TASJA ni chama cha waandishi wa habari za Sayansi Tanzania. Kikiwa na lengo la kuhamasisha na kutoa na kuelimisha umma juu ya habari za kisayansi na kitafiti zenye masilahi kwa maendeleo taifa na maisha ya Watanzania.

Tasja imepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za kifo cha Mwandishi wa habari wa siku nyingi ALFRED MBOGORA ambaye alikuwa mdau muhimu katika kufanikisha uanzishwaji chama cha TASJA.

Chama cha waandishi wa habari za Sayansi TASJA tukiwa washirika wa karibu wa Baraza la Habari Tanzania ambapo Marehemu alikuwa akifanya kazi, tunachukua fursa hii kuwapa pole familia ya marehemu, wafanyakazi wenzake na wanahabari wote kwa kuondokewa na mdau muhimu aliyekuwa akipigania kuona fani ya habari inakuwa nchini na kuhamasisha wanahabari kuandika habari zenye kuzingatiwa ukweli na weledi.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.

Imetolewa na

DAVID RAMADHAN
Katibu Mtendaji TASJA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...