Ankal!
NAOMBA UNISAIDIE KUSAMBAZA HII KWA NDUGU ZANGU WAPENDWA. HARUFU YA KIKWAPA IMEKUA TATIZO KUBWA KWA JAMII YETU NA WATU WENGI WAMEIZOEA HIYO HARUFU KIASI KWAMBA HAWAJITAMBUI KUA WANATOA HARUFU. WATU WENGI WA NCHI ZA NJE WAKIJA TANZANIA WANALALAMIKA KUA HARUFU YA KIKWAPA INAWASUMBUA.
 
HARUFU YA KIKWAPA INATOKANA NA SABABU NYINGI KAMA USAFI WA MWILI, CHAKULA (KAMA RED MEAT). MTU ANAPOTOA JASHO, BACTERIA WANATUMIA NAFASI HIYO KWENDA KWENYE JASHO KUJIPATIA CHAKULA. KADRI BACTERIA WANAVYOKUA WENGI, HARUFU NAYO INAZIDI. KUOGA KUNASABABISHA BACTERIA KUONDOKA HASA KAMA UNATUMIA SABUNI INAYOUA HAO BACTERIA (ANTISEPTIC SOAP). BACTERIA WANAOKAA KWENYE KIKWAPA WANAZIDI PIA KAMA UNATUMIA KITAULO CHA KUOGEA NA KUTOKUKIFUA VIZURI NA KUACHA KISIKAUKE. HIVYO UNASHAURIWA KUKIANIKA NJE KIKAUKE BAADA YA KUOGA, PAMOJA NA TAULO YA KUJIFUTIA ILI VIONDOKANE NA BACTERIA AU KAMA INAWEZEKANA KUFUA KILA SIKU.
 
KWA SABABU MTU HAWEZI KUSHINDA ANAOGA SIKU NZIMA NI BORA KUTUMIA NJIA ZA KUKINGA HARUFU YA KIKWAPA. NJIA HIZO NI KAMA ZIFUATAZO:
 
1.     KUTUMIA DEODORANTS AU ANTIPERSPIRANTS. DEODORANTS ZINASAIDIA KUONDOA BACTERIA AMBAO WAKO KWENYE KIKWAPA. MARA NYINGI HUA ZINA HARUFU NZURI NA KUNA AMBAZO HAZINA. KAZI YAKE NI KUFANYA BACTERIA WASIKAE KWENYE KIKWAPA. ANTIPERSPIRANTS ZINAZUIA JASHO LISITOKE KWA WINGI. UNAPOENDA KUNUNUA DEODORANT ANGALIA YENYE INGREDIENT INAYOITWA ALUMINIUM CHLOROHYDRATE.
 
2.     KUTUMIA BAKING POWDER. HII NI NJIA RAHISI ZAIDI AMBAYO INATUMIA GHARAMA NDOGO ZAIDI. KUNA PACKET YA BAKING POWDER AMBAYO INAUZWA BEI CHINI YA SHILLING MIA NA ITADUMU KWA MUDA HATA WA MIEZI MITATU. WEKA KIDOGO KWENYE KIGANJA, CHANGANYA NA MAJI  HALAFU PAKA KWENYE KIKWAPA BAADA YA KUOGA. HII ITAZUIA HARUFU YA KIKWAPA SIKU NZIMA.
 
3.     VAA NGUO ZA KITAMBAA CHA COTTON AU WOOL. NINA MAANA KWAMBA NGUO AMBAZO NI SYNTHETIC KAPPA POLYESTER AU NYLON ZINAFANYA MTU ATOE JASHO ZAIDI.
 
4.     NYOA NYWELE ZA KIKWAPA. NYWELE ZIKIWA NYINGI ZINAKUA KAMA MTEGO WA BACTERIA NA KUSABABISHA HARUFU.
 
5.     KUNYWA MAJI MENGI. MAJI YANASAIDIA KUTOA SUMU KWENYE MWILI NA KUSABABISHA HARUFU KUPUNGUA.
 
6.     OGA ANGALAU MARA MBILI KWA SIKU NA KUSUGUA VIZURI SEHEMU YA KIKWAPA.
 
7.     VAA NGUO SAFI KILA SIKU.
 
8.     HAKIKISHA HUNA HARUFU YA KIKWAPA KABLA YA KUTUMIA PERFUME KALI. MCHANGANYIKO WA HARUFU YA KIKWAPA NA PERFUME INATOA HARUFU MBAYA ZAIDI.


 ASANTE SANA,
MdaU 
RAHELI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Una kazi wwe,
    mdau paris

    ReplyDelete
  2. Naomba michu au mdau atuletee na tiba ya harufu ya kinywa.

    ReplyDelete
  3. Mdau, ni baking Soda na sio Baking powder. Rekebisha hapo usije kuwachanganya watumiaji

    ReplyDelete
  4. Sasa jamani, KUKOGA MARA MBILI KWA SIKU, MAJI YENYEWE YAKO WAPI? AU TUTUMIE MCHANGA.

    ReplyDelete
  5. Bora maana waweza kuona mtu na heshima zake na uwezo wa kununua deudorant anao lakini akikusogelea mmmmmh! HASA WANAUME

    ReplyDelete
  6. Kikwaba ni suala nyeti kwa sisi na hata bloggers ? Kimesikika DSM,Paris,DC,London,na hata NY ? WaTZ tuamke.

    ReplyDelete
  7. hii matata lazima kitoke Je na harufu ya kinywa nayo vipi hapo

    ReplyDelete
  8. Mdau Raheli, hiyo yooote uliyosema ni tisa,yaani nina maana ya kwamba ,umesahau kitu mhimu zaidi. Naama wasomaji, harufu inayokera zaidi ni harufu mbaya inayotoka kwenye sehemu za siri za baadhi ya wanawake wetu.Hii Raheli ndiyo angeizungumuzia kwanza tena kwa undani zaidi, achana na kwapa kwa vile madhara yake ni madogo sana .Tuambie huko chini vipi ?? huo uvundo unatisha na ni aibu kubwa sana.Raheli ,usiogope wewe toboa siri na utaokoa ndoa zetu.Zebedayo msema kweli

    ReplyDelete
  9. umelenga wewe manake daladala za bongo full kikwapa noma

    ReplyDelete
  10. Sasa mdau, huyo mtanzania wa hali ya chini anao uwezo wa kuoga mara 2 kwa siku?na kuvaa nguo safi kila siku na maelezo mazuli sema tuwaaachie watendaji kama wataweza na wengi wao ni watu wa hali ya chini hao na mkumbuke mambo mengi ya manukato ya rahisi sio yenyewe ni (look like)feki nafikiri nayo yanachangia pia,sema ndio tujitahidi kuelimishana kila upande.

    ReplyDelete
  11. There is nothing worse that a beautiful girl trying to cover up the bad smell by heavy perfumery.

    ReplyDelete
  12. Pia unweza kusugua nandimu hii nimujarab mkonokwamkono.
    Tatizo litakuwa limekwishwa.

    ReplyDelete
  13. kweli maneno yako, hujakoseaika ua nilipof hili suali ni kweli. nilikunduwa nilipofika dar seaport.

    ReplyDelete
  14. ALuminium chlorohydrate pia ina side effect hhasa kwa wenye sensitive skin. Ndio chanzo cha eczma na other skin conditions. Sio kila mmoja itamfaa. Zipo baadhi ya annti perspirant zisizotumia alchol au aluminium ambazo ziko safer zaidi kwa mtu mwenye sensitive skin au kwa wale walio na tatizo la ellergies nazo zimekuwa labelled kama ni natural deodorant crystal ambazo zinawekwa potasium rather than aluminium..ziko nyengine zinazotumia ammonium..ni vyema kujuwa skin yako na sensitivity yake na hizo ingredients then kufanya inform choice isio na madhara kwa ngozi yako...

    ReplyDelete
  15. Sisi masela tunaita kindim ndim..hakina jinsia kipo kotekote..kwa wakakaz na wadadaz..angalizo kwa wadau..hakina dawa...dawa ni kuoga kwa sana..na kupulizia kikata ndim ambacho kinaitwa pafu pafu kwa luga ya hapa uk..ukiwa unaitumia unasikia inafanya fuuu fuuuu..zaidi ya hapo utaibiwa tu..naitwa tajiri wa mawazo endelevu..sikusoma ila naona mbali...amani kwa wadau wote.

    ReplyDelete
  16. Unaposema "...watu wengi wa nchi za nje wanapokuja TANZANIA wanalalamika kua harufu ya kikwapa inawasumbuwa."

    Unataka kutwambia nchi yetu ndio producer wakuu wa harufu ya kikwapa au umekusudia nini hapo? Kama ni kwa sababu ya joto, basi ukanda wote wa equator ni nchi zenye joto kali na sio TZ tu, yawezekana hao wanaokuja na kukumbwa na kashfa hiyo ya kikwapa, pengine hawajishughulikii unadhifu wa miili yao, pia yawezekana kwa baadhi wengine ni kama maradhi (kunuka kikwapa muda wote), hata watumie kitu gani unakuta vikwapa vyao bado ninatowa harufu.

    Ila hongera sana kwa kutupatia somo zuri na lenye manufaa na khasa kwa kutufahamisha sababu za kikwapa na jinsi ya kuzitafutia suluhu, shukran.

    ReplyDelete
  17. Harufu ya kinywa ( Hallitosis) 1)Piga mswaki angalau mara 3 kwa siku baada ya mlo.2) Hakikisha unapiga mswaki kwenye ulimi pia.3)Tumia mouth wash itaua bacteria kwenye mdomo. 4)Acha kula vitunguu saumu au vitunguu vibichi ambavyo havijawekwa ndimu. Yangu hayo machache mwenye kuongeza aongezee.
    Naongezea moja kwenye usafi wa kikwapa nunua ndimu na isugulie kwapani. Inasaidia kutoa harufu.

    ReplyDelete
  18. Harufu mbaya ya kinywa yaweza kusababishwa na afya mbovu ya meno. Pia vinyaji na chakula kama vile beer za kienyeji na pia tumbo chafu. Tumia haluli.

    ReplyDelete
  19. Ni kweli harufu ya kikwapa,Na ya mdomo na sehemu nyingine za mwili zinakera sana!mimi ninatoa ushauri ktk TV na magazeti yetu wangekuwa wanaelimisha wananchi jinsi ya kutumia vitu kama deodorant n.k,maana watu wengine hawajui matumizi yake wala hawafahamu kuwa kuna kitu kinaitwa deodorant!

    ReplyDelete
  20. Afadhali HK umeona!

    sesophy

    ReplyDelete
  21. USAFI WA SEHEHU ZA SINI KWA KINA MAMA NI MUHIMU SANA. OGA KABLA YA KWENDA KULALA NA UZISAFISHE SEHEMU HIZO KWA MAJI NA VAGINA DOUCHE. HII INASAIDIA KUTOA HARUFU. USIOGOPE KUTUMIA MKONO KUSAFISHA NYETI ZAKO VIZUURI. USIFUGE NYWELE SEHEMU HIZO NYOA NI RAHISI KUSAFISHA UKIWA UMENYOA, KUNA NYEMBE NZURI ZA KINA MAMA SIKU HIZI RAHISI TU DAKIKA TANO KWISHA. HATA NYUMBA YA KUPANGA UNANYOA MARA MOJA KWA WIKI JUMAPILI NI SIKU NZURI. KUOSHA NYETI NI KILA USIKU.

    ReplyDelete
  22. Kwa wale wenzangu na mie ambao bei ya deodorant ni tatizo kwetu, chukua sufuria ambayo imepikiwa ugali wa mahindi, baada ya kutoa huo ugali, weka maji ndani ya sufuria hiyo na yaache yalale kwa siku moja, baada ya hapo paka maji hayo yaliyolala kwenye kwapa. Fanya hivyo kwa muda wa siku mbili au tatu... harufu yote ya kikwapa itatoka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...