazuri...hata mchezaji mpira kama Mrisho Ngassa analipwa donge nono na simba SC la Tshs. 2,000,000 kwa mwezi....(by the way hapa kiwanja unatengeneza dola 500 kwa week au $2000 kwa mwezi kwa kufunga burger tu @McDonald)....mliokosa visa msitukasirikie sisi...bongo mambo mazuri? simama pale njia panda ya buguruni au tazara alafu niambie watu onaowaona wanakwenda wapi na wanatoka wapi....
ReplyDeleteNJAA HAINA UBAUNSA!
ReplyDeleteHayo ni maneno yaliyoandikwa chini ya chota matope la basi la Daladala aina ya Toyota DCM linabeba abiria kati ya Mbagala Rangi 3 na Mwenge hapa Dar Es Salaam.
Ni maneno matatu (3) lakini yana maana kubwa sana.
Jamani ,Jamani,Jamani wandungu zetu Ugiriki acheni ubishi msikatae hali halisi ya njaa, kwani njaa haina siri!
TAFADHALINI SANA KUWENI JASIRI MRUDI NYUMBANI, TUNAELEWA WENGINE MLIONDOKA KWA MISALA MAKWENU KAMA KUWAZIKA NDUGU NA JAMAA FEDHA NA MALI NA WIZI, WENGINE MLIUZA MALI ZA FAMILIA MKASAFIRI,,,MRUDI AU KABLA TUMENI TAARIFA KWA MJOMBA MICHUZI ILI WATU WENYE BUSARA (Kwa bahati humu jamvini tunazo hazina ZA BUSARA kama Yeye ANKALI MWENYEWE, Mdau DAVID. V .Mdau ZEBEDAYO MSEMA UKWELI, Mdau Bibie AHLAM WA UK na wengineo) WAJIPANGE KUWAOMBEA MSAMAHA MAKWENU MKIWA MAJUU KABLA HAMJARUDI.
MSIJE MKAKAA UGIRIKI ZAIDI MKAKUTA NCHI IMEINGIA KABURINI KABISA NA IMESHAUZWA KWA MKOPO KWA MABILIONEA WA URUSI!