Brother michuzi:

Nashukuru sana kwa msaada wako ulionipa mpaka sasa hivi. Ningependa kukufahamisha kuwa nimeingia kwenye top 10 ya multimedia award na hii inatokana na mchango wako wa blog yako ya jamii na wadau wako wote.

Ahsante sana na naomba uwaambie Watanzania waniombee dua  kwenye Miss World finals Leo jioni.

Asante

Lisa Jensen

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa


  1. Congrats for Top 10 and Good luck!

    ReplyDelete
  2. Tupo pamoja mrembo wetu tutoe kimasomaso..na cc tujivune jamani....ila tafadhari mrembo usiwe kama wenzako waliopita wote wamepapatikia mijishetani mijizungu ya ajabu yani wameludi utumwani...nakuomba usitupe utu wako na asiri yako...coz wengi tushasusa nakujisumbua na ujinga wanaofanya hao wanao jifanya eti warembo...mfano huyu wa kuitwa Nancy sumari...bila ya aibu kabisa kasema eti mrembo lazima awe na jizungu..kwenye kwenye kipindi cha yule mjinga..mkasi...tena cha kushangaza huyu Nancy yuko kwenye ile kampeni ya kuwajengea wanafunzi wa kike mabweni...tena hawa hawa wanao jifanya warembo wanafanya mchezo mchafu wa kuwatongozea hiyo mishetani wanafunzi wa kike wa secondari...tafadhalini sana msituhalibie wanafunzi wetu...naomba wahusika wamtoe huyu nancy sumari..kwenye kampeni ya kujenga mabweni ya wanafunzi wa kike...asanteni sana wadau amani kwenu...ni mm tajiri wa mawazo endelevu sikusoma ila naona mbali.

    ReplyDelete
  3. Hongera mpaka hapo ulipofika lakini sahau suala la kuombeana dua. Hizo ni kasumba za kijinga ambazo sie watanzania tunajipa. Kushinda ni jitihada zako na inatokana na uwezo wako wa kujibu maswali ila si dua. Kumbuka kila mtu ana mungu wake. Jiamini utashinda.

    ReplyDelete
  4. Hongera sana mtoto wetu Mungu atakutangulia utafanikiwa

    ReplyDelete
  5. NAKUOMBEA DUA MDOGO WETU
    NAJUA UTASHINDA TUPO NAWE
    KWANI NIOMEONA VIGEZO VYOTE UNAVYO;
    MUNGU AKUBARIKI :NA IBARIKI TANZANIA

    ReplyDelete
  6. Jamani kuna mtu hapo juu kazumgumzia swala na Nancy , Je swali lina husu nini hapa ??? hayo ni maisha ya Nancy
    alituwalikilisha vizuri sasa kama kachagua mzungu ni maisha yake.Tuache wivu au Mchangiaji ni mbunge anamwonea wivu Mbunge mwenzie alioa miss Tanzania????
    Tuache ushamba mapenzi ni ya mtu binafsi;

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mshamba huyo achana nae! Kwanza huoni hata kuandika anachanganya maneno!
      Na amesema mwenyewe kuwa hajasoma ila eti anaona mbali! Hahaah mwenyewe anaona katoa pointi kumbe anajidhalilisha tu.
      Kweli ubao mweusi dili kuuona tu achilia mbali kuutumia.

      Delete
  7. Mimi mbona sijamuona kwenye hii video? Katika kumi bora yeye alichukua nafasi ya ngapi?

    ReplyDelete
  8. Asante kwa feedback.Tutakuangalia live bila chenga.

    ReplyDelete
  9. mpaka hapo watu wanaona juu juu tu unavyoteseka kujituma kwaajili ya nchi yetu hua hawa vioni ukishinda ndio wanasifiaukishindwa wanazomea bila kujali jitihada zako ulizozitoa ambazo hazionekani.kwa ufupi tu jitahidi kupigania nchi yako.utapokelewa kama mfalme.

    ReplyDelete
  10. Naam, Daaah kuna watu wanakatisha tamaa kweli kweli huyo mtoa mada wa kwanza kama alivyojitamburisha mwenye kuwa hakusoma na wala haoni mbali. Yani jamaa libaguzi halina AKILI hata moja mimi nimeangalia mkasi na NANCY wala sijaona sehemu aliposema kuwa miss lazima aolewe na mzungu. Kwanza kwa nini unawaita MIJUZUNGU MISHETANI hivi wewe ungekuwa mzungu na ukaitwa hivyo ungejisikiaje, baba yako angekuwa mzungu angejisikiaje, mama yako, kaka yako, demu wako au mkeo na ndugu zako wote muhimu wangepewa kauli hiyo ungejisikiaje? ACHA USHAMBA WEWE...............!!!!!! Afu kwa nini unimuita SALAMA mpumbavu kakukosea nini mbona yeye hakufuatilii? Ebana eee afu huyu jamaa hajatulia kweli kweli una ushahidi gani kuwa NANCY anawakuwadia wasichana kwa wazungu tutajie mmoja tu kama mfano wa hilo.

    Mzee wa libeneke maoni ya wapuuzi kama hawa usiyaweke bwanaa yanachafua hali ya hewa ile mbaya kwa sisi wadua wa juu.

    Mdau UK.

    ReplyDelete
  11. Tajiri wa mawazo endelevu wa taifa letu...hewani tena...nimeludi kwa hasira...ww mdau wa uk mm sio mbaguzi ninachokisema hukijui kabisa ww piga box lako huko uliko na kiuno chako nahisi tayari kishavunjika....mm nitakemea uooooozo wa aina yoyote tazama vizuri hiko kipindi chako cha kipumbavu cha mkasi...kuanzia watangazaji mpaka baadhi ya wageni zake..mgeni wake anaweza kua mstaarabu lakini yeye bado anamuuliza maswali ya kipumbavu kabisa...mpaka unaona kichefu chefu...Nancy kaulizwa kwanini walimbwende wote wanaoshiliki miss tz wanazaa na mijizungu...sasa ww mwehu wa uk...msikilize Nancy majibu yake...na kwa taarifa yako najiandaa kuandika waraka maarumu juu ya uchafu wao wanaouufanya kuhusu wanafunzi wetu.. ni yule yule tajiri wa mawazo endelevu wa taifa letu..amani kwenu wadau.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mshamba wewe acha kuongeaongea ovyo humu kwenye public! Ukoje?
      Nimekudharau hadi mwisho!
      Bila wazungu ungekuwa hapa leo hii?
      Hebu jitambue kwanza.

      Delete
  12. Eti bila ya mijizungu ningekua wapi?...ningekua hapa hapa bongo kwa bi mkubwa wangu na taifa langu..ww mdau wa uk nishakwambia vunja mgongo na kiuno chako kwa kubeba mabox na ukiludi tutakuuguza maumivu yako...kwahiyo ukiona nakemea mambo ya umuhimu kwenye hii nchi yetu ww tulia kabisa na ww ndio kabisa umeenda utumwani eti unasema bila ya woga eti mdau uk..hu si usawa wa kutisha na uk yako...watu wa huku bongo siku hizi wajanja kuliko ww huko..bwanamdogo karaga baho...waraka nitauandika tu..sitaki kabisa kuona wanafunzi wetu wa kike wa secondary kwenye hii nchi yetu wakifanyiwa mambo ya kukatisha masomo yao..full stop..ni mm tajiri wa mawazo endelevu ya nchi yetu..amani kwenu wadau.

    ReplyDelete
  13. Naam, sawa tajiri wa mawazo endelevu na nchi yako.

    UKIBISHANA NA CHIZI WATU WA PEMBENI HAWATAWEZA KUTOFAUTISHA CHIZI NI YUPI. so nakuacha mdau lkn usikose kuwaomba msamaha hao madada wawili NANCY na SALAMA vinginevyo una deni nao.

    mdau UK.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...