Habari Bwana Michuzi, mkuu wa libeneke,
Fikisha salamu hizi, kwa Ngahu na timu yake,
Mwambie ni upuuzi, kuwabeza ndugu zake!
Afrika Mashariki, sisi sote tuwamoja.

Kaiponda Tanzania, huyu Bonifasi Ngahu,
Kaandika kihisia, ni wazi hajakubuhu,
Mambo hasi kakazia, mema yote kasahau,
Afrika Mashariki, sisi sote tuwamoja.

Wazi ainyemelea, Bongo yetu kifurusa,
Njia anayotumia, ni kubeza kibubusa,
Tafiti hajatumia, japo zipo kwa rumbesa,
Afrika Mashariki, sisi sote tuwamoja.

Kodi kama ziko ghali, nenda kwenye afadhali,
Nchi ‘bomba’ kweli kweli, utozwe shilingi mbili?!
Ngahu acha ufedhuli, andika vyenye akili,
Afrika Mashariki, sisi sote tuwamoja.

Wasifu kwa Museveni, na udugu wau-unga,
Kisa vitu vya melini, kwenu vinatia nanga,
Tunakaza kampeni, vyote vitapita Tanga!,
Afrika Mashariki, sisi sote tuwamoja.

Na wahanga wa ajali, eti nayo kwako dili,
Uovu waunakili, ‘-tadhani si Mswahili,
Ule japo ujangili, si sera zetu kwa kweli,
Afrika Mashariki, sisi sote tuwamoja.

Eti twachoma misitu, wanyama wasende Kenya,
Ukweli si hivyo katu, Ngahu acha kudanganya,
Bora uliza ‘Misitu’, kuliko kutusengenya!
Afrika Mashariki, sisi sote tuwamoja.

Ndugu Ngahu nakuasa, upunguze vyako visa,
Umoja ni kwa hamasa, na si kuleta siasa,
Kama kwetu ngumu pesa, nenda kavue Mombasa,
Afrika Mashariki, sisi sote tuwamoja.

Mwamgongo (Bw)
Mwenyeji wa Tanga,
24 Agosti 2012 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Ahsante Muungwana wa Tanga Mwamgongo wa mistari bunduki kabisa ya kumshindilia Baazazi Ngahu na wenzake Mau mau.

    Ningemuona Ngahu na wenzake kuwa mzalendo halisi wa Kenya nchi yake kama angetuma madai au kuandika malalamiko dhidi ya Uingereza na Uholanzi.

    La zaidi Wakenya hao wasitulaumu Watanzania na nchi yetu ikiwa na mali zake na fursa zake lukuki, wao waende wakafuatilie na kuandika malalamiko yao kwenye ile kesi ya Mau mau huko London wanaowashitaki dhidi ya Waingereza.

    Au kwa nini akina Ngahu wasilalamike dhidi ya Uholanzi huko The Hague kwenye kesi ya akina Uhuru Kenyatta?

    ReplyDelete
  2. Wakenya walijenga mtazamo ya kuwa kuingia ktk Umoja na sisi kwa mara ya pili tena watapata kwa ubwete kama walivyotuingiza mkenge kwenye Jumuia ya zamani ya Afrika Mashariki iliyokufa mwaka 1977.

    Kenya inajenga imani ya kuwa watatatua matatizo na njaa zao za kimaisha (kwa wao kunufaika pekee)kupitia mgongo wetu Tanzania badala ya kujenga umoja wenye manufaa kwa pande zote.

    Hawa wanafikiri Tanzania ilivyokuwa mwaka 1977 na Watanzania na ndio ilivyo sasa?

    ReplyDelete
  3. Kenya wanaichukulia Tanzania na mali zake, fursa zake na rasilimali zake kama SHAMBA LA BIBI!!!

    Hivi ninyi mabwege Wakenya mnafikiri FURSA za Tanzania ni mali ya msituni haina mwenyewe?

    ReplyDelete
  4. KENYA:

    ONYO KWENU,

    Kwa sasa hivi safu ya Utawala wetu ni ya Maafisa wa Majeshi, hivyo mkija Ofisi za Utawala Tanzania ya sasa msitegemee kukuta Wanasiasa na suti za kaunda zisizo na ukosi na Mashati ya vitenge kama enzi zile za Baba Nyerere.

    Sasa hivi Ofisi zetu za Utawala mtakuta mezani kwa mabosi Nyaraka za mikataba,kalamu, wino wa kutilia sahihi kwa dole gumba na Bastola !!!

    Sasa bandugu mnafikiri (Tanzania) kushirikiana na mshirika Jambazi(Kenya) utajihami vipi?

    ReplyDelete
  5. Mdau asante kwa shairi lako zuri. Huu ndo uzalendo tunaoutaka, kuetea kilicho chako kisidhalilishwe na mtu wa nje.

    Pia nimefurahishwa na mdau aliyesema ni unafiki kwa tanzania kushirikiana na jambazi (Kenya)- BIG UP mdau kwa kuliona hili.

    ReplyDelete
  6. Ukiona Wakenya wanalalamika ujue wameshindwa kupata vya dezo kutoka Tz. Tanzania endelea kushikilia mkazo vinginevyo hao jamaa ni manyang'au watabeba kila kitu kupeleka kwao.

    ReplyDelete
  7. Sawa sawa Mdau wa Fri Aug 24, 07:46:00 PM 2012

    Kenya tutaingia mikataba nao kwa Umoja na tutawasainisha mikataba safari hii chini ya Mtutu wa bastola!

    Hawa ni watu wa ajabu sana, angalieni wao wanadai kuzingatia Ibara muhimu ktk Umoja wa Afrika ya Mashariki vitu kama:

    1-Rule of Law
    2-Social Justice
    3-Investment sharing
    4-Political Federation
    5-Monetary Federation
    6-Customs Union/Federation

    Lakini hapo hapo wanawasifu na kuwapa Credibility Wasomali wanaoteka meli na kudai Mamilioni ya $ Dola za ngawira wanazotumia kuwekeza kwa ujenzi wa magorofa Nairobi na Mombasa.

    Serikali ya KENYA nimewahi kuona inasifia uwekezaji wa namna hii unaotokana na Fedha za Kijambazi na Uhalifu wa Wasomali!!!

    Je, kwa msimamo huu Kenya inazingatia No.1 na No.2 yaani Rule of Law na Social Justice?

    Ina maana hata tukiwa na Umaoja na kushirikiana nao ktk EAC sisi(Tanzania) tufuate No.1 na No.2 lakini wao (Kenya) ibara hizo wakiuke?

    ReplyDelete
  8. Assalama Lekko zao Maafisa Wakuu na Waandamizi wa Umahiaji na Wizara ya Mambo ya Ndani kwa KUENDELEA NA MASHARITI YA VIBALI TANZANIA, na kuongeza ADA YA VIBALI VYA WAGENI NCHINI.

    Kama anavyosema Mdau wa 7 hapo juu jamaa (Kenya) wanataka sisi (Tanzania) tufuate kanuni kama hizo 6 hapo ikiwemo No.1 Rule of Law na No.2 Social Justice halafu wao wakiuke.

    Mfao ktk Ibara zingine za EAC kama

    7-Free Movement of Labor within EAC
    8-Free Movement of Capital, goods and services within EAC,

    Ina maana wao walete watu wao kufanya kazi huku Tanzania lakini sisi tukifika kwao Kenya watubanie na kuwa hizo kanuni zitubane sisi ili wao wapate nafasi na fursa zaidi ktk Umoja wa EAC.

    Kama John Mashaka anavyoeleza, wao wanatoa Kibali kwa mfanyakazi ambaye ni mgeni kutoka nchi za EAC mwenye umri wa zaidi ya miaka 35 na mwenye kipato cha zaidi ya US$ 24,000 kwa mwaka, kitu ambacho Watanzania wafanyakazi wengi hawana sifa (wao wenyewe Kenya hawana uwezo wa kumlipa Mtanzania akifanya kazi kwao hela hiyo kwa mwaka) na kuwa hiyo ni janja ya kupunguza fursa za kazi kwa Watanzania huko Kenya lakini wao wanataka wapate kazi huku waingie bure na bila mashariti.

    Hiyo ndiyo akili yao ilipo, na ndio maana wanataka kuharakisha na kutuingiza mkenge lakini Viongozi mwetu wamekuwa makini na wamewakazia uzi kwa kuwaambia WE ARE NOT IN THE LEVEL OF EAC INTEGRATION THAT WE CAN ALLOW FREE INCOMING LABOR AND WAIVE FOREIGN WORK PERMITS!!!

    ReplyDelete
  9. Kenya wanafikiri sisi tunategeka kirahisi sio?

    Achana na Mtanzania kabisa, unakuta mtu hana elimu kubwa lakini anaona mbali sana.

    ReplyDelete
  10. Kenya:

    Mjiheshimu na muheshumu wengine ktk hii EAC.

    Zaidi ya hapo tumeshaingia ktk ndoa ya mkeka ya huu muungano na ninyi, lakini mkumbuke kila Mtanzania kwa walio wengi wamepitia kama sio Mafunzo ya Mgambo watakuwa wamepitia JKT hivyo msitegemee kuwa Mtanzania ni lege lege.

    Itakula kwenu!

    ReplyDelete
  11. Kenya, muwe kwanza ninyi mnafuata Kanuni kama mkitaka wenzenu wafuate kanuni.

    Sio mnakuawa mabingwa wa malalamiko na madai.

    Pia Tanzania kwa kuwa ni hot-cake ktk EAC ni lazima tuweke mashariti ya Vibali vya kazi kwenu na kwa wageni wote, na pia kuongeza Ada ya Vibali ili hata ninyi mje kwa vigezo na ushindani kufanya kazi na kuendesha shughuli zenu TZ.

    Hakuna bwege mtampata wa kumshinikiza afuate kanuni halafu ninyi msifuate!

    Hii hata jirani yenu Somalia asiye na Serikali imara hawezi kukubali.

    Hii hata Malawi kweli watakubali?

    ReplyDelete
  12. Hi,

    Allow me to comment; I was born to a Kenyan father and a beautiful Tanzanian mother. I have lived in both countries,have strong blood relations in both, friends who I wouldn't part with equally - the list is endless.Tanzanians are beautiful people - mind and heart - but they have been poisoned to believe that Kenyans are materialistic, arrogant and selfish individuals. On the other hand, Kenyans - who happen to be aggressive in nature - believe that they are faster and better than Tanzanians because of their mastery of the Queens English, exposure and work ethic. Both are wrong, but both again are also right - The fact is, Tanzanians walk freely and work in Kenyan companies without fear of Immigration officials coming to knock at their doors every week. Is it reciprocated in TZ? Another fact is, Kenyan's seek wealth to the detriment of anything - including social enrichment and well-being, and justice - a purely capitalistic attitude - do Tanzanians do that in Kenya?
    Am lucky - I have both. I do not hesitate to rush to TZ and have my fill of 'trupa' and 'mbege' with genuine people,laughing through the night because I feel at home .On the other hand, it will take me 48hrs by email to get a $ 25,000 personal loan approved in Nairobi - because i mean business...
    Kenyans, Tanzanians, we are separated by an imaginary border crafted by a white man whose sole intention was to separate us...and its working. Reflect on that....
    In conclusion, Kenyan's, manage your greed and as for Tanzanians, manage your fears....We will have an East Africa which can shame the south...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...