Ubao ukionyesha namna kila nchi ilivyopiga kura wakati Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, lilipokutana siku ya Ijumaa kulipigia kura Azimio liliwasilishwa na Saudi Arabia. Azimio ambalo pamoja na mambo mengine lilikuwa linajaribu kutoa shinikizo kwa utawala wa Syria kuacha matumizi ya silaha dhidi ya wananchi wake, lakini wakati huo huo Azimio hilo kutoonyesha ukali wowote kwa upande wa Upinzani, vikundi vya kigaidi au nchi ambazo zimekuwa zikiwapatia wapinzani silaha. Azimio hili limepitishwa kwa kupigiwa kura ambapo nchi 133 zimeunga mkono, 12 zimepiga kura ya hapana huku 31 zikipiga kura ya kutofungamana na upande wowote. nchi ambazo zimepiga kura ya hapana na zile ambazo hazikufungamana na upande wowote baadhi zimeeleza kwamba zimechukua hatua hiyo kutokana na ukweli kwamba azimio hilo limeegemea zaidi upande mmoja, lakini pia lilikuwa linaingilia masuala ya ndani ya nchi huru jambo ambalo ni kinyume na sheria za kimataifa.
========= ========= ======== ========
UMOJA WA MATAIFA WAJARIBU TENA KUIBANA SYRIA
Na Mwandishi Maalum
Ikiwa ni wiki mbili zimepita tangu Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa kushindwa kupitisha azimio ambalo lingeongeza kibano kwa utawala wa Syria, jana ( Ijumaa) Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, limepitisha azimio jingine ambalo licha ya kuibana serikali ya Syria lakini pia limeitupia lawama Baraza Kuu la Usalama kwa kushindwa kutimiza wajibu wake ipasavyo.
Azimio hilo ambalo limeandaliwa na Saudi Arabia na washirika wake wengine, limepitishwa ikiwa pia ni siku moja, tangu Bw. Koffi Annan alipotangaza kujiuzulu wadhifa wake wa kuwa Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, na Muungano wa Nchi za Kiarabu katika mgogoro wa Syria. Azimio hilo limepitishwa kwa kupigiwa kura ambapo nchi 133 zilipiga kura ya ndiyo, 12 zikapiga kura ya hapana na nchi 31 zikapiga kura ya kutofungamana na upande wowote.
Pamoja na kupitishwa kwa azimio hilo, lakini linakosa nguvu ya kisheria kwasababu, kwa utaratibu wa Umoja wa Mataifa, mara nyingi maazimio yanayopitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa yanakuwa ya kisiasa zaidi na hayana nguvu kama yale yanayopitishwa na Baraza Kuu la Usalama.Azimio hilo ambalo limeinyosheza kidole zaidi serikali ya iliyoko madarakani kuliko upande wa upinzani. Linaalani vikali pamoja na mambo mengine,matumizi ya silaha nzito ikiwamo mizinga na helikopta za kivita na mauaji holela ya wananchi wasio kuwa na hatia.
Aidha azimio hilo linaitaka serikali iliyopo madarakani kurudisha nyuma vikosi vyake na vifaa vya kijeshi kutoka maeneo ya raia, lakini halitamki lolote kuhusu makundi ya upinzani ambayo nayo yamekuwa yakitumia silaha nzito ikiwa ni pamoja na mauaji.
Awali akizungumza kabla ya kupigwa kwa kura, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, aliwasihi wajumbe wa Baraza kuliunga mkono kwa kauli moja azimio hilo. Akasema kuwa sauti ya pamoja na Baraza hilo inaweza siyo tu kupeleka ujumbe kwa watawala wa Syria lakini pia itaongeza shinikizo la kuwataka watawala na pande nyingine zinazohusika kurejea katika meza ya mzungumzo.
Akasema Ban Ki Moon. “ Mgogoro wa Syria ni mtihani mwingine kwa Umoja wa Mataifa, kwamba, kushindwa kwa Taasisi hiyo ya kimataifa kuutafutia ufumbuzi mgogoro huo ni hatari na hakutatoa ujumbe mzuri”
Akasititiza kwamba Umoja Mataifa usingependa kushuhudia yale yaliyotokea Rwanda au Sebrenica kwasababu tu Umoja huo ulishindwa kuchukua hatua kwa wakati muafaka. Akasisitiza kwamba machafuko na mauaji ya kiholela ya wananchi wasio na hatia nchini Syria yanaweza kuchukuliwa kama ukiukwaji wa haki za binadamu na makosa ya jinai dhidi ya binadamu ambapo wote watakaopatwa na hatia watapashwa kuchukuliwa hatua za kisheria bila kujali ni wa upande gani.
Ban Ki Moon akasema ni jambo la kushangaza na kusikitisha sana kwamba pande zinazopingana zimeamua kutumia njia ya vita kila mmoja akiamini kwamba kwa njia hiyo anaweza kushinda, lakini ukweli ni kwamba hakuna mshindi zaidi ya wananchi wasio na hatia kuendelea kuangamia.“ Sisi sote tuliopo hapa tunawajibika kwa wananchi wa Syria, ni lazima tutumie njia za amani kama zinavyoelezwa katika Katiba ya Umoja wa Mataifa, ili kuaanda mchakato wa upatikanaji wa amani ambao utawahusisha wananchi wenyewe wa Syria”. Akasisitiza Ban Ki Moon.
Nchi ambazo zimepiga kura ya hapana au ya kutofungamana na upande wowote baadhi zilieleza kwamba zimefanya hivyo kwa sababu moja kuu ya msingi ambayo ni, Azimio hilo lilikuwa limeegemea upande mmoja, lakini pia zilikuwa zinapinga uingiliaji wa mambo ya ndani ya nchi nyingine jambo ambalo ni kinyume si kama inavyoelezwa katika Katiba ya Umoja wa Mataifa bali hata katika sheria mbalimbali za Kimataifa.
Aidha nchi nyingine zimeeleza bayana kwamba hazikuunga mkono azimio hilo kwa kuwa, wakati mataifa mengine yamejikita katika kuilamu na kuilaani serikali ya Syria, lakini zilikuwa hazisemi lolote kuhusu baadhi ya mataifa ambayo yamekuwa yakisaidia kwa hali na mali ikiwa ni pamoja na kuvipatia silaha vikundi vya upinzani hali ambayo imechochea zaidi mgogoro huo badala ya kuutatua.



Kabla ya Umoja wa Mataifa (United Nations Organization) tuliokuwa nao leo dunia ilikuwa na League of Nations, umoja/ushirika huu ulindwa kutuliza amani ya mataifa ambayo kimsingi ndio jukumu kubwa la uanzish=shwaji wake. Ilivyokuwa UNO nayo jukumu hilo imeshindwa kulitekeleza sasa kuna haja kubwa (sio choo) ya kuanzishwa umoja mwingine wa mataifa ambao utatupilia mbali masuala ya kura ya veto! Hivi leo Syria inashambuliwa na waasi wenye silaha ambazo zinatolewa na Marekani lakini yenyewe inaambiwa eti iache kuwashambulia hao waasi,yaani iache kujilinda, sasa wafanyeje? Huu si ni upuuzi jamani?
ReplyDeleteHaswaa ni upuuzi, miye hata sielewi malengo ya hawa wakubwa. Somalia walikuwa na amani mwaka 2006, marekani kwa kuwa waliokuweko madarakani kipindi hawakuwa vibaraka wao wakawatumia Ethiopia kusambaratisha nchi. Sasa wanasema kuna al-shaabab, wakati hawa ni wale ambao walikuwa wameunda serikali mwaka 2006 na ambao marekani hawakuwataka.Nasikia pana mafuta na gesi hapo somalia na waheshimiwa wameshaanza kuyafanyia kazi.Sielewi siye hapa nchini kwetu tutakaposema wazee faida izidi sisi kwani ni masikini kuliko nyie na nyie matajiri sana..., sijui kama hawatasema Tanzania ni nchi ya kishenzi... na kutaka kuivamia...
ReplyDeleteaMERIKA INACHOCHEA WA-sYRIA WAUANE BURE BADALA YA KUWAKUTANIISHA KWA SABABU WANATAKA REGIME XHANGE! eTI REGIME CHANGE.! hAWAMTAKI HUYO rAIS WA sYRIA TU NA WANAMWUA KWA NJIA ZOZOTE. sASA ciaNDIO WANAOPIGANA VITA HIYO!
ReplyDeleteNa sisi tusipotaka ushoga watatuvamia. Dunia imeisha!!!!!"""
ReplyDeleteChange ime fika Tanzania. Mambo yana badlika kidogo dogo watu wame lala. Una ona vipi Rais na safari zake za kisiri siri Merikani. Ufisadi tu. Sasa hana laku sema.
ReplyDelete