Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uamuzi wa Serikali wa kuwafukuza  kazi  watumishi watatu wa wizara hiyo kutoka na ukiukaji wa sheria na utekelezaji wa majukumu yao ya kazi kufuatia sakata la usafirishaji wa wanyama pori  kupitia Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro kwenda Quatar. Picha na Anna Nkinda wa MAELEZO

Wizara ya Maliasili na Utalii imechukua hatua za kinidhamu kwa watumishi wake tisa (9) kufuatia kadhia ya utoroshaji wa Wanyamapori hai katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na masuala mengine yanayohusu Wanyamapori. Watumishi hao wamechukuliwa hatua husika kufuatia kukamilika kwa uchunguzi wa tuhuma zilizokuwa zikiwakabiri.

(1) Waliofukuzwa kazi kutokana na ukiukaji wa sheria katika utekelezaji wa majukumu yao ni:

    - Bw. Obeid F. Mbangwa         -    Mkurugenzi wa Wanyamapori. Wakati wa kadhia hiyo alikuwa             Mkurugenzi Msaidizi Matumizi ya Wanyamapori,

     - Bw. Simon Charles Gwera – Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii – CITES na Utalii wa Picha Arusha,

     - Bw Frank Mremi - Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii – CITES na Utalii wa Picha Arusha.

(2) Aliyeondolewa Cheo cha Madaraka kutokana na kutochukua hatua kamilifu za ulinzi ambazo zingeweza kuzuia kutokea kwa tukio la utoroshwaji wa wanyama ni:

    - Bw. Bonaventura M.C. Midala – Mkurugenzi Msaidizi, Undelezaji Wanyamapori. Wakati wa tukio alikuwa Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Kuzuia Ujangili.

(3) Wafuatao ni Maafisa Wanyamapori Daraja la II waliotekeleza maelekezo ya Wakuu wao wa kazi yaliyo kinyume cha Sheria ambao wamepewa Onyo Kali la Maandishi:

  - Bibi Martha P. Msemo       -        Afisa Leseni, Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha Arusha.

    - Bibi Anthonia Anthony – Afisa Leseni, Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha Dar es Salaam.

(4) Bw. Silvanus Atete Okudo ni Mkuu wa Kituo cha Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha Arusha aliyeshindwa kufuatilia kupata maelekezo ya Mkurungezi wa Wanyamapori kuhusu mtumishi wake aliyekiuka Sheria katika utoaji wa vibali. Aidha, alishindwa kupeleka kwa Katibu Mkuu taarifa kuhusu mtumishi huyo ili achukuliwe hatua za nidhamu.

    - Silvanus Atete Okudo – amepewa Onyo Kali la Maandishi.

(5) Wafuatao ni Maafisa ambao uchunguzi dhidi yao unaendelea:

    - Bw. Mohamed Madehele – Ofisi ya Matumizi Endelevu ya Wanyamapori

    - Bibi Mariam Nyallu – Kituo cha Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha – Arusha.

Wahusika wengine katika kadhia hiyo wasiokuwa waajiriwa wa Wizara ya Maliasili na Utalii watachukiliwa hatua na mamlaka nyingine husika.

Mhe. Khamis Suedi Kagasheki

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII

13 Agosti 2012

 (Imetolewa kwenye Press Conference iliyofanyika Katika Viwanja vya Bunge Dodoma tarehe 13 Agosti 2012)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Wanafukuzwa tu,je pesa yetu ipo wapi?
    Tunataka walipe pesa yetu waliouzia hao wanyama,serikali ikamate mali zao kufidia ,liwe fundisho kwa wengine.
    je viongozi/wanyakazi wa airport walioshiriki wapo wapi?
    Tunaomba iwe hivi kwa vitengo vyote vya serikali,hii ni mali yetu wote na ni kwa manufaa ya wote.

    ReplyDelete
  2. Safi sana muheshimiwa. Fagia faigia labda tutabahatika kubaki na wanya pori waliobaki badala ya kuletewa kutoka nje. Na huo uwe ni mwanzo tu wengine waanze kutia maji!

    ReplyDelete
  3. wote wesi hao bana kagasheki, fukusia mbali hao bana

    ReplyDelete
  4. Kufukuzwa isiwe mwisho wapelekwe mahakamani kwa uhujumu uchumi.

    ReplyDelete
  5. Hongera waziri wetu

    ReplyDelete
  6. Mlolongo Uko hivi: Mawaziri kadhaa wanatuhumiwa kwa ufisadi na kutokuwa makini(unakumbuka kiwanja alichouziwa Mohamed Entreprises na madudu ya TANESCO?)---Wabunge wanachachamaa, Zitto anakusanya saini za wabunge kupiga kura ya kutokuwa na Imani na Waziri Mkuu na ajiuzulu au amshauri Rais awawajibishe mawaziri----Waziri Mkuu hajiuzulu, Raisi analazimika kuwafukuza mawaziri na kurekebisha baraza la mawaziri---Anapowatangaza wapya anasema walioondoka wasiende peke yao, bali na wakurugezi/wakuu wa Idara na Mashirika walioharibu kazi pia waondoke----wanaondolewa Uchukuzi, Nishati na Madini, Maliasili na Utalii---, stori inaendelea.

    Somo: 1. Upinzani una faida kwasababu unaweza kusababisha mabadiliko kwanyoosha wanaotuangusha
    2. Rais akitaka ana uwezo wa kunyoosha mambo. Tafakari.

    ReplyDelete
  7. Mwakyembe,Magufuli,Kagasheki. Mawaziri watatu katika Baraza la watu lukuki. Hao wengine kwa nini wasiachie tu ngazi;wanafanyaga nini maofisini?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...