Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik muda mfupi baada ya kuwasili akitokea nchini Ghana ambapo alishiriki mazishi ya aliyekuwa Rais wan chi hiyo Marehemu John Atta Mills.Kushoto ni Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama Jenerali Davis Mwamnyange.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisoma barua aliyoandikiwa na mtoto Khaitham Jumbe(kulia) wakati wa futari aliyowaandalia watoto walemavu na yatima ikulu jijini Dar es Salaam.Katikati anayeangalia ni mtoto Hamida Jacks mdogo wake Khaitham.Mtoto Khaitham Jumbe ni mlemavu wa ngozi na alikuja ikulu na wazazi wake.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisoma barua aliyoandikiwa na mtoto Khaitham Jumbe(kulia) wakati wa futari aliyowaandalia watoto walemavu na yatima ikulu jijini Dar es Salaam.Katikati anayeangalia ni mtoto Hamida Jacks mdogo wake Khaitham.Mtoto Khaitham Jumbe ni mlemavu wa ngozi na alikuja ikulu na wazazi wake.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakigawa zawadi kwa watoto yatima na walemavu walohudhuria futari waliyowaandalia ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni.
Baadhi ya watoto yatima na walemavu wakishiriki katika futari ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni(picha na Freddy Maro).
Khaaa, mbona hajaleta mananasi aliyokuwa anayashangaa kule Ghana?
ReplyDeleteIsiishie futari tu mapesa ya rada yawaendeleze kielimu kwa vile ulimu ni ufunguo wa maisha
ReplyDeleteHapa ndipo panaponifanya nimpende huyu Raisi wetu(SIONGELEI MAMBO YA VYAMA NAONGELEA MY PERSONAL ADMIRATION TOWARDS HIM)Mimi nampenda sana mtu yeyote anayeonesha hisia za huruma kwa wale wasiokuwa na uwezo.Mambo yenu mengine ya kisiasa nawaachieni wenyewe mimi huko simo na wala siyawezi hayo.
ReplyDeleteMimi sio shabiki wa CCM wala Kikwete, lakini hii ni safi. Ni muhimu sana kuwakumbuka ndugu zetu, hasa watoto. Ahsante!!
ReplyDeleteALHAMDULLILAH BWA MKUBWA MWENYEZI MUNGU AKUPE ZAIDI HIO NDIO FUTURU SIO WENGINE MISIFA TU HAWAJUI NINI UTAONA MIJITU INAUWEZO YOTE INA ALIKWA ATI MTU ANAFUTURISHA KAMA SIO MISIFA NINI SASA KUFUTURISHA MAYATI JAMA NA WASIO JIWEZE THX JK
ReplyDeleteHII IMETULIA TUWAKUMBUKE KILA SIKU SIO SIKU MOJA MOJA
ReplyDeleteHawa ndio wenyewe kufuturishwa
ReplyDelete