Ofisa Mtendeaji Mkuu wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Said Amir Said akikabidhi zawadi za Sikukuu ya Idd kwa Sista, Mary Grisaldia na Mary Annie kwa ajili ya watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto yatima cha Mama Teresa’s kilichopo Mburahati jijini Dar es Salaam.
Watoto wa Kituo cha kulelea yatima cha Msongola Kivule Kitunda jijini Dar es Salaam, Maria Daniel na Neema James wakipokea sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali vilivyotolewa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Said Amir Said kwa ajili ya Sikukuu ya Idd.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Said Amir Said akiwa katika picha ya pamoja na walezi wa vituo vilivyopewa misaada pamoja na watoto.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Said Amir Said akifafanua jambo kabla ya kukabidhi msaada kwa vituo vya yatima.


Kama hao TTCL wangetaka PR ya aina hiyo ya kugawia watoto misaada na kuwapiga picha, basi angalau wawape na T-shirts za TTCL, watoto wanatangaza Vodacom kwenye hafla ya TTCl, Kaazi kwelikweli.
ReplyDeletemmeiga !!!!! mulikuwa mnatukatia simu nyie wakati wa kutuunganisha mikoani, eti operator kachoka au kaamua kulala tu , au anajaribu mara moja tu halafu anakujibu ,simu yako haipatikani, jeuri,kiburi, kisa nini ??? one company one nation,slogan iliyokuwa siyo ya motisha hata kidogo,slogan ya kiburi wala siyo ya kibiashara, sasa mmeigia ubia na mzungu !! TTCL inaanza kupata faida mpaka inatoa misaada kwa yatima !!! Basi Yesu yuko karibu kuja ,maana imeandikwa kwamba siku za mwisho ,mutaanza kuona maajabu !! ndiyo haya sasa !!! si ajabu kabla ya kutimiza miaka 95 ya uhai wangu, nitasikia Tannesco imefuturisha Watoto walemavu,hii itakuwa mwezi wa Ramadhani wa mwaka 2080. Msikazanie kukamata wahindi na wezi wengine wa umeme ,kwanza safisheni madonda sugu ya wafanyakazi wenu.
ReplyDelete