Wazalishaji wa mazao ya nafaka kutoka Wilaya ya Singida wakimpatia maelezo mgeni rasmi wa uzinduzi wa sherehe za Wakulima nane nane Kitaifa mkoani Dodoma Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa niaba ra Rais wa Zanzibar Dr. Sheni jinsi ya uzalishaji wa mazao hayo Kitaalamu.
Waziri wa Mifugo na Uvuzi wa Zanzibar Mh. Abdillah Jihadi Hassan aliyevaa suti nyeupe akiuliza swali kwa mtaalamu wa utengenezaji wa boti kutoka shirika la Uvuvi la Mwanza . Kati kati ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ambaye ni mgeni rasmi wa sherehe za Wakulima nane nane kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohd Shen akifuatilia ufafanuzi wa jibu la swali hilo. Kushoto ya Balozi ni Naibu Waziri wa Kilimo na Mifugo wa Tanzania Bara Mh. Adam Malima. 
Wataalamu wa Kituo cha sana za Kilimo Arusha { Camartec } wakimpatia Maelezo Balozi Seif Ali Iddi ya usanifu na utengenezaji wa vifaa mbali mbali kwa ajili ya matumizi ya taasisi, Vikundi vya ushirika pamoja na jumuiya za uzalishaji mali. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif, Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar Mh. Jihad Hassan pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo na Mifugo wa Tanzania Bara Mh. Adam Malima  wakipatwa na butwaa kwa jinsi wajasiri amali wa manispaa ya Singida walivyokuwa mahiri katika kusarifu Boga kwenye mapishi tofauti ikiwemo   pia Keki.
Kikundi cha Utamaduni cha Vijana wanaojiita Form Six wakitoa burdan katika uzinduzi wa sherehe za Wakulima nane nane katika uwanja wa nzuguni Dodoma ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohd Shen.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Nimelipenda sana jina lao, eti Form Six lol

    ReplyDelete
  2. Vijana wa Form Six :

    wananikumbusha Mganda-Nyasaland, ngoma ya Kinyasa

    ReplyDelete
  3. Zidumu fikra za Mhe. Rais, kwa kuanzish shera ya Kilimo Kwanza.

    ReplyDelete
  4. Kinyasa,

    One step, One step, One step!

    Pre, pre, pre, pre!

    Ni ngoma ya kishua sana unatakuiwa ucheze huku una kitambaa mkononi cha kufutia jasho.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...