Jumuiya ya Watanzania wa Wichita, Kansas, nchini Marekani (TAWICHITA), inasikitika kutangaza kifo cha mtanzania ndugu Martin Phiri kilichotokea Julai 22, Wichita, Kansas.
Baba mzazi wa marehemu Philemon Phiri ameshawasili Wichita, Kansas na mipango ya maziko inaendelea. Taarifa kutoka kwa mke wa marehemu zinasema, marehemu alikutwa na mauti usingizini.
Marehemu ameacha mke na mtoto mmoja. TAWICHITA inawaomba Watanzania wote wanaoishi nchini Marekani na duniani kote kuweza kutoa msaada wao ili kufanikisha mpendwa wetu akapumzishwe katika nyumba yake ya milele.
TAWICHITA imefanya harambee kwa siku za Jumanne na Jumatano, na vilevile harambee hiyo itaendelea tena siku za Ijumaa na Jumamosi. Kwa walio nje ya Wichita, Kansas, wanaweza kuchangia kupitia mfuko maalum unaoitwa "Martin Phiri Fund," kupitia Bank of America.
Tunatanguliza shukrani zetu za dhati katika kufanikisha kupumzishwa kwa mpendwa wetu Martin Phiri. Bwana ametoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.
Amina!



Wafiwa pole saana, kazi ya Mungu haina makosa.
ReplyDeleteMungu awape nguvu katika kipindi hichi kigumu sana.
Kwa yule aliyeweka habari hii amesahau kuweka account number. Bank of America sometimes ukienda na jina tu bila acct wanakataa. Kupunguza usumbufu ungeweka acct #..
Jamaa kama namjua aliwahi kukaa uk?
ReplyDeletePoleni sana kwa kufiwa NA Mungu aiweke mahala pema
ReplyDeletePeponi roho yake.
Hiki ndicho kitu ambacho nimeanza kukiogopa sana hapa duniani. Kumbe tupo kama hatupo, Ndugu zangu,turekebisheni mienendo yetu,tujiwekeni tayari kuingia kwenye uzima wa mbinguni,tusipende sana ya dunia bali tufuateni yaliyoandikwa kwenye maandiko matakatifu.Haya tunayoyafukuza ni yakupita. Mungu akuweke pema peponi ndugu yete Martin Phiri,na tuliobaki nyuma yako, tujiulize kama tuko tayari au tumejaa makosa kibao.
ReplyDeleteNdugu poleni kwa msiba
ReplyDeletePole ni sana watanzania wenzangu hasa hasa nyie mliopo marekania hasa hapo Wichita nakumbuka huyu bwana alitokea chuo kilichoitwa Waldorf College cha dar es salaam
ReplyDeleteJamani Poleni sana kwa msiba lakini kwa nini msimrudishe kuzikiwa nyumbani Tanzania?? itakua vizuri sanaa kwake pia, alipapenda sana Tanzania hakuacha kusema kwamba lazima arudi mwishoni mwa mwaka huu.. RIP brother
ReplyDeletePoleni sana ... bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe.... astarehe kwa amani ...Amen
ReplyDeleteAti tujiweke tayari kuingia uzima wa mbinguni... ni kitu gani kinakufanya ufikirie kuwa kuna maisha zaidi ya haya hapa duniani? tuache kujipa matumaini yasio na ukweli wowote wa kuaminika. Tuishi vizuri hapa duniani na kufanya maisha yetu yawe bora hapa ambapo maisha yake tunayajua, ya mbinguni hayana uhakika na hatuyajui.
ReplyDeletewewe unayekanusha kwamba hakuna maisha ya milele huko mbinguni, basi unalako jambo. Je ?? ina maana hakuna Mungu ?? maajabu yooote haya unayoyaona hapa duniani ,je ? nani kayaumba ? huo mwili wako mwenyewe ulivyo delicate na viungo vyake vyote na jinsi vinavyofanya kazi ndani ya mwili !!!! laiti ungelifikiri angalau sekunde 2 tu, basi ungeliinama na kumtaka radhi Muumba wetu. Uhakika ni kwamba ,hujui kama utaamuka hai kesho. wasalam.
ReplyDeleteSijakanusha kuhusu maisha ya milele ila nimesema hatujui nini kinatokea baada ya kufa na gamma sababu ya msingi ya binadamu kufikiria kuna maisha ya milele. Ati unasema maajabu ya dunia, yaani kweli unafikiri njia pekee ya sisi kuwepo hapa duniani no kuwa na muumba "aliyeamuru" vitu vitokee? Seriously? Nakushauri usome zaidi ya vitabu vya dini update uelewa was mambo mpana zaidi. Hayo "maajabu" mengi tu yanaelezeka kisayansi.
ReplyDeleteSijakanusha kuhusu maisha ya milele ila nimesema hatujui nini kinatokea baada ya kufa na hamna sababu ya msingi ya binadamu kufikiria kuna maisha ya milele. Ati unasema maajabu ya dunia, yaani kweli unafikiri njia pekee ya sisi kuwepo hapa duniani no kuwa na muumba "aliyeamuru" vitu vitokee? Seriously? Nakushauri usome zaidi ya vitabu vya dini update uelewa wa mambo kwa upana zaidi. Hayo "maajabu" mengi tu yanaelezeka kisayansi.
ReplyDelete