Wachezaji na Viongozi wa timu zote, TBF , Don Bosco na JWTZ.

Timu 4 za Tanzania za Kikapu zimeondoka leo kwenda Kampala, Uganda kushiriki mashindano ya kutafuta bingwa wa kikapu wa kanda ya tano ya Shirikisho la mpira wa kikapu Duniani - FIBA ( FIBA zone 5 Club Championship).

Timu zetu zinazoshiri mashindano hayo ni Savio kutoka Don Bosco ambao ndio Mabingwa wa Tanzania upande wa wanaume na washindi wa pili ABC, na kwa upande wa wanawake ni Jeshi Stars ambao ndio mabingwa wa Tanzania na washindi wa pili ni Don Bosco Lioness.

Kila timu imeondoka na wachezaji 12 na viongozi watatu, mkuu wa msafara ni Kamishna wa wanawake katika TBF, Meja Specioza Budodi (Mrs.), viongozi wengine wa juu wa TBF watakwenda Kampala baade akiwemo Ndg. Alexander Msoffe ambaye ni mjumbe wa bodi ya FIBA kanda ya 5.

Msafara huo uliagwa rasmi na Makamu wa Rais wa TBF ndg. Phares Magesa katika viwanja vya ABC - Chang'ombe leo asubuhi, pia walikuwepo Kanali Busungu ambye ni Mkurugenzi wa Michezo katika JWTZ, Katibu Mkuu wa TBF ndg. Alexander Msoffe na Mkurugenzi wa kituo cha Don Bosco Father Swai.

Kwa sasa bingwa kikapu kanda ya 5 ni timu ya Urunani toka Bunjumbura, Burundi kwa upande wa wanaume na Kenya Ports Authority(KPA) toka Mombasa , Kenya ambao walichukua ubingwa katika mashindano yaliyofanyika Dar es Salaam mwaka jana. Mshindano haya yanashikisha timu 2 za wanaume na wanawake washindi wa juu kutoka katika kila nchi za kanda hii ya 5 inayojumuisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Somalia, Sudani, Sudani ya Kusini, Eritrea na Misri.

Pia mashindano ya kanda ya 5 kwa timu za Taifa mwaka huu yatafanyika Dar Es Salaam Tanzania mwezi desemba, hivyo ushiriki wa timu zetu 4 katika mashindano ya vilabu huko Kampala yatasaidia kuwanoa wachezaji wetu na ni matumani yetu watafanya vizuri na baadae wale watakochaguliwa katika timu zetu za taifa basi pia watatuwakilisha vizuri.

Tunawashukuru sana Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) , Precision Air na wafadhili wengine walisaidia kufanikisha safari hii na kuwezesha kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu Tanzania kupeleka nje timu 4 katika mashindano haya.

Tunaomba wafadhili wengine waendelee kujitokeza kusaidia michezo na hususani mchezo wa kikapu ili kufanikisha malengo yetu na kutumiza wajibu wetu katika jamii yetu.

Tunawatakia kila la heri na tuwaombee Mungu wafanye vizuri katika mashindano haya na kuitangaza vizuri nchi yetu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...