Viongozi watatu wa ngazi ya juu wa Serikali ya Mkoa wa Katavi wametapeliwa na watu wasiojulikana baada ya kuelezwa kuwa wameshinda promosheni ya Airtel ya Shilingi milioni 50.

Waliotapeliwa ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajabu Rutengwe, Katibu Tawala wa Mkoa, Emmanuel Kalobelo na Mganga Mkuu wa Mkoa, Yahaya Hussein.

Viongozi hao walitapeliwa kwa nyakati tofauti na watu waliojitambulisha kwao kwa simu kuwa ni watumishi wa Kampuni ya Simu ya Airtel.

Tukio la kwanza lilikuwa ni la Mkuu wa Mkoa kuambiwa ameshinda zawadi ya Sh. milioni 50 na aliombwa awatumie namba za simu za watu watano aliozungumza nao mara ya mwisho na baada ya kufanya hivyo simu yake ya mkononi ikafungwa na matapeli hao.

Akieleza mkasa huo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Yahaya alisema yeye baada ya kupigiwa simu na matapeli hao hakuwa na shaka nao kutokana na kauli yao ilivyokuwa ya ustaarabu. Alisema baada ya kuwapa majina ya watu watano alizungumza nao mara ya mwisho kwenye simu yake na kuombwa awatajie namba zake za siri za akaunti ya Benki ya NMB ili wamtumie zawadi ya Sh. milioni 50. Baada ya kuombwa namba yake ya siri, Dkt. Yahaya hakuwa na shaka yoyote na hivyo akawapatia namba hiyo ya siri. Hata hivyo hakuweza kuibiwa fedha zozote kwa vile akaunti yake haikuwa na salio la kutosha.

Meneja wa Wawi la NMB Wilaya ya Mpanda, Erick Luhanda alisema amepokea malalamiko kutoka kwa viongozi hao. Alisema kiongozi wa mwisho kumpa taarifa alikuwa ni Katibu Tawala wa Mkoa, Kalobelo. Luanda alisema tayari taratibu za kibenki zimefanyika hivyo hakutakuwa na hujuma kwenye akaunti za viongozi hao.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari alithibitisha kutokea matukio hayo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Utapeli huu ulikuwa unafanywa na Wanaigeria miaka ya 80 na 90 na ukapitwa na wakati, sasa kwa viongozi hawa kuingizwa mkenge wa wazi wazi namna hii !!! basi kama ningelikuwa naishi mkoa wa Katavi,ningeuhama kabisa na huo mkoa.Kuongozwa na viongozi wa namna hii duh !!!. Na yote hii tamaa ya kupata kiurahisi.Kwanza fikiria hiyo kampuni ya simu,ina uwezo upi wa kuzawadia watu million 50 ??? kwa biashara gani ??? wangeanza na million moja ,hapo labda ,lakini dau kubwa namna hiyo ??? hata mtoto mdogo angeshituka.

    ReplyDelete
  2. Sasa mwandishi mbona ktk habari yako sijaona sehemu inayoonesha hawa viongozi kutapeliwa?au neno tapeli lina maana gani wadau?

    ReplyDelete
  3. mimi nashauri serilaki ifutilie mbali hii kampuni mpya ya kitapeli iliyokyja nchini.hawa jamaa wanauza software ambazo ukinunua basi unakuwa na uwezo kusikiliza mazungumzo na kupokea message za mtu yoyote yule.hii ni hatari sana yani mtu anakuwa na uwezo wa kuaccess details zako wakati wowote ule.uncle hawa jamaa wapo ppf tower.nawakilisha

    ReplyDelete
  4. loooo !!! na wewe ,basi utakuwa wale wale wanaobeba mabox Uturuki maana wameondoka baada ya kuogopa umande wa shule, hebu sema ,nini usichokielewa hapo ? umeambiwa , wamepigiwa simu na watu waliojifanya wako kampuni ya simu,kumbe siyo. Hapo kwa mtu angalau mwenye darasa la 3 atakuwa kisha elewa. Na maana ya utapeli ni kumchota mtu akili na ukampokonya mali zake kwa njia ya kitapeli ( udanganyifu) Utapeli mwingine unakuwa mgumu kuugundua hasa kama utalenga kwenye weak point za mwanadamu ( yaani Pesa) hapa inabidi uwe na elimu kidogo angalau darasa la 7,lakini kama una cheti kikubwaa cha phd kumbe umekipata kwenye computer na kukiprint !!! hapa wewe bado,huna elimu .Hivyo kulizwa kama hivi, ni halali kabisa.Zebedayo msema kweli

    ReplyDelete
  5. Kuna nchi kule South American countries ukipigwa poketi, wanakuzomea kuwa wewe ni mpumbavu. Hawa jamaa kuambiwa wameshida zawadi na watoe namba ya akaunti ya benki na pasiwedi, na wakafanya hivo, yashangaza, nilitaka kusema wastahili wazomewa.

    ReplyDelete
  6. Mdau hapo juu ckubaliani nawe, pesa sio weak point ya mwanadamu, ni baadhi ya watu tu kwa tamaa zao kutaka kuvuna pale asipopanda. Anayetapeli, na anayetapeliwa ni walewale kutaka kula pale asipomwagilia!! Wewe hujacheza bahati na sibu, hiyo mil 50 ya bure utaipataje??

    Ila spidi ya kutaka vya bure ikiendelea kwa kasi hii hapa TZ, basi tutawafanya watakatifu wale waliopita hapa bila kutaka vya bure au kuiba hazina za nchi!!

    ReplyDelete
  7. Hawo ndio viongozi wetu wa Bongo bwana...vilaza ile mbaya.Mtu mwenye kujitambua hawezi kumpa mtu yyt password yake hata mfanyakazi wa bank hapaswi kuijua sasa mtu km Mkuu wa Mkoa na katibu Tawala wanafanya uzembe km huo tutegemee nini?Hawa hawapaswi kupewa madaraka km haya kwa sababu upeo wao wakufahamu mambo ni mdogo watawezaje kusimamia mambo makubwa na nyeti ynayogusa maslahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla?
    Wadau huu mtinfo wakupeana vyeo kwa misingi ya ujama,ukabila na kujuana unauwa nchi,watu wanaotapeliwa kizembe namna hii itakuaje pale watakapokuja matapeli proffesionls na gear za uwekezaji?Lazima tuwe na watu makini kuanzia balozi wa nyumba 10 mpaka rais la sivyo nchi yetu pia itaibwa nzima nzima.

    ReplyDelete
  8. Naomba tupate funzo moja muhimu sana hapa katika utapeli huu:

    USIMPE MTU YE YOTE USIYEMJUA NAMBA YAKO YA SIRI KWA KUPITIA SIMU AU MTANDAO.

    Funzo hili kila siku tunaambiwa lakini sisi ni binaadamu ukiambiwa umeshinda tu basi roho imeanza kupiga mahesabu ya fedha hizo, na hapo ndipo unapoingia mkenge.

    Poleni sana muliofikwa na mikasa hii.

    ReplyDelete
  9. Inaitwa "namba ya siri" for a reason, ukimpa mtu yeyote mwingine hiyi namba,basi hiyo siyo namba ya siri tena, jamaa wamepigwa changa la macho laivu, I don`t feel sorry for them at all, it is through their utter stupidity and greediness that they got duped.
    Dr Gangwe Bitozi

    ReplyDelete
  10. Zebedayo,
    Watu wameondoka tanzania kuepuka kuendeshwa na viongozi kama hawa waliotapeliwa. Ni tamaa tupu ndiyo iliyowapelekea kutapeliwa, itakuwaje utowe number yako ya siri ya akaunti yako kwa mtu usiemjua, ila tu kwambia umeshinda milioni? Sharti moja na la muhimu unaloambiwa kuhusu number yako ya siri kuwa iwe siri yako, huhitaji kumpa mtu number yako ya siri ili akuwekee pesa kwenye account yako.
    Hawa jamaa ambao wewe ndio unaowaona viongozi maridadi akili zao ziliruka mara tu baada ya kusikia neno milioni, na ndio kawaida yao kwa kila maamuzi wanayofanya kila siku.

    ReplyDelete
  11. Ukisikia kucheze sharubu za Simba ndio huku!

    Ahhh watu majasiri sana, hadi Mkuu wa Mkoa (Raisi wa Jimbo) anatapeliwa?

    Haya ndio yale ya kumchinja kobe kwa 'timing' na ndio sasa hapa utathibitisha kuwa Bongo ni tambarale!!!

    ReplyDelete
  12. Mkuu wa Mkoa kaingizwa kingi?

    Hapo ndio pale unakuta tembo anauwawa kwa kutegewa siafu katika maji mtoni wanakokunywa.

    Wakija tembo kunywa siafu wanazama katika mkonga na pua na kutembea ndani ya mkonga na ndipo tembo atapata ghadhabu anakimbia akiupigiza mkonga wake kwenye miti na majabali ili kuwakung'uta na kuwatoa, na huku siafu wasitoke kwenye mkonga wake hadi anajiua mwenyewe!

    ReplyDelete
  13. Jamaa hawa Matapeli ni wakata vimeo:::

    Mkasi wa ngariba hauna ujanja, omba uwe umeshapita ama usirudishwe kimakosa kama vile hujaonana nae!

    ReplyDelete
  14. This is interesting, huku ni kutokwenda shule, hivi mkuu wa mkoa anashindwaje kutambua sheria za michezo hiyo? kama mtu kashinda anaambiwa aende kwenye ofisi za kampuni husika ili aweze kukabidhiwa hundi yake au kupewa taratibu za namna ya kupata kitita chake. Hivi password inahusiana nini na mi 50? kwa sababu password haihitajiki kwenye kudepost any cash, hawa waheshimiwa wanatakiwa kusikia aibu kwani inaonesha dhahiri kuna mapungufu fulani kwenye elimu zao.

    ReplyDelete
  15. Mimi nauliza hao waheshimiwa walipoambiwa kwamba wameshinda wao walikua wamecheza huo mchezo au kwa vile kitita cha pesa kilitajwa basi wao wakaamini zilishuka kama mana kule jangwani.
    Pole zao na liwe fundisho kwa wengine kwamba uwezi kushinda zawadi kama ujaingia kwenye mashindano na numba ya accounti yako ni siri yao wewe mwenyewe.

    ReplyDelete
  16. You have to be the dumbest of the dumbs to fall for that. Lete namba ya siri ya benki na wewe unatoa tu? Imagine folks like these watumwe kwenda kunegotiate mikataba kwa niaba ya taifa...! Lord have mercy!

    ReplyDelete
  17. KAMA KIONGOZI ANAFANYIWA HIVI NA ANAINGIA MKENGE KWA KIURAHISI JE MWANANCHI WA KAWAIDA ITAKUAJE MAANA KIONGOZI HUJUI MAHUSIANO YA NAMBA YA SIRI NA KUTUMIWA HELA (NA HAWA WATU KWA TITLLE ZAO WAMESHAFANYA TRANSACTION NYINGI TU BINAFSI NA ZA OFISI), BORA WANGEIBIWA TU HAWA JAMAA MAANA KUSIKIA 50MILLION AKILI ZIMEWARUKA MPAKA MITEGO MIDOGO YA PASSWORD WAMESHINDWA KUGUNDUA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...