Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini ukishirikiana na Jumuiya ya Watanzania waishio Gauteng (Talga) unapenda kuwatangazia Watanzania wanaoishi katika Jimbo la Gauteng (Pretoria na Johannesburg) kuwa kutakuwa na mkutano wa Watanzania wanaoishi katika jimbo hilo utakaofanyika tarehe 25 Agosti, 2012 katika ukumbi wa Lions Club, No. 9 Umagazi Rd, (off 26th street) MENLOPARK Pretoria kuanzia saa nane mchana,kufika kwako mapema ndiyo mafanikio ya mkutano huu.

Mkutano huo una lengo la kupitisha maoni ya katiba , kuchagua viongozi wa kudumu wa jumuiya ambapo zoezi hili litahusisha wanachama hai pekee, inamaana wale walioweza kulipa kiingilio katika Jumuiya R200 na Ada ya mwaka R300,pia kujadili mambo mbali mbali yanayohusu watanzania wanaoishi katika jimbo hili. Aidha Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini Mheshimiwa Radhia M. Msuya atazungumzia masuala mbali mbali yanayohusu Ubalozi na Watanzania wanaoishi nchini Afrika ya Kusini.

Kufika kwako ni muhimu katika kufanikisha shughuli hii. Tafadhali sambaza taarifa za mkutano huu kwa watanzania wengine unaowafahamu. Akaunti ya jumuiya ni Nedbank Ac.no.1916139183 .

Kwa mawasiliano zaidi piga simu: 0735926045, 0721999833, 0762949049 , 012 344371/012 3425921. Vile vile waweza kupata maelezo zaidi kwa kutuma barua pepe kwenda: watanzaniagp@gmail.com

IMETOLEWA TAREHE: 09.08.2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...