Na Mahmoud Ahmad, Arusha
Serikali ipo mbioni kubadili mikataba ya madini kati ya wazawa na wawekezaji na kuifanya kuwa nusu kwa nusu yaani asilimia 50%kwa50% ili kuchangia pato la taifa na kuifanya rasilimali ya madini kusaidia kukuza uchumi .
Kauli hiyo imetolewa na katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini Bw. Eliakim Maswi (pichani) wakati akizungumza katika mkutano na wafanyabiashara wadogo wa vito jijini Arusha
Maswi alitanabaisha kuwa kwa kuanzia na mkataba wa kampuni ya Tanzanite one ya wilayani Simanjiro mkoani Manyara ambao upo mwishoni mwa mkataba wake.
“Kampuni ya TANZANITE ONE mkataba wake umefika kikomo hivyo wakishailipa serekali mrahaba na kama watahitaji kuendelea basi mkataba wetu ni nusu kwa nusu”alisema Maswi.
Aliongeza katibu mkuu huyo kuwa kuanzia sasa watajitahidi ili sekta hiyo ichangie pato la taifa kama nchi nyingine zenye rasilimali hiyo zinavyo nufaika na sekta ya madini.
Nae Mwenyekiti wa wafanyabiashara wadogo wadogo wa madini hapa nchini Sammy Mollel alisema kuwa wanataka kuifanya Tanzania kuwa kituo cha uuzaji,ukataji na ununuzi wa madini na vito katika bara la Afrika na kuitaka serekali kuwapa ushirikiano kwenye hilo
.
Mollel alisema kuwa wao watatoa ushirikiano kwa serekali kuweza kuwadhibiti wale wote wanaokwepa kuilipa serekali mapato na kuwafichua wafanyabiashara wakubwa wanaokwenda moja kwa moja migodini.



ReplyDeleteHivi ni kweli mikataba iliyopita tulikuwa tunapata asilimia nne (4%) tu?
Botswana wameweza kuwashawishi kampuni ya De Beers ya Afrika Kusini kuhamishia shughuli zake za ukataji vito nchini humo, na sasa wananchi wa Botswana kwa sasa wana uhakika wa ajira na maisha bora.
ReplyDeleteBaadhi ya shughuli hizi pia zitajumuisha ukataji, utengenezaji, na uuzaji na Botswana inatajiwa kupata mapato ya zaidi ya dola za Marekani bilioni 6!
Kwahio mtaalam Maswi chapa kazi mkuu, pitia mafaili yote na safisha secta hiyo tajiri Tanzania.
Mdau Richard.
Tatizo siyo madini,ni viongozi wetu.TANZANIA NI TAJIRI IKIPATA VIONGOZI TAJIRI WA MAWAZO.
ReplyDelete